MTANZANIA RAMADHANI SHAURI KATIKA “RUMBLE IN THE CITY”
■ Atapambana na bondia kutoka Uganda kugombea mkanda wa IBF Afrika
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa IBF limetangaza rasmi mpambano kati ya bondia
Ramadhani Shauri wa Tanzania na Sande Kizito kutoka Uganda. Mpambano huo
utafanyika kutafuta bingwa wa “IBF Continental Afrika” katika uzito wa Unyoya (Featherweight) kilo 58 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-Es-Salaam
Bondia
Ramadhani Shauri anatoka katika kundi la kocha Mzazi lenye makao yake
makuu eneo la Mabibo. Shauri ana rekodi ya mapabano 12
ambapo katika maisha yake ya ngumi ameshinda mara 11na kupoteza mara 1. Naye bondia Sande Kizito ana rekodi ya mapambano 12 ambapo ameshinda mapamambano 7 na kupoteza 9
Aidha, bondia Nasibu Ramadhani atapambana na bondia Twalibu Mubiru toka Kenya kugombea mkanda wa “IBF East & Central Africa” katika uzito wa Bantam. Nassibu
Ramadhani ana rekodi ya mapambano 9 na kupoteza mara 2 wakati Twalib
Mubiru ana rekodi ya mapambano 11 amepoteza mara 7 na kutoka draw mara
2.
Mpambano
kati ya Ramadhani Shauri na Sande Kizito unafanyika wakati Tanzania
ikijijenga katika medani ya michezo ya kimataifa. Tayari Rais Jakaya
Mrisho Kikwete ameshakutana na viongozi wa vyama na taasisi mbalimbali
za michezo kujadili programu za kuiendeleza michezo hapa Tanzania.
Promota wa mpambano huo mkubwa uliopewa jina la “The Rumble in the City” ni mfanyabiashara maarufu katika jiji la Dar-Es-Salaam Lucas Rutainurwa wa kampuni maarufu ya Kitwe General Traders ya jijini Dar-Es-Salaam.
Kampuni
hii ndiyo iliyopromoti mpambano mwingine wa IBF mwezi wa Aprili ambapo
ulimshughudia bondia machachari wa Tanzania anayejiita kuwa mbunge wa
Rorya kwa wakazi wa jimbo hilo wanaoishi katika jijini Dar-Es-Salaam
Manda Maugo akipoteza katika raundi ya nane!
Nalo Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lilizindua program maalum ya “Utalii wa Michezo” katika
mkutano wake wa 29 uliofanyika mwezi wa Juni uliofanyika katika jijini
la Honolulu jimbo la Hawaii nchini Marekani ambayo imelenga kuinua
mchezo wa ngumi katika bara la Afrika wakati nchi za Ghana na Tanzania
ni nchi za mfano (Pilot Countries).
Katika programu hii ya “Utalii wa MIchezo” IBF
mbali na kuwapa nafasi mabondia kadhaa toka Tanzania na Ghana kugombea
mikanda mbalimbali itaendesha pia programu ya mikutano yake hapa
Tanzania na kuwaleta wanachama wake kupanda wa mlima Kilimanjaro kila
mwaka. Programu hii itawaleta watalii wengi nchini Tanzania na kutangaza
vivutio vya kitalii kupitia michezo
Tayari
bondia Helen Joseph wa Ghana anategemea kupanda ulingoni Agosti 11
kupambana na bondia Dahianna Santana wa Dominican Republic kugombea
mkanda wa dunia katika uzito wa unyoya (Featherweight) upande wa
wanawake. Mpambano huo utafanyika wiki mbili kabla ya mpambano wa
Ramadhani Shauri ya Sande Kizito.
Wakati
huo huo promota wa mpambano huo bwaan Lucas Rutainurwa akizungumza na
mwandishi wa habari hii alisema kuwa ameamua kuwekeza katika “Utalii wa Michezo” ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kujenga uchumi wa nchi ya Tanzania.
Rutainurwa
alisema kuwa ana ratiba ya mapambano ya ubingwa wa Afrika kila baada ya
miezi miwili mwaka huu na mwak akesho ambayo itaipa Tanzania nafasi ya
kunyanyua medani ya michezo pamoja na kuwawezesha vijana kujiajiri.
Ameziomba
kampuni pamoja na watu wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kusaidia
kufadhili mapamnano haya ili kuiwezesha Tanzania kuinuka kimichezo.
Imetolea na;
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission(TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
IBF/USBA President for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission(TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
No comments:
Post a Comment