Tangazo

Pages

Tuesday, September 10, 2013

Wageni washuhudia madudu katika masumbwi Tanzania


 
Na Mwandishi wetu
MAPEMA siku mpya ya Agosti 31 ikiwa ndio inaanza kujongea Bondia Fransis Cheka akatangazwa kuwa ndio bingwa wa pambano la kimataifa la kugomea mkanda wa dunia wa WBF baada ya kumtandika Phil Willams wa Marekani.
 
Hakika kila Mtanzania alifarijika kuona Tanzania inafungua ukurasa mpya baada ya Cheka kufanya vizuri katika pambano hilo lililojaa umakini na ufundi kabla ya kumpata bingwa wa mkanda huo wa dunia katika uzito wa kati.
 
Naamini kila m Mtanzania hadi kufikia wakati huu atakuwa anajua matokeo hayo ya Cheka kuwa bingwa wa dunia katika mkanda huo na kufanya Tanzania kuanza kupita tochi ya kufanya vizuri kimataifa.
 
Katika hilo nampongeza mratibu wa pambano hilo kwa uzalendo aliouonesha katika kwa kuwatafutia mabindia watanzania mapambano hayo makubwa ambayo yameifanya Tanzania kung'ara kimataifa.
 
Kitu ambacho naamini ni cha msingi kukisema ni madudu katika maandalizi yake katika sula zima la kuwalipa mabondia fedha zao mapema kabla ya mchezo au baada ya mchezo kulingana na mkataba jinsi unavyojieleza.
 
Kila mmoja anaamini kuwa panapokuwa na makubaliano yasiyo na shaka inasaidia kuondoa changamoto zisizo za msingi kama zilizojitotikeza katika pambano la Agosti 30 kuamkia 31 mwaka huu ya ubingwa wa WBF Afrika na dunia.
 
Nasema kutokana na maandalizi kuonekana ya ubabaishaji hali iliyofanya baadhi ya mabondia kugoma kuingia ulingoni hadi walipwe fedha zao hali iliyokuwa ikitishia usalama wa watu waliokuwepo ukumbini kwa maana lolote lingeweza kutokea.
 
Kwa maana watu lukuki walioingia ukumbi walikuwa wamelipa fedha zao kwa lengo la kutaka kuona burudani kibaya zaidi wachache tayari walikuwa wamelewa kwa maana ingekuwa rahisi kwao licha ulinzi kuwepo kutumia nafasi hiyo kufanya fujo.
 
Baada ya mchezo wa pili kati ya Deo Njiku wa Morogoro na Allain Kamote kutoka Tanga kumalizika na kutakiwa Alphonce Mchuamiatumbo na Chipa Chipindu kupanda ulingoni waligoma hadi walipwe gfedha zao.
 
Hali hiyo iliendelea hata katika pambano la Mada Maugo na Thomasi Mashali hali iliyofanya mashabiki kukaa zaidi ya nusu sasa bila mchezo kuanza hali iliyofanya baadhi ya wadau kuanza kuwabembeleza mabondia wapande ulingoni na wafuate fedha zao asubuhi ya Agosti 31.
 
Ni ukweli nguvu kubwa ilitumika kuwashawishi mabondia hao kupanda ulingoni jambo ambalo binafsi nawapongeza wanamasumbwi hao kwa kudai haki zao mapema kwani wapo mabondia waliowahi kupanda ulingoni na mrataibu akashindwa kuwalipa stahiki zao.
 
Binafsi naliita tukio hilo kuwa ni la aibu kutokana na pambano hilo kuwa la kimataifa ambalo lingehitaji  maandaliz yake kuwa ya si ya kubabaishaji na kuonesha madudu mbele ya wageni wa kimataifa waliokuja kuangalia mapambano hayo.
 
Bingwa wa zamani wa dunia wa mchezo huo wa Afrika Kusini, bondia Francois Botha alipoulizwa kama amelipwa fedha za ujio wake akabaini kuwa alikuja kwa mradi maalum wa kampeni ya kuhamasisha kuzuia Malaria hivyo hakuna alichotakiwa kulipwa.
 
