Tangazo

Pages

Wednesday, March 5, 2014

Francis Miyeyusho: Uswazi kunaharibu wanamichezo

Francis Miyeyusho: Uswazi kunaharibu wanamichezo


Kwa ufupi
Katika Jiji la Dar es Salam maeneo kama Tandale, Temeke, Magomeni, Manzese, Keko, Kinondoni ni baadhi ya maeneo yenye sifa hizo. Maeneo ya Morogoro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Mbeya nazo zimesheheni sifa hizo.
Photo: Miyeyusho ‘alia’ kuandamwa na madeni
Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
Dar es Salaam. Bondia Francis Miyeyusho amesema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano lake na Viktor Chernous wa Ukrane kumemuingiza katika deni na kocha wake.
Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
“Hadi sasa sijui kama pambano litakuwepo hiyo Jumamosi au la kwani nimekuwa nikijifua, lakini sijaambiwa chochote kuhusu kuwepo kwa pambano hilo,” alisema Miyeyusho.
Alisema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano hilo kumemuingiza katika gharama kubwa za maandalizi yake.
Hadi jana mchana Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBF) halikuwa limetoa kibari cha pambano hilo ambapo rais wa TPBF, Chatta Michael alisema wanasubiri agizo la Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kutoa kibari cha pambano hilo.
Kwa mujibu wa promota wa pambano hilo, Jay Msangi huenda pambano hilo likasogezwa tena mbele endapo hakutapatikana kwa mwafaka kati yake na BMT ambayo ilimpa sharti la kulipa madeni yote ambayo anadaiwa licha ya kueleza tayari ametimiza masharti hayo na BMT bado inaendelea na msimamo wa kumfungia.Katika hali isiyo ya kawaida mabondia wanaofanya vizuri na kujizolea umaarufu nchini wamekuwa wakitokea kwenye maeneo hayo ya uswazi, hii inawezekana inachangiwa na aina ya mchezo.
Mchezo huo wa ndondi huhitaji watu wakakamavu, wenye stamina na uvumilivu ambao ni vigumu sana kuwapata maeneo ya ‘Kishua’ kama Mbezi Beach, Mikocheni na Masaki.
Kauli ya Miyeyusho kuhusu bangi
Alipoulizwa kuhusu shutuma kuwa mabondia wengi wanajihusisha na uvutaji wa bangi, Bondia Francus Miyeyusho alisema, “Unajua mabondia wengi tunatokea uswahilini ambako hayo mambo ndio yanafanyika. Ndiyo maana utakuta baadhi ya mabondia wanatumia vitu hivyo.”
“Hili siyo la mabondia tu ila hata wanaocheza michezo mingine kama soka, riadha na kikapu wanaotokea maeneo yetu haya ya uswahilini utakuta wanatumia.” Aliongeza Miyeyusho anayeishi Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho anadai kuwa malengo ya kutumia vitu hivyo yanatofautiana, ambapo wengine hutumia kama starehe wakati wengine hutumia ili iwasaidie kupata hamasa ya mchezo.
Mkali wa ‘Knockout’
Katika mapambano 47 aliyopigana Miyeyusho, 32 yalimalizika kwa ‘knockout’. Kati ya mapambano hayo 32, mapambano 23 alishinda kwa knockout na kupoteza tisa kwa knockout akiwa ndio bondia pekee wa Tanzania mwenye rekodi ya kushinda michezo mingi kwa ‘knockout’ na kushindwa mingi kwa staili hiyo hiyo. Katika michezo kumi aliyopoteza tisa amepoteza kwa ‘knockout’
“Mimi huwa napenda kuimaliza michezo yangu kwa ‘knockout’ kwa sababu mara nyingi ushindi wa pointi humalizika kwa utata. Wengine huona kama bondia amependelewa ushindi kitu ambacho siyo sahihi.”
“Nimepoteza mapambano mengi kwa ‘knockout’ kwa sababu ya kuwa na maandalizi duni, kutokana na hali ndogo ya kipato likitokea pambano hata kama sina mazoezi huwa nakubali ili nipate fedha japo ninajua sitaweza kushinda.

