Tangazo

Pages

Thursday, September 15, 2011

Khan aombea Ortiz apigwe



Khan aombea Ortiz apigwe
na Mayweather

LONDON, Uingereza
AMIR Khan hataki rafiki yake Victor Ortiz ampige Floyd Mayweather Junior kesho kwa kuwa anataka kupiga na mbabe huyo.

Ortiz atapiugana na Mayweather mjini Las Vegas keszho na Khan anataka ‘Pretty Boy’ abakie kuwa bondia asiyepigwa hadia yeye atakapopambana naye k0atika mechi ainayotaraj iwa kuchezwa Agosti mwakani.

Victor ni mpiganaji mzuri, lakini sipendi ashinde,” alisema bingwa wa WBA na IBF uzani light-welter n kukaririwa na Daily Mirror.

"Ninataka kwua wa kwanza kupigana naye na kumshinda."

Sioni kama Ortiz atashinda, ingawa ana nguzu zaidi, Mayweather ana uzoefu zaidi na ufundi.”

BONDIA KALAMA NYILAWILA ATAFUTA PROMOTA KWA AJILI YA KUPAMBANA NA CHEKA


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Kalama Nyilawila amesema kwa sasa ameanza mchakato wa kutafuta promota kwa ajili ya kumuandalia pambano dhidi ya francis Cheka ili aweze kutetea ubiungwa wake wa WBO.

Akizungumza na majira jana, Kalama alisema, kutokana na malengo yake ya kutaka mkanda huo ubaki hapa nchini hivyo alionelea kucheza na Cheka kutokana na kuwa na uwezo mkubwa na hasa mchezo mzuri aliouonyesha katika pambano lao la marudiano dhidi yake na Mada Maugo kwa kumtandika na kumzidi tofauti ya pointi.

Alisema, kwa sasa ameishaanza kusaka promota ambapo bado wapo katika mazungumzo ya awali ambapo watakapoa afikiana ndipo watapanga tarehe halisi ya kufanya pambano hilo ikiwa ni pamoja na mahali.
"Kama nilivyosema sitaki mkanda huu utoke nje hivyo nikifanikiwa kucheza na Cheka itakuwa faraja kwangu kwani najua uwezo wake na hata anatambulika Duniani hivyo haitakuwa vibaya kwani naye alishawahi kucheza mapambano ya Kimataifa," alisema Kalama.
Aliongeza kuwa wakati wa yeye kutetea ubingwa huo umefika ambapo akishindwa kucheza na bondia wa hapa nchini anatakiwa kutafuta pambano la nje ya nchi ili kuweza kutetea ubingwa huo kiyu ambacho yeye hakitaki lakini ikishindikana kupata pambano hilo itabidi atafute pambano la nje.

Wednesday, September 14, 2011

ISSA SEWE AJIFUA KUMKABIRI RAMADHANI SHAULI

 Kocha Mkongwe wa mchezo wa ngumi Nchini Habibu Kinyogoli'Masta' (kushoto) akimwelekeza jinsi ya kutupa masumbwi bondia, Issa Sewe wakati wa maoezi yanayorndelea ya kambi ya Ilala Sewe atapambana na Ramadhani Shauli mwishoni mwa mwezi ujao.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Haye adai Lewic kampa dawa

DAVID Haye amesema ameamua kuchelewa kustaafu ngumi kutokana na kutaka kupigana na Vitali Klitschko ili kuutwaa ubingwa wake wa WBC.
Mpiganaji huyo wa London alipigwa na nduguye Vitali, Wladimir Julai awali alisema kuwa anataka kustaafu ngumi baada ya kusherekea miaka 31 ya kuzali kwake  mwezi ujao.
Lakini Haye,  ambaye alidai kuwa alipigana huku akiwa na maumivu kutokana na kuvunjika kidole cha mguu na kupoteza ubingwa wa WBA,  amesema kuwa anataka kupiganba na Klitschko mkubwa.
Vitali mwenye miaka 40,  alitetea ubingwa wake kwa kushinda katika raundi ya 10 dhidi ya mpiganaji wa Poland, Tomasz Adamek Jumamosi.
kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Haye anataka kupigana na na mpinzani wake mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 raia wa Ukraine baada ya kuzungumza na bingwa wa zamani wa dunia Lennox Lewis alipokuwa Jamaica Julai mwaka huu.
Haye alisema: “Nimefikiria kila kitu baada ya kuzungumza na familia yangu na kukutana na Lennox mjini Montego Bay. Tuliuuzungumza na  Lennox alinipa vitu muhimu kwa ajili ya kupiga Vitali, kama alivyofanya 2003.
“Vitali anatakwia kunipatia nafasi, kama anajisikia.”
Vitali bado ana uchungu kutokana na Haye kuvaa fulana iliyokuwa na picha inayomwonesha ameshika kicha chake na nduguye vilivyochinjwa, Jumamosi hakutaka kuzungumzia kuhusu kuwepo kwa pambano hilo kwenye uwanja waWembley.
Vitali alisema: “Haye ni mpiganaji anayeongea mambo machafu katika ngumi. Amenigusa binafsi na ninataka kumtwanga.”

