Tangazo

Pages

Sunday, January 11, 2015

IKOTA APANIA KUJUA MCHEZO WA MASUMBWI KWA KUWA UPO KATIKA DAMU YAKE

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza jinsi ya kurusha makonde bondia Zainabu 'Ikota' Mhamila ambaye ni binti yake anaependa ngumi kwa ajili ya kujiweka fiti katika mazoezi picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza jinsi ya kurusha makonde bondia Zainabu 'Ikota' Mhamila ambaye ni binti yake anaependa ngumi kwa ajili ya kujiweka fiti katika mazoezi picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza jinsi ya kurusha makonde bondia Zainabu 'Ikota' Mhamila ambaye ni binti yake anaependa ngumi kwa ajili ya kujiweka fiti katika mazoezi picha na SUPER D BOXING NEWS

 Bondia Zainabu Ikota Mhamila kushoto akifundishwa jinsi ya kutupa makonde na baba yake mzazi wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru Dar es salaam picha na SUPER D BOXING NEWS
ZAINABU 'IKOTA' MHAMILA  NA RAJABU MHAMILA  SUPER D



Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na binti yake baada ya mazoezi

Thursday, January 8, 2015

MABONDIA IDDI BONGE NA ALIPHONCE MCHUMIATUMBO KUZIPIGA FEB 14

NA MWANDISHI WETU

MABONDIA wenye uzito wa juu nchini Aliphonce Mchumiatumbo na Iddi Kipandu 'Iddi Bonge' watapambana Feb 14 katika ukumbi wa P.T.A sabasaba wakigombania ubingwa wa taifa pamoja na pikipiki akizungumzia mpambano huo promota Shabani Manyoka amesema kupitia kampuni ya Mahamba Incorporation Limited wameamua kuandaa mpambano huo wa uzito wa juu ambao ni admu sana nchini kufanyika na ndio mabondia wanaokubalika Duniani kote

mpambano huo wa raundi kumi utakuwa ni wa aina yake kwa kuwa kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo bondia Iddi Mnyeke atapambana na Yonas Sego wakati Sahani Kaoneka atamkabili Saidi Mbelwa, na Deo Samweli akipambana na Adam Ngange Juma fundi atakabiliana na Bakari Ostadhi na Amani Bariki 'Manny Chuga' atapambana na Mohamed Kashinde siku hiyo pia kutakuwa na mpambano mwingine wa utangulizi wa uzito wa juu kati ya Bank Mwakalebela atakae mkabili Frank Kimbwilo

Manyoka aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha ndani na nje ya ukumbi huo ambapo amesha wasiliana na walinzi mbalimbali
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.



MABONDIA IDDI BONGE NA ALIPHONCE MCHUMIATUMBO KUZIPIGA FEB 14



MADA MAUGO NA KALAMA NYILAWILA WASAIDI KUZIPIGA MARCH 8 P.T.A SABASABA



Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS
Katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Antoni Rutta katikati akiwainua mikono juu mabondia Mada Maugo na Kalama Nyilawila wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika march 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS


Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS
mabondia wakiwa katika picha ya pamoja kushoton ni Emilio Norfat,Nassibu Ramaradhani,Mohamed Matumla na Amosi Mwamakula

Sunday, January 4, 2015

Bondia mtanzania Omari Kimweri anayetesa Australia kutoa sapoti ya mafunzo ya ndondi Dar

Omari Kimweri

.Kutua Februari, apania kuzalisha akina Mayweather kibao nchini

NA Mwandishi wetu

NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.

Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.

Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.

Kwa hapa nchini, wapo mabondia waliojitengenezea majina wakiwamo Emmanuel Mlundwa, Habibu Kinyogoli 'Masta' Michael Yombayomba, Stanley Mabesi 'Ninja' Rashid Matumla, Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  na wengineo wengi.

Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Mayweather, akifuatiwa na mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.

Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya nne, huku wa tano akiwa ni mkali wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant.

Pamoja na mafanikio hayo katika ndondi, Tanzania imeonekana kuzidi kulala usingizi wa pono katika suala zima la kuvumbua na kuendeleza vipaji vya mchezo huo kama sehemu ya kutatua tatizo sugu la ajira linaloitesa nchi yetu kwa sasa.

Unapopita huko mitaani, unaweza kukutana na vijana wadogo wakiwa wanafanya mazoezi ya ngumi kwa kutumia vifaa visivyo rasmi ambavyo mwisho wa siku, huishia kuwadumaza badala ya kuwajenga kama walivyotarajiwa.

Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia mchezo huo, zikiwamo kumbi na hata wataalam wa kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufikia mafanikioi ya akina Mayweather.

Ni kwa kufahamu hilo, wapo wadau wa ndondi ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia vipaji vya ndondi hapa nchini, miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Kimataifa wa Ndondi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’.

Bondia huyo wa zamani, ameshawahi kufanya jitihada kadha wa kadha kuendeleza ndondi hapa nchini, ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana chini ya klabu yake ya Ashanti Boxing Club na kupitia DVD zake zenye mapambano makali yaliyowahi kufanyika hapa nchini na duniani kwa ujumla, yakiwahusisha mabondia nyota.

Katika kuonyesha jinsi anavyoguswa na ndondi, Februari mwaka huu Super D atakuwa na ugeni mkubwa wa bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri ambaye anatua nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanamasumbwi wa Tanzania.

