Tangazo

Pages

Wednesday, September 4, 2013

CHEKA KUINGIA BUNGENI KESHO BAADA YA KUMTWANGA MMAREKANI


Cheka kuupeleka mkanda wa WBF bungeni

Bingwa wa mkanda wa WBF, Mtanzania Francis Cheka anatarajia kuupeleka mkanda wake huo alioupata mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kumtwanga kwa pointi bondia wa Marekani, Phill Williams kwenye ukumbi wa Diamond Jubillee.

Cheka ambaye alifanikiwa kutwaa mkanda huyo baada ya kumshinda bondia huyo kwa pointi katika mpambano wa raundi 12 anatarajia kuingia bungeni kesho akiongozwa na Rais wa TPBO, Yasin Aballah 'Ostadh' na Promota Mohamed Bawazil na kocha wa mchezo huo, Rajab Mhamila ‘Super D’.

Msafara huo unatarajia kuyingia Dodoma leo jioni tayari kwa kuingia bungeni kesho alhamisi asubuhi na kuwaonyesha wabunge mkanda huo ambao umeitangaza Tanzania kimataifa katika medani ya masumbwi duniani.

Imekuwa kawaida kwa wanamichezo wanapopata mataji mbalimbali kutembelea bungeni kwa lengo la kuonyesha mataji yao kwa wabunge wa bunge hilo la Tanzania.

Na hii ni kwa mara ya kwanza kabisa wadau wa mchezo wa masumbwi kukaribishwa bungeni mana tmekua tukiona timu za mpira wa miguu ikiwemo Simba na yanga kwenda na mataji yao bungeni na kuungwa mkono kwa wabunge walio wengi
www.superdboxingcoach.blogspot.com

No comments:

Post a Comment