Monday, September 12, 2011

Klitschko atetea taji lake la WBC KWAKUMTWANGA, TOMASZ ADAMEK





BONDIA Vitali Klitschko ametetea vyema taji lake la uzani wa juu linalotambuliwa na Shirikisho la Masumbwi Ulimwenguni WBC baada ya kumsimisha mpinzani wake,Tomasz Adamek katika raundi ya 10 ya pmbano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana mjini Wroclaw.
.

Kwa mujibu wa Shirika la Habri la Marekani AP,mwamuzi kutoka Italia, Massimo Barrovecchio alisimamaisha pmbano hilo dakika mbili na sekunde 20 ili kumnusuru bondia huyo baada ya kupokea makonde mfululizo kutoka kwa bingwa huyo raia wa Ukrain.

AP iliripoti kuwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 40, Klitschko alikuwa akimzidi mpinzani wake kwa urefu wa inchi sita mpinzani wake jambo ambalo lilimsaidia kumbana Adamek mwenye umri wa miaka 34 katika raundi ya pili,sita na tisa.

Kwa ushindi huo Klitschko amedhihirisha ushindi wake wa mapambano 43-2 yakiwemo 40 aliyoshinda kwa knockout huku Adamek akiendelea kubaki na ushindi wake wa mapambano 44-2.

Kwa matokeo hayao pia yanamfanya Klitschko na mdogo wake Wladimir kutetea ubingwa wao mara tatu katika uzani wa juu katika mashindano yote.

“Nadhani mwamuzi amewafanya maamuzi sahihi . Lakini alipaswa kufanya hivyo mapema ,” alisema Wladimir,ambaye anashikilia mataji ya IBF na “super” WBA sambamba na mataji ya WBO na IBO.

Wladimir alisema kuwa pambano jingine la Klitschko litakuwa ni Desemba mwaka huu.

FLOYD MAYWETHER KAPAMBANA NA VICTOR ORTIZ



BONDIA

FLOYD Mayweather Jnr le atapanda ulingoni Septemba 17,2011 kupambana na Victor Ortiz kuwania ubingwa wa WBC.

Mayweather Jnr amekuwa kama ng'ombe wa maziwa wa kutoa fedha katika ngumi, licha ya kuwa nchi yake imekwua na matatizo ya kifedha wahasibu wa nyota huyo hawana mashaka na jambo kama hilo.

Atapambana na Victor Ortiz kuwania ubingwa wa dunia wa WBC uzani wa welter mjini Las Vegas wiki ijayo.


Pambano hilo litaoneshwa katika Primetime na Mayweather anatarajia kuaingia pauni milioni 25 kwa kupitia televisheni hiyo.

Katika mapambano yake yaliyopita ambayo watu walikuwa wakilipia ili kuona alikusanya jumla ya pauni milioni
250.

Licha ya kuwa ni bingwa wa dunia mara tano na hajapigwa katika mechi zake 41,
Mayweather amepigiwa kura chache za umaarufu.

Anatwangana na Ortiz ambaye alikimbiwa na mama yake wakati akiwa na umri wa miaka saba na baba yake alikuwa na kawaida ya kupinga hadi alipoondoka.


Victor ambaye sasa ana umri wa miaka 24,alianza ngumi akiwa na miaka 10 kabla ya kaunza ngumi za kulipwa akiwa na miaka 17, aliwahi kufanya bishara ya kuuza dawa za kulevya.

Kocha Rolando Arellano alisema: "Victor ame[ita katika mageti mageti ya ahera. Ni mtu mbaya ulingoni."

Kikikaririwa na gazeti la Sun Ortiz alimwelezea mpinzani wake akisema: "Floyd ni mpiganaji mzuri lakini sikuwahi kufikia ri kuwa mzuri sana."

Inaonekana kuwa Mayweather anaweza kuwandabisha kwa maneno yake.

Baada ya pambano hilo pengine linaweza kuwepo pambano jingine linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi kati ya
Mayweather na Manny Pacquiao,

Sunday, September 11, 2011

DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI

DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI ZIPO MTAANI KWA AJILI YA MAFUNZO YA MCHEZO HUO HIVI SASA KWA MATAJI YA JUMLA NA REJAREJA PIGA SIMU 0787/0774/0715/0754/0733/0713-406938 AU FIKA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI 0652755838