Alipoulizwa kuhusu malipo yake, Botha aliyewahi kupigwa kwa mbinde na bingwa wa zamani wa dunia, Mmarekani, Mike Tyson alisema yeye amekuja kwa mradi maalum wa kampeni kuzuia Malaria na hana anachodai katika mchezo huo.
 
Hata hivyo Botha alishangazwa mabondia wa Tanzania kupanda ulingoni bila kupatiwa chao mapema na kupingoza kwa mabondia kugoma kupanda ulingoni hadi wapitiwe fedha zao na kulaani hali iliyojitokeza kwa wanamasumbwi kutolipwa mapema.

Kutokana na madudu hayo yaliyofanyika ukumbini hapo, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. David Mathayo akabainisha kuwa tukio hilo limeiletea aibu taifa na kutoa mwito, kuwashughulikiwe ili kutoa funzo kwa wengine.
 
"Haya jamaa inaonesha hawakujipanga vya kutosha katika kuandaa pambano hili na kufanya badala mchezo kuupandisha ndio wanaushusha kwa sababu zisizo za msingi hivyo ni vema wakashughulikiwa ili kutoa funzo kwa wengine," alisema Dk. Mathayo.
 
Pia mdau wa mchezo huo ambaye aliwahi kuwa promota wa mchezo huo Jamali Malinzi, waandaji wa pambano hilo walitakiwa kuwapa mabondia hao fedha zao mapema kama alivyokuwa akifanya wakati huo kulingana na makubaliano.
 
Aliongeza kuwa waandaaji hawatakiwa kusubiri fedha za mlangoni ndizo zitumike kuwalipa mabondia, kwa kufanya ni kurudisha nyuma mchezo huo na kutoa mwito ili kuondokana na changamoto hiyo promota anatakiwa kuwa na fedha za kutosha.
 
Pia maandazli ya mchezo huo yalionekana kuwa na upungufu hata katika usalama wa viongozi kwani hata baadhi yao walikuwa wakienda maliwatoni bila ya kuwa na ulinzi licha ya kuwa na watu wa tabia tofauti kitu ambacho kilikuwa ni hatari kwa viongozi hao.
 
Usalama mdogo ulionekana wazi wakati Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenella Mukangara  alipopanda ulingoni kumvika mkanda Cheka wa ubingwa watu wengi wakawa wamejazana ulingoni na kuhatarisha usalama kwa kiongozi huo.
 
Mama Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi wa pambano hilo alionekana kupita kwa taabu kwenda kumvika mkanda shujaa wa Tanzania 'SMG' kutokana na mashabiki kujazana ulingoni bila kuwepo kwa ulinzi wa kutosha wa kumpa nafasi kiongozi huyo kufanya alichotakiwa kukifanya.

Kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha kwa Waziri huyo, Malinzi ndiye akabeba jukumu la kumuondoa ulingoni na ukumbini bila hata waratibu kufahamu hilo kitu ambacho ni hatari kwani kama kungekuwa na wabaya kwa wangeweza kumdhuru kwa urahisi.
 
Waziri hata alipokuwa akishushwa na kuwekewa ulinzi na Malinzi alionekana wazi usoni alikuwa na babaiko huku akiwa haamini kama anatoka salama katikati ya vijana walioshiba wakiwa wanaharuka kwa furaha huku wakimnyanyua juu Cheka.
 
Binafsi nashukuru Tanzania kuwa kisiwa cha amani na utulivu kwani licha ya sehemu ya umati mkubwa kama kujitokeza kushuhudia pambano hilo na kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha lakini usalama uliendelea kudumishwa licha ya changamoto kadhaa kujitokeza.
 
Wakati mwingine najiuliza kama rais ambaye wadau walitangaziwa kuwa ndio angekuwa mgeni rasmi hali ingekuwaje, au ndio alitakiwa aje kuona aibu hiyo na dhaifu katika maandalizi ya masumbwi? 
 
Changamoto zilizojitokeza ni vema waandaaji ikiwa wataandaa mapambano mengine wajipanga vema ili kuondoa upungufu huo ambao unaweza kuhatarisha amani ya waliopo ukumbini na viongozi wanaoharikwa pamoja na mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment