Tangazo

Pages

Thursday, April 19, 2012

YAZIDU AMTAKA MTAMBO WA GONGO


YAZIDU AMTAKA MTAMBO WA GONGO



BONDIA Said Yazidu wa Dar es Salaam, amemuomba promota Kaike Saraju, amuandalie pambano na mbabe wa Rashidi Matumla ‘Snake Man’ Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’, ili aweze kumstaafisha ngumi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Yazidu ambaye anapigana uzani wa kati, alisema kuwa, anasikitika kuona waandaaji wa mapambano wakivunja kanuni, kwa kuwakutanisha wakongwe hao, wakati wapo mabondia wanaoweza kucheza nao.
Alisema kuwa mara nyingi amekuwa akitamani kucheza na wakongwe hao, lakini anakosekana promota wa kumuandalia pambano nao, hivyo ndiyo maana akamuomba Siraju ambaye kwa sasa amejitahidi sana kuandaa mapambano.
“Ninawaomba mapromota, hasa Kaike Siraju, aniandalie pambano na Mtambo wa Gongo, niweze kumstaafisha ngumi, aache kumpambanisha na Rashidi kila kukicha,” alisema Yazidu.
Bondia huyo, ambaye ni mmoja wa mabondia wakongwe nchini, alisema kwamba hivi sasa anajifua chini ya Meneja, Ahmed Seif Ally, katika gym iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment