Tangazo

Pages

Saturday, September 7, 2013

upotoshwaji wa taarifa za masumbwi

Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt,Fenela Mukangala wa pili kushoto akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdala pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na 
Catherini Matili  Picha www.superdboxingcoach.blogspot.com

 taarifa rasmi kwa wote mliohusishwa
hivi karibuni kumetokea baadhi ya waandishi wanaojidai kujuwa kuandika habari zihusuzo ngumi za kulipwa,na hasa baada  ya bondia francis cheka kushinda ubingwa wa shirikisho la ngumi la dunia.
wako waliopotosha watu aidha kwa kujifanya kujuwa tu wakati hawana walijualo,na hawataki kuuliza.

wako ambao wamediriki kuandika kwamba bondia kwamba mkanda aliouchukuwa cheka ni feki ,na wako ambao walikwenda mbali zaidi kwa kuingilia mambo binafsi ya bonia phill wiliam katika maisha yake ya kila siku kwamba ni kinyoozi.

na wako waliosema cheka siyo bingwa wa dunia.

                                                                  majibu yote haya hapa

mimi binafsi nilikuwako uwanja wa ndege wa mwl julius nyerere kumpokea rais wa shirikisho la ngumi dunian [WBF] wakati akiwasili nchini tanzania,na alikuja na mikanda 2 mipya ambayo mmoja ulikuwa ni wa kugombea MADA MAUGO na THOMAS MASHALI ubingwa wa afrika.

pia mkanda mwingine mpya ambao waliugombania PHILL na CHEKA.

Na mikanda yote hiyo ilikuwa vacant [wazi]haikuwa na bingwa. ,mambo hayo yalifanyika saa saba mchana.

Na ilpofika saa 4.30 usiku nilikuwa tena uwanja wa ndege kumpokea bondia PHILL WILIAM naye alikuwa ameutundika begani mkanda wa CHAMA CHA NGUMI DUNIANI [WBU]

Nataka kuwafundisha mjuwe kwamba mkanda aliokuja nao phill haukuhusika na pambano lile la tarehe 30 pale diamond.
na aliondoka nao.

kuna mjinga mmoja aliandika eti andre award ambaye ndiye ameshika namba moja katika viwango vya mabondia wa super middle kuwa ndiye bingwa wa dunia ,ni jaqmbo la kijinga sana mtu kujifanya anajuwa wakati hajuwi lolote kuandika kuhusu mchezo wa ngumi na hasa zaq kulipwa.

ukifikiri eti yule aliye kuwa wa kwanza katika viwango vya mabondai ndiye bingwa utakuwa unapoteza muda wako bure na utajidhalilisha kwa kuonekana mwandishi uchwara.

mchezo wa mpira waq miguu nchi ikiwa nafasi ya kwanza katika viwango ni baada ya kuwa bingwa wa dunia katika ngumi haiko hivyo.
kabla bondia FRANCIS CHEKA hajapigana na PHILL WILLIAM katika viwango vya ubora wa mabondia alikuwa namba 34 na mpinzani wake alikuwa namba 45, na baada ya cheka kuwa bingwa wa dunia amepandisha na kufikia namba 21 ni jambo la kujivunia sana kwa bondia cheka..

zamani walikuwako waanishi mahiri wa mchezo wa ngumi ,wafuatao na waliutendea haki mchezo wa ngumi kwa kuandika ya ukweli na kama yalikosolewa mambo yalikuwa ya ukweli na siyo uzushi kama ilivyo sasa.
tulikuwa na MAHAMUDU ZUBERI ,MAJUTO OMARI,SALEHE ALLY hao walikuwa ni wajuzi katika kuuandika mchezo wa ngumi ,na sijuwi inakuwaje hawa wanaoandika hivi sasa hawaombi misaada yao.? waelekezwe.

ELIMU YA BURE NI HII

UKITAKA KUJUWA KAMA CHEKA NI BINGWA AU SIYO BINGWA INGIA -

WBF.COM  HALAFU CLINK world boxing federation.
utajijuwa na utajihukumu mwenyewe uko katika kundi la wajuzi au mbumbumbu?

FAHAMU HAILINGANI NA UJUZI

No comments:

Post a Comment