Tangazo

Pages

Monday, February 1, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI APIGIA MKWALA MZITO MWINYI MZENGELA KUPIGANA PASAKA


Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amemchimbia mkwala mkali bondia Mwinyi Mzengela watakapokutana siku ya April 26 katika sikukuu ya Pasaka 

Mbilinyi amemtangazia kiama Mzengela baada ya kukubali kupambana nae katika uzito wa KG 63 amesema nitamsambalatisha mapema mno bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa KG 63 kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC)
Mbilinyi aliongeza kwa kusema namuheshimu Mzengela kwa kuwa ni bingwa wa Taifa ata hivyo nita akikisha nausambalatisha utawala wake na mimi nakuwa juu yake kwa kuwa nia ninayo uwezo ninao na nitaonesha jinsi ngumi zinavyochezwa  

najuwa katika ngumi za kulipwa sina mda mrefu sana na nimeshatambulika kwa kuwa najua nini nakifanya katika mchezo uhu wa masumbwi nchini

nimeingia katika ngumi za kulipwa sio kupoteza mda kwa kuwa najua mchezo wa ngumi ila kwangu mimi ni ajira na ndio ninayo itegemea

MABONDIA MOHAMEDI MATUMLA NA COSMAS CHEKA WASAINI KUZITWANGA SIKUKUU YA PASAKA

Bondia Cosmas Cheka akipokea mkataba wake wa kuzipiga na Mohamed Matumla siku ya sikukuu ya Pasaka kutoka kwa mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kutiliana saini ya kuzipiga siku ya sukukuu ya Pasaka katikati ni mdau wa masumbwi nchini Abdallah Mwasora Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto ambaye ni mklatibu wa  mpambano wa bondia Mohamed Matumla kulia atakaepambana na Cosmas Cheka akikabidhiwa mkataba wake pamoja na sehemu ya malipo ya mchezo wake utakaochezwa siku ya  sikukuu ya Pasaka jijini Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Mohamed Matumla  akisaini mkataba wake wa kuzipiga na Cosmas Cheka siku ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akimwesabia kiasi cha fedha ambacho alikabidhiwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake



Bondia Cosmas Cheka kushoto akitia saini mkataba wa kuzipiga na Mohamed Matumla mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka kulia ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Cosmas Cheka kushoto akihesabu sehemu ya fedha zake kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Mohamed Matumla utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka  kutoka kwa mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D'  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Cosmas Cheka na Mohamed Matumla wamesaini kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka uzito wa kg 61 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa

akizungumza baada ya kutiliana saini ya mikataba kwa mabondia hawo

Mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema nimewasainisha mabondia Mohamed Matumla atakaezipiga na Cosmas Cheka ata hivyo nipo kwenye mazungumzo na mabondia Fadhili Majia na Nassibu Ramadhani ambao nilikuwa ningie nao mikataba ata hivyo kambi hizo mbili wametofautiana kiswahili kuusiana na mikataba hiyo ata hivyo naendelea kushawishi kambi zote mbili ziwe katika msimamo ambano tumekubaliana ili tufanye kazi

mana tulikuwa tusaini mpambano uho leo rakini mezani nilikuwa na kambi moja tu ya Ramadhani hivyo atukuweza kuelewana na kambi ya Majia

wakati uho uho bondia Vicent Mbilinyi atatwangana na Mwinyi Mzengela katika mpambano wa raundi nane uzito wa kg 63 

na bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atakumbana na Twaha Kiduku mpambano wa raundi nane uzito wa kg 63


siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali




Friday, January 29, 2016

BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA UWANJANI FEB 26 AUSTRALIA







BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine  feb 26 akizipiga na  Michael Camellion kutoka Philippinesa  mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title  utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
 
Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
 
bondia huyo mtanzania anaefanya shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho 
 
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA 
 
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana 
 
na akishinda mchezo uho itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya feb 26
 
Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D' 
 
Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga 
 
ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake ndipo kilipozikiwa
 
 
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi  kocha wa  Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto)   kocha   Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

