Francis Miyeyusho: Uswazi kunaharibu wanamichezo
Kwa ufupi
- Maeneo ya ‘uswazi’ ndipo uhuni wa kila aina hufanyika kama vile ngono holela, lugha c
Katika Jiji la Dar es Salam maeneo kama Tandale,
Temeke, Magomeni, Manzese, Keko, Kinondoni ni baadhi ya maeneo yenye
sifa hizo. Maeneo ya Morogoro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Mbeya nazo
zimesheheni sifa hizo.
Katika hali isiyo ya kawaida mabondia wanaofanya
vizuri na kujizolea umaarufu nchini wamekuwa wakitokea kwenye maeneo
hayo ya uswazi, hii inawezekana inachangiwa na aina ya mchezo.
Mchezo huo wa ndondi huhitaji watu wakakamavu,
wenye stamina na uvumilivu ambao ni vigumu sana kuwapata maeneo ya
‘Kishua’ kama Mbezi Beach, Mikocheni na Masaki.
Kauli ya Miyeyusho kuhusu bangi
Alipoulizwa kuhusu shutuma kuwa mabondia wengi
wanajihusisha na uvutaji wa bangi, Bondia Francus Miyeyusho alisema,
“Unajua mabondia wengi tunatokea uswahilini ambako hayo mambo ndio
yanafanyika. Ndiyo maana utakuta baadhi ya mabondia wanatumia vitu
hivyo.”
“Hili siyo la mabondia tu ila hata wanaocheza
michezo mingine kama soka, riadha na kikapu wanaotokea maeneo yetu haya
ya uswahilini utakuta wanatumia.” Aliongeza Miyeyusho anayeishi
Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho anadai kuwa malengo ya kutumia vitu
hivyo yanatofautiana, ambapo wengine hutumia kama starehe wakati wengine
hutumia ili iwasaidie kupata hamasa ya mchezo.
Mkali wa ‘Knockout’
Katika mapambano 47 aliyopigana Miyeyusho, 32
yalimalizika kwa ‘knockout’. Kati ya mapambano hayo 32, mapambano 23
alishinda kwa knockout na kupoteza tisa kwa knockout akiwa ndio bondia
pekee wa Tanzania mwenye rekodi ya kushinda michezo mingi kwa ‘knockout’
na kushindwa mingi kwa staili hiyo hiyo. Katika michezo kumi
aliyopoteza tisa amepoteza kwa ‘knockout’
“Mimi huwa napenda kuimaliza michezo yangu kwa
‘knockout’ kwa sababu mara nyingi ushindi wa pointi humalizika kwa
utata. Wengine huona kama bondia amependelewa ushindi kitu ambacho siyo
sahihi.”
“Nimepoteza mapambano mengi kwa ‘knockout’ kwa
sababu ya kuwa na maandalizi duni, kutokana na hali ndogo ya kipato
likitokea pambano hata kama sina mazoezi huwa nakubali ili nipate fedha
japo ninajua sitaweza kushinda.
No comments:
Post a Comment