Tangazo

Pages

Friday, July 13, 2012

BONDIA JUMA FUNDI NA BAINA MAZOLA KUPIMA UZITO KESHO

Bondia Juma Fundi kushoto na Baina Mazola wakitunishiana misuri wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBO leo mpambano wao utafanyika julai 15 katikati ni Promota wa mpambano huo Kaike Siraju
 
Na Mwandishi Wetu
Bondia Juma Fundi na Baina Mazola wanatarajia kupima Uzito kesho katika ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es salaam kwa ajili ya mpambasno wao wa ubingwa utakaofanyika siku ya jumapili katika Ukumbi wa DDC Kariakoo mpambano huo wa Ubingwa wa TPBO 
kaike promotion imeandaa pambano lingine la ubingwa wa taifa kati BAINA MAZOLA na JUMA FUNDI(ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia nchini philipines) litakalopigwa jumapili ya tarehe 15 mwezi wa saba,pambano hili ni mtiririko wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi na wale tunaowategemea kwenda kuchukua mikanda mikubwa ya dunia.


 Inafahamika wazi kwa taifa letu,mchezo wa ngumi ni miongoni mwa mchezo unaopeperusha vema bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio na wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kishidashida bila ya utaalam mzuri wa uongozi utaalam upo katika uchezaji na mchezo unaohitaji msaada wa hali ya juu sana kuinuliwa.wadhamini wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa letu.



mchezo wa tarehe 15july utasimamiwa na Tpbo na mapambano yamepangwa na ibrahim kamwe chini ya uratibu wa kaike siraju yataongozwa na mapambano ya utangulizi kati bondia anaechipukia kwa kasi issa omar(toka bigright boxing mwananyamala) na Ramadhan kumbele bingwa wa taifa toka kambi ya matumla-keko.

Anthony Mathias(aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi mwaite juma(toka bigright boxing) mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini  na katika picha ni issa omar akinolewa na mwalimu wake Ibrahim bigright

DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim kamwe
TICKETS; +255 715 707777

Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round super feather weight - doi miyeyusho v/s shaban mtengela 6 round light weight - Bakari mohamed v/s sadiki momba - 6 round. Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja Mtagwa anayefanya shughuli zake Marekani. DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi, DVD hizo zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D.
 

No comments:

Post a Comment