Asili ya
mabondia wengi duniani wanatoka katika
familia duni kwa mfano hapa kwetu ni aghalabu kumkuta bondia ametoka
upanga,oysterbay, au masaki ushuwani.nikiwa na maana mabondia wengi wanatoka uswahilini ni watu wa
hali duni wengi wetu hatujakalia madawati ya shule wengine tuliojitahidi
tumefika darasa la tano au sita kama wazazi walikomaa ndio tunamaliza la saba.
Baadhi yetu tukiwa na umri wa kuanzia miaka sita nyumbani huwa tunaanza kupewa
uzowefu wa kuuza visheti,maandazi,vitumbua, karanga nk na vikibaki nyumbani
hauli chakula mpaka viishe, shuleni mwalimu mkali, darasani afundishi mpaka
usome tuisheni ndio unapata kufundishwa kidogo na ukishindwa maswali yake
viboko vya ghazabu ,hapo ndipo tunapoamua kuachana na shule na kutinga mitaani.
michezo yetu ni katika madampo na
vichochoroni na tukifikia umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea tunajua jinsi
ya kutafuta pesa kwa kuuza njiwa,kucheza kamari,malani,kuiba kuku na bata , na
kwa wale walio watukutu zaidi kuuza na kuvuta bangi ni sehemu ya maisha ya
kawaida tu huku mitaani kwetu. mara nyingi mlo kwetu ni mmoja tu kiubishoo au
kuwa wageni ndio tunakula milo miwili. Katika maisha yetu muda mwingi tupo huru
na michezo kuliko kusoma hasa kolokolo,ngoma,mpira na ngumi, mpira tunacheza
mabarabarani ,vichochoroni na madampo wakati ngumi tunajifundisha katika
makamali vichochoroni au uwani kwa kina masta, begi au tairi limefungwa juu
ya mti tizi linaendelea bila vifanyio
vya mazoezi vilivyo rasmi mwendo mdundo tunasonga na tunashinda au kufanya
vizuri katika mashindano yetu
tunayoshiriki na hali yetu duni hihi hii ya kimaisha, na majina yetu kutangazwa
sana katika vyombo vya habari na kupata umaarufu mkubwa nchini,nchi jirani na hata nchi za ulaya.lakini ukibahatika
kututembelea na kuangalia tunapoishi na familia zetu na umaarufu tulionao
maisha yetu mabovu yanasikitisha .
siku za hivi
karibuni kuna vimaendeleo kidogo baadhi ya mabondia tunafanya mazoezi katika
vilabu vya pombe kwa kuwalipa kodi ya mazoezi wenye bar .naweza sema Tanzania hakuna
sehemu rasmi za kufanyia mazoezi ya
ndani zilizotengwa na serikali kwa ajili ya raia wake wapenda michezo na kama
zipo ni chache katika makambi ya jeshi kwa masharti magumu kwa raia wa
kwawaida. Siku za nyuma wakazi wa mjini kama vile kisutu,gerezani na kariakoo
walikuwa wanafanya mazoezi pale anatoglu,siku hizi huwezi kusikia kuna
mwanamichezo katokea gerezani au kariakoo,iliyobaki kwao ni kuuza na kutumia
madawa ya kulevya na kukimbizana na wafanyabiashara wa maeneo hayo, naweza ilaumu
serikali kwa kutoendeleza michezo bali ilishiriki kuuwa kabisa michezo maeneo
hayo na mengineyo zaidi.
Kwa sisi
tulionza kukuwa kimchezo Pambano la ngumi likiandaliwa huwa tunalipwa kuanzia
shilingi alfu 5 mpaka 20 kwa mapambano haya madogomadogo na iwapo kutakuwa na
pambano kubwa na kupata bahati ya kucheza unaweza lipwa shilingi alfu 40 mpaka
laki moja.mapambano makubwa yanaweza kuwa moja,mawili au matatu kwa mwaka
hayazidi hapo, haya mapambano madogo tunaweza pata mawili mpaka sita kwa mwaka.
Msiwaone mabondia wakicheza mkadhani wana kipato kikubwa la hasha, ni wale tu
wachache waliobahatika kupata wadhamini au waratibu wenye uwezo wa kipesa ndio
kidogo hutoka.
Kwa sisi
wengine ukiangalia elimu ya kusoma hatuna kazi hakuna na mchezo wa ngumi
tunaupenda na pengine tuna vipaji na kwa kufanya vizuri katika mapambano
yetu,hivyo mchezo ndio huwa kama ajira zetu kwa sababu tunapata chochote kidogo
kupitia mchezo huo kuliko kuiba au kukimbizana na mapolisi katika kamari na
kuishia jela.
