Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli katikati
akiwaelekeza mabondia Yohana Robert KUSHOTO NA Ibrahimu Class jinsi ya
kutupa masumbwi kwa mpizani kwa kunyoosha mkono Class anajiandaa na
mpambano wake na Simba Watundulu siku ya Idi pili katika ukumbi wa
Diamond Jublee jijini Dar es salaam.Picha na www.superdboxingcoach. |
Na Mwandishi Wetu
KAMBI ya ngumi Ilala ipo kwenye maandalizi mazito ya kumnoa bondia Ibrahimu
Class 'Ibra Mawe' anaetarajia kuzipiga na Simba Watundulu katika uzito wa KG,60
litakalofanyika siku ya Idi pili katika ukuimbi wa Diamond Jublee
Akizungumza mmoja wa makocha wa kambi ya ilala inayongozwa na Kocha mkongwe wa
mchezo huo Habibu Kinyogoli, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema katika kipindi
hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wanamwandaa bondia Ibrahimu Class kwa ajili
ya mpambano huo utakaofanyika siku hiyo
Super D alisema wamemuandaa bondia wao kufanya vizuri hili kuweza kumzibiti
mpinzani wake kwa kuwa wanamjua uchezaji wake awapo ulingoni hivyo wanamfundisha
mbinu mpya kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake
Kambi hiyo ya ngumi imewataka wadau wa mchezo uho kuja kuangali mchezo mzuri wa
masumbwi utakaoneshwa na bondia wao kutoka kambi ya ilala
Ibrahimu Class anaetamba kwa jina la Ibra Mawe yupo chini ya maandalizi makali
chini ya makocha wake Kinyogoli na Super D kwa ajili yampambano huo na kuwataka
wapinzani wake kwa sasa wakae chonjo kwa kuwa moto umesha washwa na akuna wa
kuuzima kwa bondia huyo chipkizi na mwenye nia ya kuupaisha mchezo wa masumbwi
Kimataifa mabondia hawo watakuwa wakicheza katika mpambano wa utangulizi wa
RAUNDI 6 uku pambano kuu ni kati ya Ramadhani Shauli wa Tanzania na Sande Kizito
wa Uganda watakaopambana kugombania mkanda wa Ubingwa wa IBF se3sAfrika
No comments:
Post a Comment