Sunday, April 15, 2012
TIMU YA TAIFA YA MASUMBWI YAENDELEA NA MAJARIBIO
13/04/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Katika kuhakikisha kuwa timu ya taifa ya ngumi inapata maandalizi mazuri kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya kufuzu kuelekea Olimpiki .leo kuanzia saa 4.00 asubuhi kumefanyika mashindano timu ya taifa na timu ya ngumi ya jkt.matokeo ni kama ifuatavyo;-
1-49kg l/fly said hofu wa jkt amemshinda john christian taifa kwa majaji 3,0
2.52kg fly abdalah kassim taifa amemshinda amdani issa wa jkt kwa majaji 2,0
3. 56kg bantam emilian patrick taifa amemshinda revocatus chomari wa jkt kwa majaji 2,0
4. 60kg l/weight elias damson jkt amemshinda Denis maritn wa taifa kwa majaji 2,0
5.64kg l/welter victor njaiti wa taifa amemshinda kassimu hussein wa jkt kwa dakitari
kusimamisha pambano baada ya kassim kuchanika juu ya jicho
6. 69kg welter selemani kidunda wa taifa alimshinda gurudani saidi wa jkt kwa k.o round
ya kwanza
7. 91kg heavy weight kati ya ditram kaimbe wa jkt na haruna swanga wa timu ya taifa pambano ambalo lililokuwa na mvuto na msisimko mtangazaji alishindwa kutangaza matokeo baada ya kuzongwa na mashabiki wa pande zote kutaka mchezaji wao atangazwe mshindi.hadi tunaondoka haikujulikana nani mshindi.
timu ya taifa bado itakuwa na jaribio moja na kombaini ya vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya kwenda morocco.
kwa sasa timu ya taifa ipo kambini mkuza kibaha katika shule ya filbert bayi chini ya makocha watatu na daktari mmoja
timu hiyo ina tarajiwa kuondoka tarehe 26/04/2012 kuelekea morocco kushiriki mashindano ya kufuzu kushiriki olimpiki julai london uingereza
hadi kufikia leo tumepata jumla ya tiketi sita kutoka kamati ya olimpiki tanzania toc.
ambazo ni kwa ajili ya wachezaji 4na makocha2. hata hivyo bft bado inaomba wafadhiri kwa ajili ya kuongeza idadi ya wachezaji na viongozi wa bft kwa ajili ya kuhudhuria kikao muhimu cha shirikisho la ngumi la afrika.
taarifa hii imeletwa na makore mashaga katibu BFT,mara tu baada ya kumalizika kwa mashindano hayo. 0713588818
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment