Tangazo

Pages

Friday, March 9, 2012

ZENGWE TRA LAMKABILI MANNY PACQUIAO


Hii ni picha ya maktaba iliyopigwa Mei 7, 2011, Manny
Pacquiao wa Philippines (kulia) akizipiga na Shane Mosley wa Marekani
(kushoto)katika pambano la taji la WBO, uzito wa Welter kwenye ukumbi wa
Garden Arena, MGM Grand mjini Las Vegas, Nevada. Marekani, Manny Pacquiao
anakabiliwa na kesi ya kukwepa kodina Maofisa wamesema leo watatoa tamko rasmi
kama mbabe huyo milionea amelipa kodi

Wednesday, March 7, 2012

TPBO YAMPONGEZA KOCHA WA NGUMI KIMATAIFA SUPER D

oanaizesheni ya ngumi za kulipwa inakupa pongezi na shukrani nyingi kwako Rajabu Mhamnila 'Super D' kwa jinsi unavyoutendea haki mchezo wa ngumi za aina zote za kulipwa na za ridhaa.
tunalazimika kutowa maneno mazuri na ya faraja kwako kwa kuwa umekuwa muhamasishaji mkubwa sana wa mchezo wetu huu ambao umetengwa na wadhamini lkn una wapenzi wengi tu katika nchi yetu ya Tanzania.
 umekuwa ni msaada mkubwa sana katika kila maandalizi ya mchezo kwa kuwasaidia waandaaji [mapromota [ ambao hupungukwa vifaa vinavyohusu mchezo hususan glovus na kadhalika, pia umekuwa ukifuatilia mapambano ya ngumi popote pale hata mkoani ,na huku ukiripoti yote yanayofanyika huko ukiwa nje ya Dar es salaam kwa galama zako mwenyewe.
hali kadhalika umekuwa ukiwasaidia mabondia wa mikoani kwa kuwauzia vifaa vya mchezo kwa bei ndogo kuliko hata ile ya madukani , hivyo kuwawezesha mabondia hao kuwa na uwezo wa kumiliki vifaa vya ngumi kiurahisi.
sisi TPBO.tunayo macho yenye kuona na kuthamini michango ya watu wa aina yako hivyo tunakuahidi kukupatia cheti cha kuthamini mchango wako katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi  , ktk wakati muafaka utakapofika.
pia ni kwa mwakilishi wa SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA [WORLD PROFESSIONAL BOXING FEDERATION LENYE MAKAO MAKUU NCHINI MAREKANI,
NITAKUWA NIKIKUPATIA TAARIFA MUHIMU ZA JINSI GANI MABONDIA WA KULIPWA WA TANZANIA WANAINGIZWA KWENYE VIWANGO VYA SHIRIKISHO HILI KUBWA,ILI WAWEZE KUPATA NAFASI YA KUGOMBEA MIKANDA YA SHIRIKISHO HILI KUBWA.
NINAAMBATANISHA KWAKO  HATI YA UTEUZI WA KUWA MWAKILISHI WA SHIRIKISHO HILI ILIWATANZANIA WAHABARISHWE KUPITIA MTANDAO WAKO NA WASHIRIKA WAKO
THANX IN ADVANCE
YASSIN ABDALLAH-USTAADH
RAIS -TPBO NA MWAKILISHI WA WPBF NCHIN TANZANIA

Tuesday, March 6, 2012

SELEMANI GALILE VS THOMAS MASHALI KUGOMBANIA UBINGWA WA TPBO


MKANDA wa ubingwa wa ngumi za kulipwa wa TPBO (Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa) unatarajia kuwaniwa April 9 mwaka huu Dar es Salaam.

Mkanda huo ambao upo wazi utawaniwa na bondia kati ya Thomas Mashali na Selemani Galile uzito wa kg 75 middle weight.

Akizungumza Dar es Salaam na mtandao wa www.superdboxingcoach, juu ya maandalizi yake Galile alisema amejiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua mkanda huo ambao upo wazi kwa sasa.

"Naendelea kufanya mazoezi yangu kwa ajili ya kuwania mkanda huu ambao ninaamini utaweza kunitambulisha ubora wangu katika tasnia hii ya masumbwi,"alisema Galile.

Alisema kuhusu mpinzani wake Mashali hana hofu naye kwa kuwa mchezo huo huamua nani mkali atakayetwaa ubingwa wakati wakiwa ulingoni na si nje ya hapo na kwa sasa nimepata staili mpya za mabondia wa dunia.

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa Kimataifa wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye,Lenox Lewis,Evalnder Holfilder na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

BONDIA Wladimir Klitschko ameweka rekodi ya kushinda mechi 50 kwa KO

 



BERLIN, Ujerumani
baada ya kutetea ubingwa wake wa uzito wa juu kwa kumtwanga raundi ya nne, Jean-Marc Mormeck.

Mpiganaji huyo raia wa Ukraine bingwa wa WBA, IBF na WBO alionekana kuwa katika kiwango cha juu kwa uchezaji katika pambano la upande mmoja lilichezwa mwishoni mwa wiki ESPIRIT Arena mjini Dusseldorf.

Kwa mujibu wa Sky Sports Klitschko alimmiliki mpinzani wake kabla ya kummaliza kwa ngumi kali ya kushoto baada ya kufika dakika ya 10.