Kwetu sisi
mabondia huona ni jambo la kifahari na hufurahi mno pale tu tunapopata pambano
la nje ya nchi na hufurahia kupanda ndege na vile vimisosimisosi tunavyopata
tukiwa mahotelini ugenini, tukihadisiana mambo ya safari uswahilini kwetu
tunahisi tunakosa mambo mengi ya raha,
Hapo ndipo
mawakala wa ngumi hutupata na mabondia huwa wanadiriki kukubali kwenda kucheza
popote tukijua tutapanda ndege tunakula raha bila kujali na wala kuhoji tuendako tutalipwa kiasi gani
cha pambano nitakalocheza wala kujua usalama wangu.
Ukiangalia
umbumbumbu na maskini tulionao mabondia,hapo wajanja wenye pesa
zao,wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wanatumia udhaifu tulionao mabondia
kutuhadaa kwa kutupatia safari za nje za kimichezo au matembezi ya kwenda
kufanya mazoezi ughaibuni na hatimae
kutubebesha mihadarati(madawa ya kulevya)
bila kujua kwa kutuwekea katika mizigo tunayosafiri nayo. Pindi kuna
baadhi ya wafanya biashara hao wenye pesa zao hutuweka wazi wakati unaenda
pigana umbebee mzigo wake na atakulipa pesa nyingi ,hapo ndipo tunapobanwa
ukiangalia nyumbani tunalalia telemka tukaze tunashindia tembele mlo mmoja msosi wa kengele tena kwa masimango,mfukoni
sina kitu na wala sina kazi itakayonipatia pesa ya kula kwa sasa (hapo
sijaingiza mambo ya kodi),demu wangu namlinda vipi.
Hii njaa na
umaskini tulio nao mabondia,hapo ndio vigogo wanapoamua kututumia kwa kutubebesha madawa ya kulevya kusafirisha nje
wakijua wazi hatuwezi kataa kutokana na dhiki tuliyo nayo, tutakubali tu kwani
hakuna apendae kulala njaa , kulala pachafu
au kuvaa midabwada.
’siwezi acha
dili la pesa kama hili wakati jina langu kubwa kila kona linatajwa mitaani na
vyombo vya habari lakini mimi binafsi nauli ya daladala sina,siku ya tatu leo
nakula mlo mmoja kwa siku,watoto hawapo katika hali nzuri, mazoezi yenyewe
sifanyi kwa raha nafikiria nitapata wapi mshiko,leo unaniletea ishu ya pesa
niikatae si nitakuwa kichaa’wadau wenzangu wa ngumi ,wapambe wao,na walio
karibu na sisi mabondia wana nguo za bei kubwa wanapendeza , wana magari, ukiangalia
mimi bondia ndie mtendaji wao mkuu nipo ovyo sina kitu mfukoni wala tumboni
madeni kibao yaani majanga matupu
Ushauri
wangu kwa serikali au taasisi zinazohusika na wanaolichukia jambo hili kiukweli
maana wengine hujifanya kulichukia mdomoni pembeni ndio watendaji wakuu wa
kuwatumia wanamichezo au wasanii kwa faida zao. Mabondia au wanamichezo
tuboreshewe maeneo yetu ya michezo ikiwemo katika vilabu vyetu na maeneo ya
mazoezi, vifaa viongezwe ikiwezekana kodi ya vifaa vya michezo ipunguzwe ili
viwe vingi nchini mabondia wasibabaike na vya kuazima au kuangalia katika tv
vifaa nya wenzetu. Serikali iwajali mabondia, isaidie kudhamini semina za
walimu wa ngumi ili wawaongoze vema vijana wao.magym ya makusudi yajengwe na
maeneo ya wazi wasigawane wenye pesa na viongozi kwa faida zao wajenge sehemu za michezo ya ndani(indoor), na
kama pia itatumika njia ya kutoa madarasa matupu katika mashule yetu kwa ajili
ya kutuachia sehemu ya mazoezi ya jioni itasaidia sana kukuza mchezo na walimu
wenye taaluma kufundisha vizuri kuliko mabondia kufundishana vichochoroni na
kutokuwa na nidhamu ya mchezo wala maisha
Na
IBRAHIM ABBAS KAMWE
manager and boxing trainer of Bigright boxing
Local Promoter via Bigright Promotion
Mwananyamala
Dar es salaam
+255 767 / 754 / 501991
No comments:
Post a Comment