Kocha
wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto
akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia
Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili
bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa
na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
KIU kubwa aliyonayo katika mchezo wa ngumi ndiyo unaomfanya bondia wa zamani wa klabu za Simba, Reli na Amana, Rajabu Mhamila 'Super D' ndiyo iliyomfanya kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia na kuendeleza vipaji vipya vya mchezo huo.
Mwishoni mwa mwaka jana kocha huyo anayetambuliwa kimataifa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Duniani (AIBA) alifanya ziara mikoani ili kuhamasisha ngumi akigawa pia DVD zenye (clips) za mapambano ya mabondia mbalimbali nyota ili watu wajifunze mchezo huo.
Pia mapema mwaka huu amejitolea akigawa vifaa vya michezo kwa baadhi ya klabu za ngumi lengo likiwa kuwahamasisha vijana kujifunza na kuucheza mchezo huo bila ya matatizo ya ukosefu wa vifaa.
Aligawa vifaa hivyo katika klabu ya Uhuru Gerezani, pia amekuwa akisaidia na kuuza vifaa vya ngumi kwa bei rahisi katika michuano na mapambano mbalimbali za ngumi za ridhaa na zile za kulipwa ili kusaidia kuendelea mchezo huo.
Super D, pia amekuwa akiendelea kuwanoa mabondia chipukizi katika klabu za Amana akisaidia na wazoefu wa kazi hiyo Habib Kinyogoli na Kondo Nassor na klabu yake ya Ashanti iliyoshirikina kufanya vyema michuano ya Kombe la Taifa na Klabu Bingwa ya ngumi.
Super D anasema japokuwa kazi ya ukocha wa ngumi imekuwa hailipi na pengine ndiyo sababu ya mabondia wengi wa zamani waliostaafu mchezo huo kutopenda kuifanya, lakini yeye anafurahia kwa kuona vijana waliopitia mikononi mwake wakipata mafanikio na kuwa tishio.
Baadhi ya vijana wanaotamba wakipitia mikononi mwake ni Erck Magana,Husein Pendeza, Mussa Mchopanga,Juma Bigrii, Ibrahim Class 'King Class Mawe', Idd Mnyeke, Mussa Sunga na wengineo.
"Nafarijika kuona vijana niliowaibua kupitia klabu ya Ashanti Boxing wakizidi kuwa tishio, nadhani muda si mrefu watavaa viatu vya akina Rashid Matumla, Joseph Marwa na wakali wengine," anasema.
Anasema bila kujali kama ananufaika au la, furaha yake ni kuona mchezo wa ngumi ukizidi kusimama na kuendelea kuibua vipaji vipya ambavyo anaamini watakuja kuwa faida ya baadaye kwa taifa.
Super D baba wa watoto wawili, Zainabu Mhamila 'Ikota' (11) na Saada Swedi (16) mtoto wa kuasili, anasema kumekuwa na vikwazo vingi katika kuendeleza ngumi nchini hasa suala la wafadhili na wadhamini.
Anasema wafadhili na wadhamini wamekuwa wazito kujitokeza kuupiga tafu mchezo huo na mabondia kwa ujumla kitu ambacho hakujua kinasababishwa na nini ilihali huo ni mchezo kama michezo mingine.
"Tatizo kubwa katika ngumi ni suala la udhamini, ngumi zimesahauliwa sana na hata wafadhili kwa mabondia nalo ni tatizo, japo inaelezwa ubabaishaji unaofanywa na wasimamizi wa ngumi ni sababu," anasema.
Anasema ni wajibu wa wasimamizi wa ngumi na wadau kwa ujumla kupigana kurekebisha hali ya mambo ili kutoa ushawishi kwa wadhamini na wafadhili kujitokeza kuwapiga tafu.
Rajabu Mohammed Mhamila 'Super D' alizaliwa mwaka 1977 jijini Dar akiwa mtoto wa pili kati ya wanne wa familia yao na alianza kupenda michezo tangu akiwa mdogo.
Mwenyewe anasema aliyemuingiza kwenye ngumi ni baba yake mzazi, Mzee Mhamila 'Chuck Norris, aliyekuwa mnyanyua vitu vizito na 'gateman' wa ukumbi wa DDC Kariakoo aliyekuwa akiwalazimisha kufanya mazoezi bila kupenda akidai anataka wawe fiti.
Mazoezi hayo na kule kumuona akinyanyua vitu vizito vilimfanya taratibu ayafurahie mazoezi kabla ya kuanza kupenda ngumi kwa kuvutiwa na mabondia Muhammad Ali na George Foreman.
Anasema mwanzoni mwa miaka ya 1980 alipelekwa klabu ya Simba na mjomba wake aliyewahi kuwa bondia tishio nchini, Iraq Hudu 'Kimbunga' na ikawa mwanzo wa safari yake ndefu katika ngumi mpaka
Super D anasema mbali na yeye pia kaka yake Shaaban Mhamila "Star Boy', na wadogo zake Rashid Mhamila 'Nature Fire' na 'Mohamed Hemed' 'Kadogo Ninja' wote walitamba kwenye ngumi enzi zao wakipigwa tafu na mazoezi ya baba yao aliyekuwa pia mwanamieleka.
Baada ya kupata mafanikio akiwa Simba akishiriki michezo kadhaa, alihama kujiunga klabu ya Reli kisha baadae Amana, ingawa hakupata mafanikio makubwa.
Anasema kati ya michezo yote aliyocheza hawezi kusahau pambano dhidi ya Roger Mtagwa anayeishia kwa sasa Marekani, ambapo anakiri aklichakazwa isivyo kawaida.
"Siwezi kumsahau Mtagwa kwani alinipa kichapo kutokana na jamaa alijua ngumi na alileta yupinzani wa ali ya juu kwani nilipofika raundi ya tano nilikuwa nimeumia taya," anasema.
Anamshukua kocha wake, Habib Kinyogoli pamoja na mabondia mahiri nchini kama Maneno Osward, Japhet Kaseba, Kalama Nyilawila,Fransic Miyeyusho pamoja na uongozi Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) kwa kumtia moyo katika juhudi zake za kuendeleza mchezo huo.
No comments:
Post a Comment