Tangazo

Pages

Monday, October 7, 2013

ADAMU NGANGE AMUWAZA JONAS SEGU SASA AMTAKA KING CLASS MAWE


UKIZUNGUMZIA mabondia chipkizi wanaofanya vizuri katika tasnia ya masumbwi nchini kamwe uto kosa kumtaja bondiaAamu Ngange anae wakilisha kitongoji cha chanika wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaam bondia huyo machachari awapo ulingoni amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa mchezo huo kitongoji cha chanika ambapo zimekuwa zikiandaliwa ngumi kwa ajili ya kuamasisha mashabiki kupenda mchezo huo wa masumbwi nchini

Akizungumzia historia yake ya maisha ya ngumi bondia huyo alisema alianza kuupenda mchezo wa masumbwi tangu miaka ya nyuma akivutiwa zaidi na Rashidi Matumla ambaye alikuwa akifanya vizuri katika mchezo huo wa masumbwi hapa nchini

Ngange aliyezaliwa Oktoba 10 mwaka 1989 amesema noto zake ni kuwa bingwa wa unia wa mchezo wa masumbwi nchini kwani tangu aanze kucheza kumi ni miaka miwili iliyopita

ambapo alianza kufundisha na bondia Said Mbelwa nae kutoka kitongoji cha chanika  ambaye ucheza mechi nyingi za nje ya nchi na kufanya atambulike kimataifa zaidi

Ngange ambaye ameshacheza michezo 8 kushinda 5 na kupigwa 3 alisema kuwa michezo ni ajira kubwa kwa vijana endapo watazingatia sheria na miiko ya mchezo huo kwani ina uwezo wa kukutoa kimaisha kama alivyo fanikiwa mwenzetu akimtaja bondia saidi mbelwa ambaye takribani kila mwezi uwenda ulaya kucheza mapambano ya ubingwa likiwemo lile la kulitakia amani nchi ya Afghanistan alipocheza za bondia Hamid Rahimi     Oktoba 30,2012 wakati akigombea mkanda wa WBO Inter-Continental middleweight title

Ngange katika maisha yake ya kawaida yeye ni mpiga debe wa mabasi yanayokwenda chanika buguruni na bondia anakubalika na wapiga debe wenzie kuongoza amani kituoni kwako kwakuwa wao kwa sasa ni kioo cha jamii na wanakubalika na wananchi mbalimbali katika kitongoji hicho

bondia huyo ana kumbuka mmpambano mmoja ambao alicheza na Jonas Segu ambaye alimpa tabu sana na kupoteza mchezo huo kwa point daa nilikutana na kigingi yule jamaa anajua sana mana pale ningepogwa kwa K,O lakini nika jitutumua mpaka kumaliza nae mpambano wote kwa kuwa na mimi niliandaliwa vizuri na kocha wangu Rasta Banju ambaye ndio nipo nae mpaka sasa

na mafanikio yangu ya kufanya vizuri ulingoni ni kuwasikiliza makocha na kufuata wanacho kisema wao ndio na ukiongezea na mazoezi basi wewe utakuwa unaweza kudumu sana katika mchezo

hila kwa sasa natamani kupambana na bonia machachali awapo ulingoni anae nolewa na Kambi ya Ilala si mwingine kwa sasa ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jamaa anajua na ni mzuri sana awapo ulingoni ila na mimi nataka ajue kuwa wapo wanaojua kama yeye bondia huyo anae nolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa mwiba pindi anapo kutana na mabondia wenzie ulingoni

Bondia huyo amewaomba waau mbalimbali kujitokeza kuzamini mchezo wa masumbwi ili uendelee kuwa na hamasa nchini kutokana na watu wengi kuupenda mchezo huo

kwani ni ajili moja wapo kwa vijana endapo wadhamini wakienderea kujitokeza basi vijana wengi watakuwa na muhamko wa kupenda mchezo wa masumbwi nchini na kututangaza kimataifa zaidi

Saturday, October 5, 2013

KLITSCHKO AMSHINDA POVETKIN KWA POINTI, PAMBANO LAO LILIJAA KUKUMBATIANA SANA





Wladimir Klitschko amefanikiwa kumshinda Alexander Povetkin kwa pointi baada ya kucheza kwa raundi 12.

Hata hivyo, pambano hilo halikuwa zuri sana kutokana na mabondia hao kutumia muda mwingi wakikumbatiana.
Ilionekana Klitschko alisoma uchezaji wa Mrusi huyo na zaidi alikuwa anahofia ukali wa ngumi zake za kushtukiza, hivyo akatumia muda mwingi akimkumbatia.
Pamoja na kukumbatia Klitschko alikuwa akipiga ngumi za kushtukiza ambazo zilionekana kumwelemea Povetkin na mara nne alishindwa kujizuia na kulamba sakafu.
Hata hivyo, baada alilalamika kwamba aliangushwa mara mbili tu na zilizobaki alisukumwa mpinzani wake Klitschko ambaye alimshinda kwa pointi 119-104.

ADAMU NGANGE AMGALAGAZA HUSSEIN GOBOSSY

Bondia Adamu Ngange kushoto akipambana na Hussein Gobossy wakati wa mpambano wao wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi wa Sonata uliopo chanika Dar es salaam jana Ngange alishinda kwa K,O ya raundi ya nne picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Adamu Ngange kushoto akipambana na Hussein Gobossy wakati wa mpambano wao wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi wa Sonata uliopo chanika Dar es salaam jana Ngange alishinda kwa K,O ya raundi ya nne picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Adamu Ngange katikati akiwa na kocha wake
Bondia Hussein Gobossy  kushoto akipambana na Adamu Ngange wakati wa mpambano wao wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi wa Sonata uliopo chanika Dar es salaam jana Ngange alishinda kwa K,O ya raundi ya nne picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Adamu Ngange akisubili kupigana na mpinzani wake
Bondia Adamu Ngange kulia akimwangalia bondia HUSSEIN GOBOSSY ambaye alikimbia uringoni kwa kipigo kikali ambapo mvua ya makonde ilikuwa ikimwelemea
Bondia Adamu Ngange akinyosha mikono juu baada ya mpinzani wake kuingia mitini kwa kukimbia mchezo huo

Friday, October 4, 2013

DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH '' 0713406938''

MPAMBANO WA EVANDER HOLYFIEL VS RIDDICK BOWE YA TAREHE 13,NOVEMBA,1992 NA YA TATU YA TAREHE 4,NOVEMBER 1995 ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Bus
iness Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


BONDIA DANNY GARCIA AKIWA NA MOJA YA TUZO ZAKE ALIZOWAI KUPATA
BONDIA MKONGWA WA MASUMBWI DUNIANI GEORGE FOREMAN DVD YAKE NAYO IPO TAYARI
MABONDIA MUHAMMAD ALI VS JOE FRAZIER MICHEZO YAO YOTE MITATU WALIO CHEZA IPO KWENYE DVD MOJA PEKEE AMBAPO UTAONA MAPAMBANO YOTE LIVE
BONDIA LENNOX LEWIS VS VITAL KLITSCHKO

MABONDIA Juan Manuel Marquez na Tim Bradley bingwa kucheza na mayweather

MABONDIA Juan Manuel Marquez na Tim Bradley wanatarajia kupanda ulingoni oktober 12 mwaka huu ambapo mabondia hawo waliowai kumtwanga bondia machachari Manny Paquai wamelezwa kuwa mpambano huo ndio utakaotoa dila ya nani acheze na bondia bingwa asiyepigika duniani Floyd Mayweather ambaye hivi karibuni alimtwanga kwa point bondia machachari na kijana mdogo kiumri canelo alvarez ambaye ndie aliyewanyanyasa mabondia wengi na kustop kwa Mayweather JR sasa kinachosubiliwa siku dakika na saa

Wednesday, October 2, 2013

IDD MNYEKE ALIVYO MSAMBALATISHA Keis Amal

Refarii wa mchezo wa masumbwi nchini Saidi Chaku akimwinua mkono juu bondia Idd Mnyeke kuwa mshindi baada ya kumsambalatisha, Keis Amal wengine kushoto ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wengine kulia ni kocha Cristopher Mzazi na Ramadhani Shauli picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Idd MNyeke kushoto akipambana na Keis Amal wakati wa mpambano wao wa masumbwi mnyeke alishinda kwa point
Bondia Idd MNyeke kushoto akipambana na Keis Amal wakati wa mpambano wao wa masumbwi mnyeke alishinda kwa point
Bondia Keis Amal kushoto akipambana na Idd Mnyeke wakati wa mpambano wao Mnyeke alishinda kwa point
Refarii wa mchezo wa masumbwi nchini Saidi Chaku  kutangazwa kwa matokeo ya  Idd Mnyeke kuwa mshindi baada ya kumsambalatisha, Keis Amal wengine kushoto ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wengine kulia ni kocha Cristopher Mzazi na Ramadhani Shauli picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA PANANDI PANANDI ILALA OKTOBA 26

MPAMBANO mwingine wa masumbwi kufanyika katika ukumbi wa panandi panandi Oktoba
26 mpambano huo wa mchezo wa masumbwi utakaokuwa chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition utawakutanisha mabondia mbalimbali wenye majina na wanaotamba kwa sasa katika anga za masumbwi nchini

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda

pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali

Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
 
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi