Tangazo

Pages

Wednesday, September 18, 2013

CHAMPIONI LATOA MSAADA, MATUMLA AANZISHE SHULE YA MCHEZO WA NGUMI





Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph akimkabidhi glovu mbili, bondia mkongwe nchini Rashid Matumla. Vifaa hivyo vimetolewa na gazeti la Championi ukiwa ni msaada kwa Matumla kwa ajili ya kusaidia ndoto yake ya kuanzisha shule ya ngumi.

Wengine katika picha hiyo ni Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (wa pili kulia) aliyeratibu zoezi hilo.  Wanaoshuhudia ni waandishi wa gazeti hilo, Wilbert Molandi na Martha Mboma.
 
AKIWA NA SALEHJEMBE
Matumla amekuwa na ndoto ya kuanzisha shule ya ngumi lakini hana mtaji, hata Championi halijatoa vifaa vya kutosha, lakini uongozi wa gazeti hili umekuwa ukisisitiza wadau wajitokeze zaidi kumsaidia Matumla kutimiza ndoto yake.
 
AKIWA NA JOHN JOSEPH
Bingwa huyo wa zamani wa dunia mara mbili, amekuwa akiandamwa na ugonjwa wa ganzi na maumivu makali kwenye uti wa mgongo na daktari amemshauri kutoendelea kupigana ili kuokoa maisha yake.
Matumla amesema anaweza kuendeleza maisha yake kwa kufungua shule ambayo anaamini itazalisha wachezaji wengi nyota wa mchezo wa ngumi.
Championi limeamua kumsaidia katika hilo na kuendelea kuhimiza wadau kujitokeza zaidi kumsaidia ili atimize ndoto hiyo kwa kupata vifaa na kulipa pango angalau la mwaka, angalau aanzishe Matumla Boxing School.
PICHA NA KHATIM NAHEKA

No comments:

Post a Comment