Tangazo

Pages

Tuesday, July 9, 2013

TPBO LTD KUSIMAMISHA SHUGHULI ZOTE ZA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA ZA ULINGONI KIPINDI CHA RAMADHANI



NDG ZANGU WAPENDWA KTK MICHEZO

UONGOZI WA ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO-LIMITED],

UNAPENDA KUWAJULISHA WADAU WOTE WA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA ,KWAMBA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI TUNASIMAMISHA SHUGHULI ZOTE ZA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA ZA ULINGONI MPAKA HAPO MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UTAKAPOMALIZIKA.

HII HAINA MAANA KWAMBA OFISI ZETU ZITAFUNGWA BALI NYAKATI ZA KUFANYA KAZI ZA OFISI PIA ZITABADILIKA , ,BADALA YA OFISI KUFUNGULIWA SAA 2.00  ASUBUHI KAMA ILIVYO KAWAIDA HADI SAA 12.00 JIONI,

SASA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI OFISI ZITAFUNGULIWA KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI HADI SAA 9.00 JIONI.

 NA  KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI TUTAKUWA TUNARATIBU MAPAMBANO AMBAYO YATAFANYIKA BAADA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KUISHA [MUNGU AKITUJAALIA KUUMALIZA SALAMA TUKIWA HAI.]

UONGOZI WA ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO-LIMITED UNAWATAKIA WAISLAMU WOTE CHINI TANZANIA HERI NA BARAKA NYINGI KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

NA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIDUMISHE AMANI TULIYONAYO KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MFUNGO WA RAMADHANI.

                                                      IMELETWA KWENU NAMI;-

                                                 YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                          
                                                        +255-713-644974 ,752-335584

Monday, July 8, 2013

MABONDIA WA TANZANIA THOMAS MASHALI NA FRANCIS MIYEYUSHO WAWACHAPA WAKENYA KWA KO



Bondia Francis Miyeyusho (kushoto) akizipiga na Shadrack Muchanje kutoka Kenya.
Thomas Mashali (kulia) akichapana na Patrick Amote kutoka nchini Kenya.

PAMBANO LA HALIMA MDEE NA JACQUELINE WOLPER HAKUNA MBABE



 Mbunge wa Kawe Halima Mdee (kushoto) akichana na Msanii wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, wakati wa Tamasha maalum la Usiku wa Matumaini, lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Mabondia hao walitooka sare kwa pointi.
 Bondia Halima Mdee akiingia kwa mbwembwe.
Wolper akipanda ulingoni kwa mbwembwe.

Saturday, July 6, 2013

KASEBA AINGIZA FILAMU YA BONGO MAFIA MTAANI



BINGWA wa mchezo wa Kick Boxing nchini Chapion Japhert Kaseba ameingia katika fani ya utoaji filamu za mapigano Live akianzia na picha yake ya kwanza itakayo mtambulisha inakwenda kwa jina la Bongo Mafia

Filamu hiyo iliyo rekodiwa katika ubora wa hari ya juu sasa ipo mtaani Ikisambazwa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya wapenzi wa filamu nchini wajionee vitu tofauti kidogo kwani kuna wakali kibao alio washirikisha 
Picha hiyo ni mfululizo za picha zake nyingine ambazo zipo njiani kwani amekuja kufanya kazi katika jamii  ili watambue ipi pumba na upi mchele
Bongo mafia ilioshilikisha wasanii kama vile ,Dotnata,Kelvin,Muhogo Mchungu,Pendo Njau Champion na Rogers MASTER SHIVO,na Wasanii wengine kibao

Amesema filamu hiyo kwa sasa ni gumzoo mtaani wakati ndio kwanza inamaliza wiki moja tangu kuingia sokoni 

Kaseba ambaye hivi karibuni ali mdunda bondia Rasco Simwanza wa Malawi amejitamba kuendeleza ubabe  kwa mabondia wengine huku akifanya kazi zake za sanaa ambazo kwa kiasi kikubwa anamshukuru sana Dotnata kwa kuona kipaji chake hicho ambacho kilikuwa kimejificha na sasa kipo mtaani

Kaseba amesisitiza kwa mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua kazi hiyo kwani ndio kwanza ananza kulishika soko la filamu hapa nchini endapo wataendelea kumunga mkono na ndipo watakapofuraia kazi zake nyingi zilizopo jikoni kwani nina kazi tofauti tofauti Nne hivi na sijui nianze na ipi ndio mana nimeamua kutoa hii kwanza alisema Kaseba

Tuesday, July 2, 2013

MAANDALIZI USIKU WA MATUMAINI WAPAMBA MOTO



 


JACOB STEVEN 'JB' AJIFUA KUMCHACHAFYA IDD AZZAN KATIKA USIKU WA MATUMAINI J'PILI HII


Jacob Steven 'JB' akijifua kwa ajili ya mpambano wake na Idd Azzan utakaofanyika katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013.
Jb akipiga pushapu kadhaa wakati wa maandalizi hayo.
JB akiwa tayari kumkabili Idd Azzan.MSANII nguli wa Filamu nchini, Jacob Steven 'JB' akifanya mazoezi ndani ya The Atriums Hotel kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wa ndondi kati yake na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 7 mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini. (Picha na Denis Mtima/GPL)