Tangazo

Pages

Sunday, July 8, 2012

CHEKA AMGWAYA KASEBA TAIFA


Bondia Francis Cheka usiku wa leo amegoma kuzipiga na mpinzani wake, Japhet Kaseba katika pambano lililotakiwa kufanyika Uwanja wa Taifa, kwa visingizio ambavyo haviingii akilini.
Ulipowadia muda wa mabondia hao kupanda ulingoni, Kaseba alipanda akiwa tayari amevalia vifaa vya michezo kasoro glavu ambazo alizikuta ulingoni na baadaye MC akamuita Cheka. Ajabu Cheka alipanda kama hahusiki na pambano, akiwa amevalia kiraia.
Akaomba mic azungumze, lakini MC akanyima naye akaamua kuteremka ulingoni. Ni kama kuna siri ilikuwa inaendelea, ambayo waandaaji walikuwa wanaijua. Yaasin Abdallah ‘Ustadh’ rais wa TPBO, alimchongea Cheka kwa mashabiki kwamba, amefanya kitendo kisicho cha kiungwana kwa kula fedha ya promota na kugoma kupigana.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kitendo hicho ambacho hakika si cha kiunamichezo na kingeweza kuhatarisha amani uwanjani kama mashabiki waliolipa fedha zao kwenda kuwaona wawili wakizipiga, wangeamua ‘kulianzisha’, hakika Cheka hakuwa na hoja za msingi kukwepa kukipigana.
Alidai mpinzani wake amepigana mapambano matatu, kapigwa mawili hivyo ni kibonde si sawa yake hawezi kupigana naye na pia walipopima uzito alikutwa na uzito mdogo, hivyo pia si sawa yake na hawezi kupigana naye. Lakini swali ambalo hakujibu ni kwa nini alisaini mkataba na kuchukua malipo ya kupigana, halafu anagoma kupigana. Pichani Kaseba akivaa glavu ulingoni tayari kwa pambano.

Francis Cheka (mwenye T-sheti nyekundu) akitoka ulingoni baada ya kushindwa kupambana na Kaseba.
...Cheka akitoka nje ya ulingo.

Cheka anapiga story na Thomas Mashali 

Andoka Cheka

kama anataka kurudi

Anaamua tu kuondoka zake

Baba yake Kaseba kulia akiwa na mdogo wake Japhet

Japhet hana mpinzani ulingoni

Japhet baada ya kupewa ushindi 

Cheka anazungumza na Waandishi

Anateremka ulingoni

No comments:

Post a Comment