Tangazo

Pages

Tuesday, August 23, 2016

Oscar De La Hoya na vituko kwa wanawake



Na Suit Jose, Madrid
BONDIA mstaafu wa Marekani mwenye asili ya hapa Hispania, Oscar De La Hoya anaweza kuwa na mali nyingi, lakini amefanya mambo ya ajabu sana.
Hoya anayetajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 200 ametuhumiwa na wanawake kwa vituko vyake alipokuwa nao hotelini, ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo zao za ndani.
Hoya alizaliwa Februari 4, 1973 mashariki mwa Los Angeles, California na ni mmoja wa mabondia wachache wa uzito wa juu kuwa mtu maarufu katika utamaduni wa pop.
Ametoka kwenye familia yenye historia ya ngumi, ambapo mwaka 1992 alilipatia taifa lake medali ya dhahabu baada ya kushiriki Michezo ya Olimpiki jijini Barcelona, Hispania.
Alikuwa ndio amehitimu masomo yake katika James A. Garfield High School na alikuja kujulikana kama ‘The Golden Boy’.
Amepanda ulingoni mara nyingi ambapo ameshinda mara 234 kati ya hizo kwa Knock Out (KO) ikiwa ni mara 163 na amepoteza mapambano sita tu katika ngumi za ridhaa na za kulipwa.
Alianza rasmi ngumi za kulipwa Novemba 1992 na kustaafu 2009 akiwa na amepigana katika uzani sita tofauti na kuwashinda mabingwa 17 wa dunia na ni mmoja wa mabondia waliotengeneza fedha zaidi.
Katika vituko vyake, Hoya anadaiwa kwamba akiwa kwenye hoteli ya Ritz Carlton jijini New York, alimbeba mwanamitindo wa jijini hapo Angelica Marie Cecora (25).
Hoya anadaiwa kuwa kama chizi, kwa jinsi alivyokuwa akicheza cheza chumbani humo, akavaa chupi ya Cecora na kuanza kuruka ruka kama mwanasarakasi na baadaye akavaa sketi yake.
Mwanadada huyo anadai walifanya ngono kabla ya Hoya kuagiza dawa za kulevya aina ya cocaine kuingizwa chumbani humo, kisha akaanza kumtisha.
Hii ni mara ya pili Hoya anatuhumiwa kuvaa chupi za kike, kwani mara ya kwanza alifanya hivyo kwa chupi ya mrembo wa Siberia, Milana Dravnel ambaye anadaiwa alilipwa dola milioni 20 mwaka 2008.
Hoya anadaiwa kuwasiliana na Cecora ili amliwaze baada ya safari ndefu ya kutoka Irak alikokuwa ameenda kuwasalimu wanajeshi wa Marekani.
Kwamba alikuwa anataka kustarehe baada ya kupitisha muda mrefu pasipo kutumia kilevi, mihadarati na wanawake.
Hata hivyo, Hoya alificha jina lake, akadaiwa kwamba alikuwa anaitwa Thomas Crown, jina la milionea aliyetumika kwenye filamu ya ‘Thomas Crown Affair’ iliyochezwa na Pierce Brosnan 1999.
Cecora aligundua jina la kweli la mwenzake huyo wakati wa chakula cha jioni baada ya kujisahau na kuiona kadi yake ya benki.
“Kuna vitu vingi alivyofanya ambavyo siwezi hata kuelezea … alivaa nguo yangu ya ndani tena ikamwenea vizuri tu, akavaa na sketi yangu,” mwanadada huyo aliliambia gazeti la The New York Post. 
Baadaye msichana huyo alimwalika rafiki yake wa kike chumbani wakakaa kabla ya kumtisha Hoya hadia kaondoka.
Hata hivyo ilipofika asubuhi, wasichana hao wawili walijikuta katika hali mbaya na deni la dola 1,500.
Hata hivyo, meneja wa Hoya alifika baadaye na kulipa deni hilo lililotokana na vitu walivyokula na chumba walichotumia.
Mwanasheria wa Cecora, Tony Evans anasema aliyofanya Hoya ni mambo mabaya na ni mfano anuai wa matumizi mabaya ya nguvu zake kwa kuwadhalilisha wanawake.
Hoya ana asili ya Hispania, ambapo babu yake, Vicente, baba Joel Sr. na kaka yake, Joel Jr wote walikuwa wana ndondi. Hoya alikuwa bondia wa mwaka 1995, akapewa tuzo.
Hoya alianzisha kampuni ya promosheni ya ngumi inayokwenda kwa jina la ‘Golden Boy Promotions’.
Huyu ni Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Hispania kumiliki kampuni ya promosheni ya ngumi kati ya mapambano aliyoshindwa ni mara mbili kutoka kwa mikono ya Shane Mosley.
Mama yake, Cecilia, aligunduliwa kuwa na saratani ya matiti na alifariki dunia 1990 na akiwa kwenye kitanda chake cha mauti alieleza matumaini kwamba mwanawe angekuja kutwaa medali ya dhahabu kwenye Olimpiki, na kweli ikawa hivyo.
Hoya anasema kwamba alijituma vilivyo kwenye mazoezi na pia katika ulingo kwa ajili ya kutimiza ndoto za mama yake, hata baada ya kufariki kwake dunia.

No comments:

Post a Comment