Nikiwa kama mdau mwingine wa michezo,nieamua kujaribu kuhamasisha na kuinua vipaji kwa watoto wadogo ili kesho tuwe na mabingwa wa ukweli.
ukiwa kama mchezaji wa judo wa zamani jaribu kutumia ujuzi wako kuwapa wengine kwa manufaa ya taifa letu la kesho.
mimi nipo katika ngumi kwa kipindi tokea 1987 pale anatoglo baadae nikaamia simba,nikapata bahati ya kwenda uingereza ambako huko nilikaa tokea 1995 mpaka 2003 nikabahatika kucheza kule na nilikuwa karibu sana mabondia,mameneja na mapromota wakubwa.
kwa sasa nipo kama mtaalam wa ngumi,jaji,supervisor na katika kuufanya mchezo usilale zaidi kwa uwezo wangu mdogo najitahidi kuandaa mapambano mbalimbali,kuwafundisha vijana wadogo nao wapate
nilichonacho.
*****
BigRight awakomalia vijana wadogo
Ibrahim kamwe`bigright` ambae ni local promoter wa ngumi ameamua kwa dhati kabisa kuwafundisha vijana wadogo mchezo huo.
Ibrahim anasema “Mabondia wengi hapa
nchini wanapigana ili mradi wanapigana hawana formula zozote,hawajui kujilinda pale wanapoelemewa,hushambulia kwa kubahatisha tu, pia hawajui sheria za mchezo wenyewe yote kutokana na kukurupukia mchezo ukubwani.
Bondia akicheza sparing kidogo anatafuta fight,na akipata fight moja au mbili basi huwezi kumkosoa kila kitu anajua yeye wakati ana mapungufu mengi na hajafikia kuitwa professional boxer.hivyo nimeamua kuwafundisha vijana wadogo ambao wanafundishika .
kwani SAMAKI MKUNJE YUNGALI MMBICHI. Sio baadae tunailalamikia serikali.sisi tujitahidi then tuiamshe serikali itusaidie,sababu inatulazimu kujua kama serikali yetu imelala katika michezo mingine ambayo pia ndio inayoleta ushindi na sifa ulimwenguni.wenyewe wamelalia soka
ambayo hawaiwezi ni kupeana matumaini tu
No comments:
Post a Comment