Akizungumza Dar es salaam jana, Super D anasema kuwa ujio wa Kimweri ni fursa nyingine adimu kwa mabondia wa Tanzania katika kuona ni vipi wanaweza kutimiza ndoto zao za kutoka kimaisha kupitia mchezo huo.

Anasema kuwa Kimweri atatua akiwa na vifaa mbalimbali vya masumbwi ambapo pia atatoa mafunzo na mbinu mpya zinazotumiwa na mabondia wa nje kwa mabondia pamoja na kushuhudia mapambano kadhaa yatakayofanyika kwa kipindi atakachokuwapo hapa nchini.

“Kimweri anakuja akiwa na msafara wa watu kadhaa, akiwamo mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. Akiwa hapa nchini, Melanie atapata fursa ya kukutana na wanasoka wa kike wa hapa , kwani amechezea timu nyingi za Ulaya,  Hispania,” anasema Super D.

Anasema kuwa ujio wa Kimweri umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na promota wake, Brian Amatruda ambaye ni miongoni mwa mapromota maarufu nchini kwao Australia, akiwa amekubali kutoa baadhi ya vifaa vya kisasa kutoka Hispania na Marekani kwa ajili ya ziara hiyo.

Super D anasema kuwa Kimweri ambaye ni bingwa wa WBO, atatua nchini akiwa na mikanda yake yote aliyowahi kutwaa, ukiwamo wa ubingwa wa Australia, lengo likiwa ni kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujikita zaidi katika ndondi.

“Nimezungumza na Kimweri na ameonyesha kuwa na uchungu wa kuwainua mabondia wa hapa nchini ili waweze kutimiza ndoto zao na anafanya hivyo chini ya mradi wake wa ‘Kimweri Project’ na atakuwa hapa nchini kwa wiki moja,” anasema.

Anasema kuwa ujio wa bondia huyo uliochagizwa na Super D Boxing Coach and Promotion, umelenga kuwahamasiaha mabondia kucheza mara kwa mara ili kupandisha viwango vyao kwani hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanamasumbwi wengi duniani.


Mbali ya mafunzo kutoka kwa Kimweri, pia katika ziara zake zote sehemu mbalimbali nchini, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Super D zenye lengo la kutoa mafunzo kupitia mapambano ya mabondia maarufu duniani, akiwamo Floyd Mayweather,Manny Paquaio, Mohamerd Alli, na wa hapa nchini kama Mbwana Matumla, Francis

Miyeyusho,Ibrahimu Class' King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa WPBF Africa na wengineo.
OMARI KIMWERI
bondia  Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine march 13 mpambano utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
   

BONDIA OMARI KIMWERI KUWASILI NCHINI FEBRUARI KUHAMASISHA NGUMI



BONDIA wa kimataifa Mtanzania Omari Kimweri anayeishi nchini Australia


BONDIA wa kimataifa Mtanzania Omari Kimweri anayefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi  nchini Australia anatarajiwa kuwasili nchini Februari mwaka huu.

 Super D ambaye ni mratibu wa safari ya bondia huyo alisema, Kimweri atakuja nchini na ujumbe wa watu nane ambao watakuwa na kazi hiyo kwa muda wa wiki mbili.
Akizungumza jana , kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi, Tanzania Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa lengo ya bondia huyo kuja nchini ni kuhamasisha masumbwi.

Pindi atakapokuja atashikua uwanja wa Kia na baadaye atakwenda mkoani Tanga  ambapo ni nyumbani kwao alipo zaliwa kwa ajili ya mapumziko na baada ya hapo atakwenda Dar es Salaam.

Alisema kuwa pindi atakapokuwa Dar es Salaam atakuwa mgeni rasmi katika pambano litakalokuwa
siku ya wapendanao 'Valentine Da y' 
Kocha huyo wa kimataifa alitoa mwito kwa wadau wa mchezo huo kutoa ushirikiano pindi ujumbe huo utakawasili nchini.
bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine march 13 mpambano utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia

Friday, January 2, 2015

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE KATIKA KIPINDI CHA XMASI NA MWAKA MPYA

Bondia Jacobo Maganga kushoto akipambana na Shabani Kaoneka wakati wa mpambano wao uliomalizika kwa sare Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia wa uzito wa juu Iddi Bonge kushoto na Mussa Mbabe wakipambana wakati wa mpambano wao Bonge alioshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na kumsambalatisha Mussa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia wa uzito wa juu Iddi Bonge kushoto na Mussa Mbabe wakipambana wakati wa mpambano wao Bonge alioshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na kumsambalatisha Mussa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Shomari nMirundi kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anayejiandaa kugombani amkata wa UBO Africa na bondia Cosmas Cheka Feb 28

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na mabondia Shomari Mirundi katikati na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anayejiandaa kugombani amkata wa UBO Africa na bondia Cosmas Cheka Feb 28
Bondia Ramadhani Kumbele kushoto akipambana na moro best wakati wa mbambano wao kumbele alishinda kwa pointi mpambani huo wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Jacobo Maganga kushoto akipambana na Shabani Kaoneka wakati wa mpambano wao uliomalizika kwa sare katika mpambano huo uliovuta isia za watu wengi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Dula mbabe akivalishwa glove na Shomari Kimbau
Mabondia Abdallah Pazi Kushoto na Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mbambao wao wa kufungua mwaka uliomalizika kwa droo baada ya kugongana vichwa katika raundi ya tatu  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Abdallah Pazi Kushoto na Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mbambao wao wa kufungua mwaka uliomalizika kwa droo baada ya kugongana vichwa katika raundi ya tatu  Picha na SUPER D BOXING NEWS