Mormeck, ambaye ni bingwa zamani wa uzani wa cruiser ambaye alipigwa na David Haye mwaka 2007, alisema kabla ya pambano kuwa ataingia ulingoni bila ya kuwa na mashaka lakini hakuonekana kama aliamini kuwa angeweza kumalizwa mapema.

Badala ya yake Klitschko alitawala mechi na kuboresha rekodi yake na kuwa 57-3, huku akishinda mechi saba kwa kumaliza raundi zote ulingoni.

Klitschko alianza vya pambano hilo kwa nguvu huku akibadilishana ngumi na mpinzani wake.

Katika raundi ya pili ilionekana wazi kuwa Mormeck alikuwa na wakati ngumu dhidi ya mpinzani wake ambapo aliangushwa baada ya kupata konde la mkono wa kulia.

Mormeck alinyanyuka lakini mashabiki kiasi cha 50,000 waliona dhahiri kuwa ilingumu kwake kumaliza vizuri.

Klitschko aliendeleza mvua ya ngumi raunsi ya tatu ambapo alitupa makonde mchanganyiko, licha ya kwamba alionywa na refa kwa kumsukuma Mormeck na kumwangusha.

Shughuli iliisha raundi ya nne ambapo ngumi yua mkono wa kulia ilitua kwa Mormeck ambapo alionekana kulewa kabla ya kuanguka jukwaani.

Baada ya kuanza kuhesabiwa Mormeck alijaribu kunyanyuka lakini refa, Luis Pabon alimaliza pambano ili kuepusha madhara zaidi kwake

Saturday, March 3, 2012

FLOYD MAYWETHER NA MIGER COTTO KUPAMBANA MWEZI WA TANO


BABONDIA FLOYD MAYWETHER NA MIGER COTTO WAKIWA WAMEPOZI KUTANGAZA MPAMBANO WAO MWEZI WA TANO

TPBC KUANZISHA TAASISI YA RASHID MATUMLA SPORTS ACADEMY





Katika juhudi za kuwaenzi wanamichezo walioliletea sifa kubwa taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) iko kwenye mchakato wa kuanzisha Taasisi ya Michezo ya Rashid Matumla (Rashid Matumla Sports Academy) ya kuibua vipaji vya vijana wanaochipukia katika michezo hususan ngumi.





Huu ni mkakati wa kumwandaa bingwa wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (Rashid Matumla) kustaafu ngumi ili aweze kutumia kipaji chake cha ngumi kuendeleza vijana.


TPBC inajivunia historia nzuri ya Rashid Matumla kwa kuwa bondia wa kwanza Tanzania kuwa bingwa wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) pamoja na sifa kemkem alizoliletea taifa hili kipindi hiki chote anachopigana ngumi. Tunapenda kuutangazia umma kuwa tunamwandalia Rashid Matumla mazingira mazuri ya kustaafu ngumi.


Katika taasisi hiyo ya Rashid Matumla Sports Academy, Rashid atakuwa ndiye Rais na atakuwa analipwa mshahara kama mwajiriwa kwa kipindi chote cha uhai wa taasisi hiyo na kumfanya aweze kujipatia ajira ya kudumu wakati hachezi tena ngumi. Huu ni moja ya mikakati ya TPBC kuhakikisha kuwa mabondia wake walioiletea nchi hii heshima kubwa wanaenziwa kwa kuandaliwa maisha mazuri wanapostaafu ngumi!
Ni lazima kama taifa tuwajali wale wote wanaolipigania taifa hili na tutaendelea pia kuandaa mazingira mengine ya kuwawezesha waishi vizuri na kuheshimiwa daina ili kuleta changamoto kwa wengine ili nao wapigane kufa na kupona kuliletea sifa taifa letu katika michezo.

Taasisi hii itazinduliwa rasmi wakati wa mpambano wa Rashid Matumla na Vitaly Shemetov bondia anayetoka Urusi litakalofanyika mjini Moshi tarehe 22nd Juni na kuhudhuriwa na Mcheza sinema maarufu wa Marekani, Deidre Lorenz wa sinema maarufu ya Santorini Blue. Mcheza sinema huyo atakuwepo nchini kwa ajili ya kukimbia mbio za Marie Frances Mt. Kilimanjaro Marathon kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika zikazofanyika tarehe 24 Juni mwaka huu kuanzia Moshi Club.



Taasisi ya Rashid Matumla Sports Academy ambayo itakuwa inafanya kazi nchi nzima itajumuisha pia bingwa mwingine wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) Magoma Shaban. Hawa wote watakuwa waajiriwa wa taasisi ya Rashid Matumla Sports Academy wakifanya kazi za kuibua vipaji kwa vijana Tanzania nzima!

Thursday, March 1, 2012

BO


Bondia wa kike Mchezo wa Masumbwi Pendo Njau akiwa amepozi baada ya kujifungua salama na anawashukulu wadau wote kwa kumuombea na kwamba yupo njiani kurudi katika mchezo huo hivi punde

Bondia Pendo Njau akiwa amepozi na MTOTO WAKE






Bondia Pendo Njau kulia akiwa amepozi na mtoto wake siku ya kushudia mpambano wa Maneno Osward na Rashid Matumla