Monday, March 3, 2014

PAMBANO LA KUKUBUKWA



  Shavers amwadhiri Norton
•    Adondoshewa vitasa vizito na kulamba sakafu
BONDIA  Earnie Shavers alikuwa akijulikana kama bondia mwenye ngmi
nzito kuwahi kutokea katika uzito wa juu, wenyewe wakielezea kwa lugha
yao wakimwita  ‘The Hardest Heavyweight Puncher Ever’
Bila shaka na kwa uhakika ndivyo ilivyokuwa, alikuwa ni bondia mwenye
ngumi za hatari, mabondia waliogopwa wakati ule kwa ngumi nzito na
nguvu akina Joe  Frazier, Georgr Forema na hata Muhammad Ali
walichemka kumpiga kwa KO japo walimshinda katika mapambano yao.
Earnie Shavers aliingia rasmi katika ngumi za kulipwa mwaka1969. Mbali
na mabondia niliowataja, pia alitwangana na  Ron Lyle, Jerry Quarry,
Jimmy Ellis, Jimmy Young na George Chuvalo kuwataja wachache na hakika
alikuwa si bondia mwenye ngumi nzito tu bali pia bondia mwenye kipaji
katika ngumi za uzito wa juu.
Bila shaka bondia Ken Norton alikuwa akijulikana kwa umahiri wake hasa
baada kumvunja taya Ali na kumshinda kwa pointi, katika pambano la
kwanza na kwa hivyo pambano hilo lilikuwa ni la kukata na shoka na
mashabiki wengi walimpa nafasi kubwa Norton ya kushinda pambano hilo.





Pambano la Norton dhidi ya Shavers lilifanyika Machi  23, 1979 japo
lilikuwa ni pambano au wakati ambao mabondia hawa wote walikuwa
wakielekea ukingoni mwa taaluma yao.
Ken Norton alikuwa amepoteza mapambano yake mawili ya kuwania ubingwa
wa dunia  alipanda ulingoni akiwa na rekodi ya mapambano  41 akipigwa
5 huku  33  akishinda kwa ‘knockouts’ (KO). Pambano lake la mwisho la
KO lilikuwa dhidi ya bondia Randy Stephens. Norton alikuwa amepigwa na
kupoteza taji, alipigwa na Larry Holmes.
Earnie Shavers  alkiuwa bado shupavu hata hivyo, akionekana bado
mwenye nguvu na stamina .  Alikuwa ameshinda mapambano yake matatu kwa
KO dhidi ya  Harry Terrell, John Girowski na  Harold Carter kabla ya
kupanda ulingoni.
Shavers alikuwa na rekodi ya mapambano 57 akipigwa 7 na kutoka sare 1
huku mapambano 54 akishinda kwa ‘knockouts’ na rekodi za mabondia hao
zilifanya pambano hilo kuwa gumzo kwa hakika.

1.    Raundi ya kwanza:

1.    Raundi ya kwanza:

Mabondia wanakutanishwa katikati, baada ya kutambulishwa na mtangazaji
ulingo yaani ‘ring announcer’ wanakutanishwa kaikati, wanasalimiana
kisha kila mmoja anarejea kwenye kona yake huru (neutral corner).
Kengele ya kwanza inalia, Shavers anaanza kwa kasi bila kupoteza muda
na kumfuata Norton na kumbana kwenye kamba za ulingo, Shavers
anasukuma makonde ambayo yanapanguliwa na Norton na katika harakati
hizo, Norton alirusha ngumi ya kushoto na kumpata Shavers kwenye shavu
na  Shavers akajibu na ngumi ya kushoto aliyeungnisha na  ‘uppercut’.
Ngumi hizo zilikuwa si mchezo, zilikuwa ni ngumi za nguvu na
zinaonekana mkumuumiza Norton. Shavers anaona hali hiyo ya Norton
kuelemewa mapema tu na ngumi zake, anamfuata kwa kasi na kusukuma
‘uppercut’ ningine ya nguvu na mwanamme  Ken Norton hana namna, konde
lile linakuwa zito zaidi kwake na anashuka chini na ‘kulamba’ sakafu.
Mwamuzi wa pambano hilo anamuhesabia Norton lakini anapofia hesabu ya
sita, Norton ananyanyuka. Mwamuzi anamwamuru Norton apanguse glavu,
anafanya hivyo kisha anaruhusiwa kuendela a pambano.
Shavers hapotezi muda, anamfuata kwa kasi Norton ambaye bado
anaonekana kuwa katika maumivu ya ngumi, anamshushia ngumi ndoano ya
kulia ‘right uppercut,’ na  Norton anakwenda tena chini kama gunia la
mchele mbovu.
Norton anasubiriwa kunyanyuka lakini hajiwezi kabisa na mwamuzi
anamaliza pambano, Earnie Shavers anakuwa mshindi kwa TKO ambayo
kiukweli inapaswa kuwa KO bor
a. Pambano hili linaingia kwenye rekodi
za mapambano bora ya KO.
Kwa upande wa Earnie Shavers pambano hilo lilikuwa ni kila kitu kwake,
alikuwa na faida na hasa nguvu zake katika makombora. Katika pambano
hilo Shavers alimshushia makombora kadhaa Norton ambaye muda wote
alikuwa akirudi nyuma na kujikinga.
Ikumbukwe kuwa  Ken Norton hakuwa bondia wa kurudi nyuma hata kidogo,
lakini siku hiyo alikuwa katika shida kubwa, alikuwa amepambana na
bondia mwenye nguv
u

