TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
NOVEMBER 14, 2012
Bondia maarufu
kuliko wote Tanzania Francis Cheka atamvaa Udiadia Mwahia kutoka nchini DRC
Kongo kugombea mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya
Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mabondia hao
watakutana katika mpambano wa kwanza tangu Arusha liwe jiji katika uwanja wa
Shekh Amri Abeid tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day!
Akimtambulisha
Francis Cheka kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Melezo jijini
Dar-Es-Salaam leo, mratibu wa mpambano huo na ambaye alishawahi kuwa bingwa wa
Tanzania kwenye ngumi za ridhaa George Andrew alisema kuwa bondia Udiadia
Mwahila anakaa Lusaka Zambia ambako ndipo anapofanya shughuli zake za ngumi
chini ya promota maarufu Anthony Mwamba!
Udiadia ana rekodi
ya mapambano 12 na ametoka sare pambano moja na hajapoteza hata moja wakati
Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza 6 na kutoka sare pambano
moja.
Geporge alisema
kuwa mpambano huo utatumika kulitangaza jiji la Arusha kama Las Vegas ya ngumi
katika bara la Afrika na kulifananisha jiji la Arusha na jiji la Geneva
lililoko nchini Switzerland.
Mpambano
huo unakuja wakati ambapo mpambano mwingine wa Francis Cheka na bondia kutoka
Ujerumani wa kugombea mkanda wa IBF wa mabara ulifutwa baada ya Simon kuumia
katika mazoezi.
Naye Rais wa IBF
katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi
Onesmo Nhowi alisema kuwa wao kama IBF wamesharuhusu maandalizi ya mpambano
huo. Rais huyo aliwataka wadhamini pamoja na wananchi wa mkoa wa Arusha na
mikoa mingine kujitokeza kwa wingi ili kulifanya pambano hilo kuwa la
mafanikio.
Naye bondia Francis
Cheka alisema kuwa amejiandaa kwa kiasi kikubwa na atazidi kufanya mazoezi ili
kupata ushindi kwake pamoja na nchi ya Tanzania. Aliendelea kusema kuwa kila
Mtanzania anajua uwezo wake kwa hiyo amewataka wote wafike kwa wingi ili kupata
uhondo na burudani tosha!
Imetolewa na;
GEORGE ANDREW
MRATIBU WA MATUKIO
J.B ADVERTISEMENT
& PROMOTIONS
P.O BOX 3143,
ARUSHA, ATNZANIA
TEL: 0754-333829
Email: andrewgeorge632@gmail.com
No comments:
Post a Comment