MABONDIA KUTWANGANA DAR LIVE MARCH 12

Mabondia Iddi Mnyeke kushoto na Mohamed Kashinde wakiangaliana kwa usongo wakati wa utambuklisho wa mpambano wao utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA mbalimbali watazitwanga march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala akizungumza mbele ya waandishi wa habari mratibu wa mpambano uho

Rajabu Mhamila 'Super D' amewasainisha mabondia mbalimbali kuzipiga siku hiyo ambapo bondia Ibrahimu Maokola 'Simba wa Mbagala' atazipiga na Joseph Sinkala kutoka Mbeya mpambano wa ubingwa raundi kumi kg 74 utakaosimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa 'TPBC'  kinachongozwa na Rais Chaurembo Palasa

aliendelea kwa kusema siku hiyo bondia Iddi Mnyeke kg 61 atamenyana na Mohamed Kashinde wakati Pius Kazaula kutoka Morogoro atakumbana na Karage Suba katika uzito wa kg 66

wakati Shabani Kaoneka atakumbana na Said Seleman mpambano wa raundi sita kg 72 na Ambokile Chusa atavaana na Seleman Galile katika mpambano wa raundi sita kg 74

 pia kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayo sindikiza mpambano uho 

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali



MAYWEATHER, PACQUIAO WAKUTANA USO KWA USO NA KUSALIMIANA Pacquiao na Mayweather Mayweather akisalimiana na Manny Pacquiao Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wameudhihirishia ulimwengu kuwa uhasama uliopo kati yao ni wa ulingoni na sio sehemu nyingine, hiyo ni baada ya kukutana uso kwa uso na kusalimiana kama vile sio mahasimu wakubwa. Mabondia hao wanaoshikilia mataji makubwa ya ndondi, walikutana katika uwanja wa American Airlines usiku wa kuamkia leo(Jan27) wakati wa mchezo kati ya timu ya mpira ya Miami Heat na Milwaukee Bucks katika mchezo uliomaliza kwa Bucks kushinda kwa jumla ya vikapu 109 – 102 dhidi ya Heat. Mbali na mchezo huo, mashabiki na wapenzi wa masumbwi Duniani kote wamekuwa wakisubira kwa hamu mpambano wa wawili hao ambao wamekuwa wakitambiana kwa kipindi kirefu unaotajwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu. Watazame hapo chini wakisalimiana Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest 2FACE ANASWA NA MCHEPUKO Mwanamuziki wa Nigeria, Innocent Idibia ‘2face’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya picha zinazomuonyesha akifanya mambo ya chumbani na mwanamke mwengine katika klabu yake ya usiku kuzagaa kama njugu kwenye mitandao mbalimbali. 2face na Annie siku ya harusi yao 2face na Annie siku ya harusi yao Kwa mujibu wa tovuti moja ya udaku nchini humo, imedai mwanamke anayeoneka katika picha hiyo ni mama wa watoto wa tatu wa 2face anayeitwa Pero Adeniyi, ambaye amekuwa akipigwa vita mara kwa mara na mke wa ndoa wa mwanamuziki huyo ‘Annie Idibia’ aliyezaa nae watoto wawili wa kike. 2face mwenye umri wa miaka 39, ameamua kuzima soo hilo kwa ku-post picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mke wake katika siku yao ya harusi na kuwataka watu wasipende kuingilia mapenzi yao kwani watakuja kuujua ukweli na utawaweka huru. ”Our love does not have 2 make sense 2 u. pls go on with your perfect life and know the true story behind something before u judge and start making nasty comments based on an orchestrated story by some blog.U shall know the truth and the truth shall set u free.LYTID uwana idibia”,aliandika 2face 2face Idibia 2face na katika mapozi tofauti ya kimahaba na mzazi mwenzie,Pero Adeniyi. Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest MAGAZETI YA LEO ALHAMISI . . . . . . . . . . . . . . . DSC08790 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . DSC08804 . . . . DSC08807 . . . DSC08811 . . . . . DSC08810 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Newer Posts Older Posts Home Wanaotembelea Blogu hii Sparkline 2141575 MATOKEO YA KIDATO CHA PILI MATOKEO YA KIDATO CHA PILI BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA Tanzania National Flag Tanzania National Flag Time Dar es Salaam The Digital Company The Digital Company Mtayarishaji: Mtayarishaji: Richard Mwaikenda BONGO HITS Find more music like this on GongaMx Blog Archive

