SAFU hii inaendelea kuhusu sheria za mchezo
wa ngumi, aina na staili za upiganaji na mambo mengi yanayouzunguka mchezo huu
ambao unapendwa na wengi.
In-fighter/Swarmers
In-fighters/swarmers
(wakati mwingine huitwa "pressure fighters") ni aina ya upiganaji
ambapo bondia anakuwa hakai mbali na mpinzani wake, anakuwa ana kwa ana kila
aendako.
Lakini
jambo kubwa si kukaa ana kwa ana na mpinzani bali ni umahiri wao wa kurusha
makombora mchanganyiko yaani ‘combinations’ hasa ‘hooks na uppercuts’.
Mpiganaji
wa aina hii anahitaji kuwa mlinda kidevu chake mzuri kwani mara nyingi
upiganaji huu hushambuliwa na ngumi ya mdonowo yaani ‘jab’ kabla ya wao kufanya
kile wanachokusudia.
In-fighters
hutumia staili hii ya upiganaji kwa kuwa wengi wao huwa ni wafupi kuliko
wapinzani wao na hivyo kulazimika kupigana kwa makombora ya masafu mafupi na
yenye kasi kupata ushindi.
Hata
hivyo, baadhi ya mabondia warefu katika uzito mbalimbali wamekuwa pia
wakipigana kwa staili hii, mfano ni Mike Tyson aliyewahi kuwa maarufu sana kwa
‘uppercuts’ zake zilizokuwa na madhara makubwa kwa wapinzani, pia Julio César
Chávez, mabondia wengine ni Wayne McCullough, Amir Khan, Harry Greb, Jack
Dempsey, Rocky Marciano, Joe Frazier, David Tua na Ricky Hatton.
Counter puncher
Counter
punchers ni mabondia ‘wanaoteleza’ wenye kupigana kwa kujilinda zaidi na
kutumia zaidi makosa ya mpinzani wake. Silaha yao kubwa ni kutumia makosa ya
mpinzani na kuchukua pointi au hata kushinda kwa KO.
Hutumia
muda mwingi kujikinga kuhakikisha wanazuia kila aina ya ngumi isiwapate na
wakati huohuo kwa haraka kurusha makombora zaidi kwa kutegemea makosa ya
mpinzani wake.
Mpinzani
wake anaposhambulia yeye ndipo hupata mwanya wakati huohuo kulenga shabaha
sehemu wazi iliyoachwa na mpinzani wake, kwa kuwa ni kawaida mtu anaposhambulia
sehemu ya uso wake na nyingine huwa zinabaki wazi pasipokulindwa.
Hata
hivyo, ili uwe mpiganaji wa staili hii, unapaswa kuwa na sifa zifuatazo. Uwe na
mnyambuko (good reflexes), uwe mwenye kujaliwa akili ya upiganaji
(intelligence), uwe na shabaha ya makonde (punch accuracy), lakini zaidi ya
wepesi uwe na mikono mwepesi yenye kasi
( good hand speed).
Baddhi ya
mabondia katika kundi hili ni Jim Corbett, Jack Johnson, Laszlo Papp, Jerry
Quarry, Anselmo Moreno, Chris Byrd, Bernard Hopkins, Vitali Klitschko, James
Toney, Marvin Hagler, Evander Holyfield, Juan Manuel Márquez, Humberto Soto,
Floyd Mayweather Jr, Roger Mayweather, Pernell Whitaker na Max Schmeling.
·
Mchanganyiko wa staili
Mabondia
wote duniani huwa na ujuzi wa msingi, ambapo kila bondia anapoanza ngumi
hujikuta akitumia staili moja ambayo kwake inampa raha zaidi au inamfaa zaidi.
Lakini
wanapokomaa katika fani hiyo lazima wawe na ujuzi wa zaidi ya staili hiyo
waliyozoea ili wanapokutana na aina nyingine ya wapiganaji waweze kumudu
pambano mfano, bondia wa staili ya ‘out-fighter’ atahitajika kutumia staili
kukita miguu yake na kutumia staili ya ‘counter punch’, au kutumia mbimu za
‘slugger’ ili kuweza kumudu kupigana na bondia mwenye nguvu za mikono.
·
Staili dhidi ya staili
Je, kuna
staili iliyo bora zaidi kuliko nyingine? Kinachokubalika na ambacho ni sahihi
ni kwamba hakuna staili iliyo bora kuliko nyingine, zote zina faida yake na
hasara yake lakini zaidi inategemea bondia mwenyewe anavyotumia staili yake
isipokuwa kuna staili ambayo ina faida dhidi ya staili nyingine.
Mfano,
mpiganaji wa staili ya ‘in-fighter’ ana faida anapopigana na mpiganaji wa
‘out-fighter’, mpiganaji wa staili ya
‘out-fighter’ ana faida anapokutana na bondia wa staili ya ‘puncher’, bondia
‘puncher’ ana faida dhidi ya bondia ‘in-fighter’.
Huu ni
mzunguko ambao unafanya kusiwepo na staili iliyo bora kuliko nyingine kwakua
staili moja inaweza kuwa bora ya nyingine lakini ikawa dhaifu kwa nyingine.
Kwa asili
sababu nyingine zinazochangia ubora wa staili husika ni kipaji, ujuzi na akili
ya bondia mwenyewe pia aina ya mazoezi anayofanya na ndio maana kuna msemo
kwamba staili hutengeneza upiganaji ("styles make fights"),
Ndiyo
maana unakuta kwa mfano Joe Frazier alikuwa mzuri na kumsumbua sana Muhammad
Ali, lakini alikuwa ‘nyanya’ kwa George Foreman ambaye naye alikuwa ‘nyanya’
kwa Ali.
**Mwandishi ni kocha wa
mchezo wa ngumi anayefundisha klabu mbalimbali Dar es Salaam. Anapatikana kwa
simu 0713/0787- 406938 au email: superdboxingcoach@gmail.com
No comments:
Post a Comment