Saturday, March 1, 2014

BERNARD MWAKASANGA AJIFUA KUMKABILI IDI BONGE MARCH 23

Bondia Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha ' wa uzito wa juu akipiga panch bag kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Idi Kipandu 'Idi Bonge' mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa frends corner Manzese March 23 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha ' wa uzito wa juu akipiga panch bag up cat kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Idi Kipandu 'Idi Bonge' mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Frends corner Manzese March 23 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha ' wa uzito wa juu akijifua kwa ajili ya mpambano wake na Idi Bonge March 23 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha ' wa uzito wa juu akinua chuma  kwa ajili ya mpambano wake na Idi Bonge March 23 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
Bondia Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha ' wa uzito wa juuameingia kambini kwa ajili ya kujifua kuwinda mpambano wake wa march 23 katika ukumbi wa frends corner Manzese Dar es salaam
 ambapo atapambana na Iddi Kipandu 'iddi Bonge' mpambano huo ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki mbalimbali wa mchezo huo sasa homa yake imezidi kupamba moto baada ya kila mmoja kumtambia mwenzake kuwa atammaliza raundi za awali

akizungumza katika GYM yake iliyopo Gongolamboto Mwakasanga ameseme Iddi Bonge ni kama nyama ya bucha hivyo mimi ni shoka nitapasua kichwa chake hivyo watu waje wajionee ninavyo fungua bucha manzese siku hiyo

mpambano huo ambao utakuwa na mapambano makali ya utangulizi kwa mujibui wa mratibu wa mpambano huo Waziri Rosta ameongezea kuwa bondia Fadhili Mjia 'stoper' ataoneshana kazi na Juma Selemani uku Twalibu Mchanjo akikutana na Mohamed Babeshi, wakati Hassani Mandula akipambana na Ally Bugingo mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki na Selemani Motto, na Halidi Manjee akioneshana umwamba na Shabani Mtengela huku Mustafa Dotto akizichapa na Ismail Ndende na Salimu Chagogo atazikunja na Salumu Kombe 

aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima nmnawza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Thursday, February 27, 2014

Miyeyusho ‘alia’ kuandamwa na madeni



Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
Dar es Salaam. Bondia Francis Miyeyusho amesema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano lake na Viktor Chernous wa Ukrane kumemuingiza katika deni na kocha wake.
Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
“Hadi sasa sijui kama pambano litakuwepo hiyo Jumamosi au la kwani nimekuwa nikijifua, lakini sijaambiwa chochote kuhusu kuwepo kwa pambano hilo,” alisema Miyeyusho.
Alisema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano hilo kumemuingiza katika gharama kubwa za maandalizi yake.
Hadi jana mchana Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBF) halikuwa limetoa kibari cha pambano hilo ambapo rais wa TPBF, Chatta Michael alisema wanasubiri agizo la Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kutoa kibari cha pambano hilo.
Kwa mujibu wa promota wa pambano hilo, Jay Msangi huenda pambano hilo likasogezwa tena mbele endapo hakutapatikana kwa mwafaka kati yake na BMT ambayo ilimpa sharti la kulipa madeni yote ambayo anadaiwa licha ya kueleza tayari ametimiza masharti hayo na BMT bado inaendelea na msimamo wa kumfungia.

Wednesday, February 26, 2014

MAYWETHER KUPAMBANA NA MAIDANA MEY 3 MGM USA

Mayweather Chooses Maidana
  1. Moja ya picha za kutengeneza alizoziweka bondia Floyd Mayweather Jr kulia akimwazibu
    Marcos Rene Maidana siku itakapo fika mpambano wao ambao umepagwa kufanyika mey 3
  1. BONDIA Floyd Mayweather Jr amesaini mkataba wa makubaliano wa kupambana na bondia Marcos Rene Maidana  Mpambano utakaofanyika siku ya May 3 katika ukumbi wa MGM Grand, Grand Garden Arena, Las Vegas, Nevada, USA 

  2. Mpambano huo uliokuwa ukigombaniwa na  mabondia wawili akiwemo Amir Khani ambaye kula zake azijatosha kupambana na Floyd Mayweather Jr aliye omba mashabiki wake wampigie kula nani wa kupigana nae ambapo nafasi imemwangukia Maidana

Sunday, February 23, 2014

NGUMI ZAPIGWA MBAGALA

BONDIA Mussa Shuza kushoto akioneshana umwamba na Dackson Kawiani wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub mbagala rangi tatu Kawiani alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Ibrahimu Ahmed kushoto na Mohamed Kashinde wakioneshana ubabe wakati wa mpambano wao uliofanyika mbagala Dar es salaam Kashinde alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Hassani Kidebe kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na Shabani Mtengela wakati wa mpambano wao Mtengela alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, February 21, 2014

KALAMA NYILAWILA ASAINI MKATABA WA KUCHEZA NA BINGWA KATI YA MASHALI AU KASEBA MEI MOSI

Bondia Kalama Nyilawila katikati akitia saini ya kucheza pambano siku ya mei mosi atacheza na Thomasi Mashali au Japhert Kaseba inategemea na mshindi wa mechi hiyo ya March 29 itakayofanyika PTA Sabasaba kulia ni Alli Mwazoa na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu

Bondia Kalama Nyilawila Ameingia mkataba wa makubaliano na promota Ali Mwazoa wa Tanga kwa ajili ya mpambano wa Mei Mosi mwaka huu ambapo  anasubili mshindi wa mpambano kati ya Thomasi Mashali na Japhert Kaseba ambao watazichapa March 29 katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atacheza na

Kalama Nyilawila siku ya  mei mosi akizungumza baada ya kusaini mkataba huo bondia Kalama Nyilawila alijitapa kwa kusema iwe Mashali awe Kaseba yoyote atakae kutana nae ato kuwa na masiara nae atampiga kipigo cha mbwa mwizi kwani nafasi hiyo alikuwa anaitafuta siku nyingi baada ya kupoteza huwezo wake katika masumbwi hivyo sasa wakae mbali na mimi kwani nakuja kwa nguvu mpya kabisa akisema atakuwa hatari kama 'Mbeya City' timu ambayo inatoka mkoani kwao na kufanya maajabu kwa kuitawala ligi kuu ya Tanzania bara ndivyo na mimi nitakavyofanya

Kalama katika harakati zake za kuhakikisha anarudi katika chati kama zamani mechi yake ya mwisho katika kuukaribisha mwaka 2014 alimsambalatisha bondia Ibrahimu Maokola bila huruma kwa kumpiga K,o ya raundi ya pili mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Msasani klabu

Nae promota wa mpambano huo Mwazoa amesema kila kitu kinaendelea vizuri ikiwemo mapambano ya utangulizi yenye mabondia bora wanaotamba kwa sasa ambao wapo kwenye kiwango cha ali ya juu kwa kuwa mwaka huu ni wa masumbwi nchini Tanzania nimeanza na nitaendelea kusapoti na kupromot mchezo wa ngumi popote nchini

akizungumza kwa niaba ya chama kilichopewa dhamana ya kusimamia mchezo huo wa mei mosi Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' amesema watanzania wana bahati sana kwa kujitokeza promota mwenye uchu wa maendeleo kwa mabondia kwana mabondia wote wame saini mkataba na kupewa posho ya kufanyia mazoezi isipokuwa bondia mmoja tu kati ya watakaocheza march 29 ni Kaseba au Mashali jibu ndio tunasubili siku hiyo nani zaidi na atakaepata nafasi ya kuchapana na Kalama