Tangazo

Pages

Monday, November 12, 2012

BAINA MAZOLA NA MWAITE JUMA KUZIPIGA JUMAPILI


 
Bondia Baina mazola toka katika gym ya mzazi respect ya mabibo atazipiga na mtoto wa mwananyamala Mwaite Juma katika pambano lisilo la ubingwa  la raundi nane.
pambano litakalofanyika katika ukumbi wa DID hall wa mabibo la kugombania kuwania kucheza ubingwa,kwani mshindi wa pambano hilo atakuwa na nafasi ya kucheza pambano la ubingwa na bondia bingwa wa uzito huo.
pambano hilo lililoandaliwa na kuratibiwa na Christopher mzazi lina lengo la kunyanyua vipaji vya mabondia chipukizi litawakutanisha mabondia wenye upinzani na uhasama toka sehemu mbalimbali ili wamalize kiu zao,kwani kuna baadhi ya vijana hao kuna waliofikia kupigana mitaani na wengine kurushiana maneno makali na kutishiana kuwa kila mmoja mbabe kwa mwenzake. hivyo wameandaliwa pambano wamalize bifu na kiu zao ili waendelee na mchezo kama mchezo kwa kunyanyua na kuendeleza vipaji vyao kwa manufaa yao kama ajira na maendeleo kwa taifa.
Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo na taratibu zote za mchezo wa ngumi zipo katika hatua ya mwisho kukamilikaa na mapambano ya utangulizi yatakuwa  kama inavyoonesha hapo chini.
 
Date  ;18/11/2012
Venue;  D.I.D Hall-mabibo, Tanzania
Promoters; Bigright Promotion,Mzazi respect and 'no talking gym'
Matchmaker; Christopher "Mzaz'i
 
Bantam weight - MWAITE JUMA V/S BAINA MAZOLA  8 round
 
light fly - HERMAN SHEKIVULI V/S OMAR MAKUSUDI  4round
 
light fly - MARTIN RICHARD SHEKIVULI V/S SHOMARI PENDEZA  4round
 
light fly - ISSA OMAR V/S JAMES MARTIN 6round
 
 
wealter weight - ABDALAH LUWANJE V/S SAID MUHIDIN 6 round
 
light weight - mpole mackenzie v/s Adam Barnaba. 4 round
 
super fly - Shadrack juma v/s Ramadhan ustadh 4 round
 
  Ngoyi Gaudence v/s Idd Mbishi 4 round

No comments:

Post a Comment