Tangazo

Pages

Friday, May 16, 2014

PAMBANO LINGINE LA UBINGWA MAY 24: SULEIMAN TALL V/S DULA MBABE


Seleman

 Dar es Salaam,
Bondia mzoefu wa ngumi za kulipwa nchini, Suleiman Galile ”tall” anategemea kupanda tena ulingoni Mei 24 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam, kuzipiga na Abdalah Pazi “dula mbabe/kiroba” katika pambano lisilo la ubingwa la uzito wa kg76.
Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo, Katibu wa ngumi za kulipwa nchini, ambaye ndiye anayesimamia mapambano yote ya utangulizi, Bw. Ibrahim Abbas Kamwe alisema, Galile na Dula wamekubaliana kusheza siku hiyo ya Jumamosi ya Mei 24, huku wakisindikizwa  na Karama Nyilawila na Said Mbelwa.
Watakaogombania ubingwa wa UBO,hapo awali ilipangwa Karama kuzipiga na Thomas Mashali ambae amepatwa na majeraha kutokana na ajali ya gari.
Pia siku hiyo kutakuwepo na  mapambano mengi ya utangulizi yenye ushindani , wakati  Adam Ngange akimkabili Alan kamote wa Tanga, zumba kukwe atazipiga na kamanda wa makamanda,Seleman Zugo na Manyenza,  Ramadhan Kumbele ataoneshana umwamba na Hassan Kiwale “Moro best”, wakati Bakari Dunda atapambana na Mbena Rajabu.
Madogo wanaokuja juu kwa kasi katika ngumi, Idd Athuman atacheza na Julias Thomas Kisarawe, wakati Mwaite Juma atachuana na Daudi Giligili.
 Kamwe alimaliza kwa kusema mpaka sasa hakuna bondia mwenye matatizo wote wapo katika hali ya ushindani wanaisubiria kwa hamu hiyo siku ifikie wabanjuane kiukweliukweli .

Tuesday, May 13, 2014

MABONDIA SAID MBELWA NA KARAMA NYILAWILA WATAMBIANA KUPAMBANA MAY 24 MANZESE

Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony Rutta picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Said Mbelwa na Karama Nyilawila wametambiana kila mmoja kuibuka mbabe katika mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Univers Boxing Oganaization UBO  mpambano utakaofanyika katika ukuimbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam

likiwa linasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST mpambano huo utakao onesha kuwa nani mbabe wa uzani wa kg 76 ubingwa wa UBO akizungumzia mpambano huo Katibu mkuu wa shilikisho la ngumi za kulipwa nchini Antony Rutta amesema kuwa mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi nchini ukuiwa na mabondia wote wamecheza ngumi za kitaifa na kimataifa yani ndani na nje ya nchi

akitolea mfano bondia Said Mbelwa ndie bondia pekee ambaye anaenda nje ya nchi kucheza ngumi na kumaliza raundi zote 12 walizo pangiwa ingawa anapigwa kwa pointi ambapo mabondia wengi wa Tanzania wakienda nje wanapigwa K,O mbaya sana ambazo zinawatia mpaka itrafu katika baadhi ya maeneo

akimzungumzia Nyilawila ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa uzani huo wa WBF ambaye alichukua mkanda huo nje ya nchi jambo ambalo kubwa sana duniani kumpiga mzungu nyumbani kwao si mchezo hivyo mabondia wote hawa wana sifa zinazo lingana

nae bondia Mbelwa aliongeza kwa kusema kuwa mimi nipo fiti hivyo mashabiki waje kwa wingi kuangalia ngumi ambazo zitahacha historia kubwa katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwa kipigo nitakachompa Karam

Nae bondia Nyilawila alitamba kwa kukimbiwa na Thomasi Mashali ambaye alikuwa acheze nae ata hivyo bondia huyo amepata ajali ya gari na zamu yake atacheza Mbelwa uchu wangu mkubwa ni Mashali huyu wamemuonea bule kunipa mimi nita hakikisha namchakaza bila huruma ata chembe

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile gem ya fransic Miyeyusho vs Mohamed Matumla 'Sneak jr'  mpambano ulivuta hisia za wapenzi wengi wa ngumi nchini 
Floyd Mayweathar,
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Amir Khan Mbabe mwenye ndoto za kumchapa Mayweather Jr



