Bondia Ramadhani Shauli akiwa ameushika Mkanda wa I.B.F Africa wakati ulipokuwa ukioneshwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwasili Dar es salaam ukitokea USA mkanda huo utakaogombaniwa na Shauli na bondia Sande Kizito kutoka Uganda utafanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Diamond Jubilee kushoto ni Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Madaraka Nyerere na Promota wa mpambano huoMkurugenzi wa Kitwe General Traders, Lucas Rutainirwa http://superdboxingcoach.blogspot.com/ |
■ Wamfananisha na mcheza sinema maarufu wa Marekani.
■ Tabasamu lake lawadanganya wapinzania wake.
Mtanzania Ramdhani Shauri atapanda ulingoni siku ya Idd pili kupambana na bondia Sande Kizito kutoka Uganda kugombea mkanda wa IBF katika bara la Africa katika uzito wa unyoja (Featherweight).
Shauri anayefanya mazoezi yake Ubungo, maeneo ya Mabibo na anafundishwa na kocha mzazi anayetamba kuwa na mabondia wenye nidhamu na vipaji vya hali ya juu.
Ramdhani Shauri ni bondia chipukizi mwenye umri wa miaka 19 na historia yake ya ngumi inafurahisha kila anayeisoma na kuisikia. Ana haiba nzuri inayovutia na anafananishwa na bondia Sugar Ray Leonard wa Marekani kutokana na haiba yake na upiganaji wake.
Sugar Ray Leonard alitamba katika miaka ya 70 na 80. Shauri ni Mfalme anayekuja na hivi sasa anatishia maisha ya mabondia wengi katika bara la Afrika.
Ramadhani Shauri ana nidhamu ya hali ya juu na maisha yake katika ngumi yanafurahisha kwa jinsi anavyoishi kwa nidhamu na kufanya mazoezi ya kujijenga katika ngumi. Katika maisha yake anajiepusha sana na matatizo ambayo vijana wengi wametumbukia kama vile uvutaji wa bangi, ngono zembe na mambo mengine yasiyo na malengo katika maisha.
Huyu ndiye kweli Mfalme anayekuja katika ngumi za kulipwa na nchi yetu imepata bahati kubwa sana kuwa na kipaji cha bondia kama huyu.
Mpambano wa Shauri umepewa jina la “The Rumble in the City of Heaven’s Peace” (Vurumai katika Jiji la Amani).

Watanzania, tumuezi mwenzetu Ramadhani Shauri anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Naomba utumie picha yake kweye mtandao akiwa na mkanda wa IBF
Imetumwa na;
Onesmo
Ngowi
Rais wa IBF bara la
Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi
Rais wa kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)
Mkurrugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC)
No comments:
Post a Comment