MEXICO CITY, Mexico
"NLIKUWA nikimuangalia mama
yangu akifua na kupiga pasi nguo za watu
na nilimuahidi siku moja nitampa nyumba na kamwe hatafanya kazi hiyo
tena".Kauli hii siyo yangu mimi, bali ni ya bondia, Julio Cesar Chavez, wakati akisikitishwa na hali ya umaskini iliyokuwa nayo familia yao hadi akaamua kujikita kwenye mchezo wa masumbwi ili kuiokoa familia hiyo.
Kwa mujibu wa historia ya bondia huyo, alizaliwa Julai 12, 1962 katika kitongoji cha Ciudad Obregon Sonora nchini Mexico na baba yake, Rodolfo Chavez, alikuwa mfanyakazi wa reli.
Katika makuzi
yake alikuwa akishinda kwenye treni akiwa na dada zake watano na kaka zake
wanne.
Chávez anatajwa kuzaliwa kwenye familia maskini lakini ngumi zikamtoa na kumpa heshima kubwa.
Bondia huyo alianza ngumi za ridhaa akiwa na umri wa miaka 16 na baadaye akahamia mjini Culiacan ili kuendeleza kibarua chake.
Inaelezwa kuwa kama kuna mabondia ambao rekodi zao zinajieleza,
miongoni mwao ni Chavez.
Rekodi hiyo ni kutokana na kwamba Chavez aliwahi kusimama ulingoni kwa miaka 10
bila kupigwa na bondia yeyote.
Katika rekodi hiyo, bondia huyo
alipigana mapambano 116, ambapo kati ya hayo alishinda 108 na kati ya hayo 87
alishindwa kwa KO akapigwa 6 na kutoka sare mawili.
Kutokana na umahiri wake, bondia
huyo anafahamika kuwa kati ya mabondia ambao walipigana mapambano makubwa yaliyomfanya kupewa heshima ya bondia bora
nchini Mexico.
Kwa mujibu wa historia ya bondia huyo ambaye alijikita
kwenye ngumi za kulipwa mwaka 1980 kabla ya kutundika gloves mwaka 2005, amewahi
kutwaa ubingwa mara sita katika uzani tatu tofauti.
Mbali na sifa hizo, mbabe huyo wa
masumbwi vilevile kwenye rekodi yake ana rekodi ya kupigana mapambano 88-0 kabla ya kupoteza moja dhidi ya Frankie Randall, lakini baadaye akalipiza
kisasi mara mbili.
Inaelezwa kuwa kabla ya pambano hilo alikuwa ameshatoka
sare dhidi ya Pernell Whitaker, pambano ambalo alionekana ilikuwa ashindwe.
Mabondia wengine ambao waliwahi
kuonja kichapo kutoka kwa Chavez ni Roger Mayweather, Hector Camacho, Sammy
Fuentes.
Hata hivyo pamoja na kustaafu mchezo
huo, jina Chavez bado linatamba kwenye
ulingo wa mchezo huo kupitia kwa mwanaye, Julio Chavez, Jr.
Katika pambano hilo ikiwa mwishoni mwa raundi ya kwanza, Chavez aliachia konde lililomuangusha Ruiz.
Baada ya pambano hilo bondia huyo aliendelea kushika kasi kwa kuwachapa mabondia kadhaa kabla ya Septemba 13,1984, kutwaa ubingwa wa Feather kwa kumchapa Mmexico mwenzake, Mario Azabache Martinez, katika pambano lililofanyika kwenye ukumbi wa Grand Olympic Auditorium, uliopo mjini Los Angeles, California.
No comments:
Post a Comment