Amir Khan

LAS VEGAS, Marekani
LEO katika maisha ya wenzetu tutakuwa na bondia wa Uingereza Amir Khan ambaye hivi karibuni amefanikiwa kumchapa Luis Collazo.
Mbabe huyo amefanikiwa kuonesha kwamba bado makali yake yana uhai katika pambano hilo baada ya kufanikiwa kumlambisha vumbi mpinzani wake huyo katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
Khan amejikuta akicheza pambano hilo kwa ustadi kutokana na kutafuta nafasi ya kucheza na Mayweather ambayo miezi 12 nyuma ilionekana kuyeyuka baada ya kutocheza na bondia yeyote.
Kwa kuonesha kwamba amedhamiria kucheza na Mayweather Jr, baada ya kushinda pambano hilo alisikika akisema kuwa bondia anayemtaka kwa sasa ni mbabe huyo asiyepigika.
Alisema “kwa sasa naamini watu watakuwa wakitaka kushuhudia pambano langu na Floyd ambaye naamini nitamchapa kirahisi kutokana na umri wake kuwa mkubwa,”.
USICHOKIJUA
Ingawa watu wengi hufikiria kwamba Khan ni raia wa nchi za Asia lakini kijana huyo amezaliwa na kukulia Bolton, England, na wazazi wenye asili ya kipakistan wanaotokea katika jamii ya Punjab.
Khan ni muumini wa dini ya kiislam, na amekuwa akisaidia katika kuiwezesha tuzo inayotolewa na waislama wa nchini humo inayokwenda kwa jina la ‘Muslim Writers Awards’.
han anatoka katika familia yenye watoto wanne ambako ana dada wawili na kaka mmoja, Haroon ‘Harry’ Khan, mbabe asiyepigika.
Amir Khan ni mdogo wa mbabe na mshindi wa medali ya Olympic ya Uingereza, mshindi wa medali ya fedha ya olimpiki ya mwaka 2004 wakati akiwa na miaka  17.
Khan ana historia ya kukamata ubingwa wa dunia wa WBA akiwa na umri mdogo kuliko mwingireza mwingine wakati huo aliuchukua akiwa na miaka 22.
Ukiachilia ngumi ni mpenzi wa mchezo wa Kriketi, mpira wa kikapu na soka akiwa shabiki wa klabu ya Bolton Wanderers.
Mwaka 2012, alikuwa katika picha ya pamoja katika akaunti yake ya Twitter ikimuonesha akiwa na wachezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand, Alex Buttner, Michael Carrick na David De Gea.
Lakini pamoja na kuonekana akiwa na nyopta hao huku akiwa amevaa jezi ya klabu hiyo lakini Khan alisema kuwa 'pamoja na kufanya hivyo lakini mimi bado ni shabiki wa klabu ya Bolton kwa njia yoyote.'
MSAADA WA KIJAMII
Khan amekuwa mtoaji mzuri wa misaada kwa watu wenye mahitaji kwa mfano mwaka 2004 alitoa msaada wa Euro milioni 1 kwa familia za wahindi waliokumbwa na tetemeko la Tsunami nchini India.
Katika mwaka huo alikwenda nchini Pakistan na kutoa vyakula katika kambi za watu waliokuwa wameathiriwa na tetemeko la Kashmir.[
Desemba 2013, Khan aliongoza harambee ya kuchangia Umoja wa waislam kutoka Ufilipino kwa ajili ya kutoa msaada wa waathirika wa tetemeko la Typhoon Haiyan na walikusanya kiasi cha Euro 83,400.
JINAI
Oktoba 23, 2007 Khan alitiwa mbaroni kwa kuendesha kwa kasi na alifikishwa katika mahakama ya Bolton kujibu shtaka lake ambako alifungiwa kuendesha gari kwa muda wa miezi sita ikiwamo na kupigwa faini ya euro 1000.
Mwaka 2006 aliwahi kupigwa faini ya Euro 40,000 kwa kosa la kuendesha kwa kasi.
Januari 7, 2008 Khan alipigwa faini ya Euro 1000 na kufungiwa kuendesha gari kwa siku 42.
Kama ilivyokawaida mwenye tabia yake hawezi kuacha Julai 12, 2009 Khan alijikuta akipata ajali ingawa hakufikishwa katika vyombo vya sheria.
MAHUSIANO
Januari 29, 2012 Khan alifunga ndoa na mwanamke wa Marekani mwenye asili ya Pakistani, Faryal Makhdoom katika harusi ya kifahari iliyohudhuriwa na ndugu na marafiki waliofikia 1000 akiwamo bondia Ricky Hatton.
Wawili hawa walifanya sherehe ya harusi yao Mei 31, 2013 huko Waldorf Astoria jijini New York, Marekani.
Baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo ya kifahari wawili hawa walichukua ndege na kwenda nyumbani kwao na Khan huko Bolton kwa ajili ya kufanya sherehe nyingine ya kimila iliyofanyika Manchester na kuhudhuriwa na wageni 4,000.
FEDHA
Mbabe Amir Khan  anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 23 (sawa na shilingi bil 36.8).
MAKAZI
Mbabe Amir Khan ana mjengo wa maana ambao hajaweka thamani yake lakini pia anamiliki gari mbalimbali ikiwamo Range Rovers, Bentley Continental, New Mercedes CLS63, Audi R8, Lamborghini Murcielago na Can-Am Spyder.
WASIFU
JINA: Amir Iqbal Khan ‘King’
KIMO: Futi 5 na inchi 9
UMRI: 27
Mapambano ya kucheza: 31
Ushindi: 28
KO:     20
Poteza:    3
Sare: 0
Makala hii imeandaliwa na Shabani Matutu.
Mwisho.
Amir Khan

DVD MPYA ZA MASUMBWI NGUMI ZA TANZANIA


 DVD MPYA YA NGUMI ZA MABONDIA WENYE UFUNDI MKUBWA WA NGUMI NCHINI TANZANIA FRANSIC MIYEYUSHO VS MOHAMED MATUMLA NDANI KUKIWA NA MAPAMBANO YOTE YA UTANGULIZI KWA MAITAJI YA DVD HIZI MPYA NA NINGINE ZA FLOYD MAYWEATHER VS NICOLAUS MAIDANA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO ZAIDI PIGA NAMBA 0715406938 SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION
FRANSIC mIYEYUSHO VS MOHAMED MATUMLA DVD

Bondia Nassibu Ramadhani DVD yake kukiwa na mapambano yake ya nje ya nchi

Sunday, May 11, 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA MABIBO MWISHO

Bondia Fabian Lymo kushoto akipambana na Bakari Dunda wakati wa mpambano wao uliofanyika Mabibo Dar es salaam jana Lymo alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fabian Lymo kushoto akipambana na Bakari Dunda wakati wa mpambano wao uliofanyika Mabibo Dar es salaam jana Lymo alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
mabondia baada ya kumaliza mpambano wao
Bondia Fabian Lymo kushoto akinyoshwa mkono juu baada ya kumshinda  Bakari Dunda wakati wa mpambano wao uliofanyika Mabibo Dar es salaam jana Lymo alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Muhidiniakiwa chini baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Nassibu Ramadhani
Bondia Nassibu Ramadhani akipambana na Bondia Said Muhidini Ramadhani alishinda kwa T,K,O ya raundi ya kwanza
Kocha wa mchezo wa ngumi Ramadhani Uhadi akimwelekeza jinsi ku kutupa makonde bondia Fabian Lymo
Fabian Lymo



Msanii wa muziki wa hipop Karama Masoud 'Kala Pina'  akitumbuiza katika onesho lake lililofanyika mwishondi wa weiki iliyopita katika ukumbi wa D.I.D hall uliopo Mabibo mwisho Dar es salaam

Bondia Nassibu Ramadhani wa pili kulia akiwa na mashabiki wake uku wakiangalia ngumi katika ukumbi wa DID Mabibo mwisho jana
Bondia Juma Fundi kushoto akipambana na Baina Mazola wakati wa mpambano wao uliofanyika mabibo mwisho Dar es salaam jana Fundi alishinda kwa point mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, May 10, 2014

BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO AMSHINDA MOHAMED MATUMLA KWA POINTI


  Bondia Mohamed Matumla kushoto akikwepa konde la Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita miyeyusho alishinda kwa pointi na kuibuka msindi wa m,pambano huo wa kirafiki picha na Rajabu Mhamila
 Bondia Mohamed Matumla kushoto akimtupiana makonde  na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita miyeyusho alishinda kwa pointi na kuibuka msindi wa m,pambano huo wa kirafiki picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'
Mabondia Halima Ramadhani kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Lulu Kayage wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mchezo wao uliamliwa kuwa ni droo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Lulu Kayagekushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde naHalima Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mchezo wao uliamliwa kuwa ni droo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii Saidi Chaku akiwanyoosha mikono juu mabondia Lulu Kayage na Halima Ramadhani kuwa ni droo mpambano wao

Promota Ally Mwazoa kushoto akiwatunza mabondia Lulu Kayage na Halima Ramadhani baada ya kumaliza mpambano wao

Bondia Kassimu Gamboo akipambana na Kassimu Rajabu wakati wa mpambano wao Gamboo alishinda kwa point
kassimu gamboo akinyoshwa mkono juu kuashilia ushindi wake

NASSIBU RAMADHANI,SAID MUHIDIN,JUMA FUNDI, BAINA MAZOLA WAPIMA UZITO KUZIDUNDA KESHO MABIBO MWISHO

Bondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Said Muhidini baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya may 11 katika ukumbi wa D.I.I Hall mabibo mwisho katikati ni mratibu wa mpambano huo Bahiyo Mkumbi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Juma Fundi kushoto akitunishiana misuli na Baina Mazola baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya may 11 katika ukumbi wa D.I.I Hall mabibo mwisho katikati ni mratibu wa mpambano huo Bahiyo Mkumbi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Muhidini akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Nassibu Ramadhani kushoto
Bondia Baina Mazola akipima Uzito