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

Monday, January 25, 2016

BONDIA FRANSIC CHEKA ATUA NCHINI NA KUMPIGIA MIKWALA MSERBIA GEARD AJOTOVIC

Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia Geard Ajetovic
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni
meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia Geard Ajetovic
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni
meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS



Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam.  Bondia  Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia na kusema Mserbia Geard Ajetovic aiandae kupokea kipigo kikali katika pambano lao la mabara la uzito wa super middle la  Shirikisho la Masumbwi ya  Kulipwa Duniani (WBF).

Cheka na Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.

Akizungumza jana, Cheka alimpongeza  meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited kwa kumwezesha kuweka kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa upande wake.

Alisema kuwa Ndambile na kampuni yake imeonyesha kuwa wanajali na wanamalengo makubwa ya kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.

“Kwanza naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii, nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote duniani,” alisema Cheka.

Alisema kuwa kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.

Meneja wa Cheka, Juma Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security Limited alisema kuwa  lengo la kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.

Ndambile alisema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” alisema Ndambile.

Alisema kuwa wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.


Sunday, January 24, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA NA KUTAFUTA WAPINZANI

VICENT MBILINYI KG 63 TANZANIA 2016

Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yakawaida Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea kujifua baada ya kumchakaza bondia mkongwe wa siku nyingi Deo Njiku sasa anaendelea na mazoezi ya nguvu kwa aji ya kuwasambalatisha mabondia wengine watakaopita mbele yake

bondia huyo mpaka sasa ameshacheza michezo tisa na kushinda 7 kupoteza  na droo 1 ambapo imemuweka katika rekodi nzuri ya mchezo uho kwa mwaka jana

akizungumza na mwandishi wa habari hizo Mbilinyi amesema kwa sasa yupo fiti kucheza na mtu yoyote kwa keshaiva kikamilifu baada ya kupata mazoezi ya aina mbalimbali yanayo mjengea kujiamini katika mchezo wa masumbwi akiwa chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D'

aliendelea kwa kusema kuwa nilingia katika ngumi za kulipwa kama najitolea lakini siku zinavyozidi kwenda ndio najijengea mashabiki na kujulikana zaidi katika mchezo niupendao hivyo na ahidi sito waangusha na wala sito lewa sifa wanazonipa nitaendelea kujifua ili niendelee kupambana zaidi katika mchezo

nae kocha anaemnowa bondia huyo Super D amesema kuwa Mbilinyi ana moyo wa kufika mbali hivyo ameonesha nia ya kucheza mchezo uhu katika mazingila magumu hivyo kwa mwaka 2016 ni wake wa kutoka katika mchezo wa ngumi

na naisi katika uzito wake kwa sasa akuna wa kumsumbua kwa sababu amekutana na mabondia wa lika zote ambao wanatamba na waliotamba

Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sasa anawasimamia mabondia wake akiwemo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Shabani Kaoneka, Shomari Milundi, Vicent Mbilinyi Mwenyewe na mwanadada Lulu Kayage ambao wote wapo chini ya Super D Boxing Promotio ambayo kazi yake kubwa ni kuwafundisha na kuwatafutia mipambano mbalimbali  ya nje na ndani

MABONDIA ABDALLAH PAZI NA GORGER DIMOSO WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 BAGAMOYO MKOA WA PWANI

Bondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kutia saini za makubaliano ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri

Mabondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Abdallah Pazzi na Gerger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74

akizungumza wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo

aliongeza kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini

ambapo kwa Bagamoyo atuna jukwaa 'ring' la ngumi ata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam yaje hapa ndio vijana wapate kucheza hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hiro kwa ajili ya mchezo wa ngumi ili zisonge mbele

siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu Tuwa

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha