Bondia maarufu kuliko wote Tanzania Francis
Cheka atamvaa Udiadia Mwahia kutoka nchini DRC Kongo kugombea mkanda wa ubingwa
wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya
Uajemi.
Mabondia hao watakutana katika mpambano wa kwanza tangu Arusha liwe
jiji katika uwanja wa Shekh Amri Abeid tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing
Day!
Akimtambulisha Francis Cheka kwa waandishi wa habari katika ukumbi
wa Melezo jijini Dar-Es-Salaam leo, mratibu wa mpambano huo na ambaye alishawahi
kuwa bingwa wa Tanzania kwenye ngumi za ridhaa George Andrew alisema kuwa bondia
Udiadia Mwahila anakaa Lusaka Zambia ambako ndipo anapofanya shughuli zake za
ngumi chini ya promota maarufu Anthony Mwamba!
Udiadia ana rekodi ya mapambano 12 na ametoka sare
pambano moja na hajapoteza hata moja wakati Francis Cheka ana rekodi ya
mapambano 33 amepoteza 6 na kutoka sare pambano moja.
Geporge alisema kuwa mpambano huo utatumika kulitangaza jiji la
Arusha kama Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika na kulifananisha jiji la
Arusha na jiji la Geneva lililoko nchini Switzerland.
Mpambano huo
unakuja wakati ambapo mpambano mwingine wa Francis Cheka na bondia kutoka
Ujerumani wa kugombea mkanda wa IBF wa mabara ulifutwa baada ya Simon kuumia
katika mazoezi.
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya
Uarabu na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi alisema kuwa wao kama IBF wamesharuhusu
maandalizi ya mpambano huo. Rais huyo aliwataka wadhamini pamoja na wananchi wa
mkoa wa Arusha na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi ili kulifanya pambano hilo
kuwa la mafanikio.
No comments:
Post a Comment