Gottlieb Ndokosho kushoto akiwa kazini.
Mtanzania
Rajabu Maoja bondia mzoefu katika ngumi za kulipwa kutoka mkoa wa Tanga
atapanda ulingoni Septemba 1 kupimana ubavu na bondia Gottlieb Ndokosho
bingwa wa ngumi nchini Namibia.
Mpambano
huo unaofanyika katika jiji na Windhoek, nchini Namibia unawakutanisha
mabondia wawili ambao wanazimudu vizuri ngumi ulingoni. Hii ni mara ya
kwanza kwa bondia wa Kitanzania kugombea mkanda wa IBF katika bara la
Afrika nje ya nchi tangu mpambano katia ya Iraq Hudu na Ali Said wa
Kenya ulivyofanyika jijini Mombasa mwaka 2000.
Wawili
hao wataumana kwenye mpambano uliopewa jina la “The Battle for the
Kalahari Desert” (Vita ya Jangwa la Kalahari)na waandaaji wa mpambano
huo ambao ni Kinda Boxing Promotion chini ya promota Simon Nangolo wa
nchi ya Namibia. Namibia iko Kusini Magharibi mwa bara la Afrika
ikikingana na Afrika ya Kusini, Botswana na Angola.
Mtanzania
Rajabu maoja anatokea katika jiji la tanga na ni mkali aliyejijengea
umaarufu mkubwa katika masumbi hapa nchini. Maoja ni kati ya mabondia
wachache wenye majina yanayotishia maisha baadhi ya mabondia wenzake
katuka bara la Afrika.
Katika
uhai wake wa ngumi Maoja amepigana mapambano 31 akishinda 18 na
kupoteza kwa kiduchu mapambano 10 ambayo mengi sio yenye hadhi yoyote ya
kumharibia historia yake kwemey ngumi na kutoka sare mapmbano matatu
(3)
Naye bondia Gottlieb Ndokosho ambaye ni bingwa wa Namibia amepigana pambano 15 na kushinda 11 wakati amepoteza mapambano 3.
Mpambano
huo uliopewa jina la The Battle for the Kalahari Desert (Vita ya jangwa
la Kalahari) utasimamiwa na Rais wa Shirikiso la ngumi la Kimataifa
bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo
Ngowi. Aidha Ngowi ndiye Rais w kamiehsni ya Ngumi za Kulipwa nchini
(TPBC) na mkurugenzi wa ngumi wa baraza la Ngumi la Jumuiya ya madola.
Watanzania, tumuezi mwenzetu rajabu maoja anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment