Tangazo

Pages

Thursday, June 19, 2014

Dula mbabe kuzipiga vunja jungu


Bondia  machachali wa ngumi za kulipwa nchini Abdallah Paziwapazi  kiroba au kama anavyojulikana na wengi” Dula mbabe’ anategemea kupanda uling
oni tarehe 29/6/2014 katika ukumbi wa ccm mwinjuma-mwananyamala kuzipiga na Hamis Juma ambae amekuwa mbadala wa maneno osward. Mpambano huo ambao utakuwa wa vunja jungu yaani  wa kuikaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani ,kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi yakiwemo mawili ya kumaliza uhasama wa wababe wa kitaa,yaani mbabe wa mwananyamala kwa mama zakaria  Mwinyi mzengera”mambwa”  na mbabe wa mwananyamala kwa kopa George manywele “G-mawe”.nae mbabe wa mwananyamala kisiwani joseph piter “mbowe” atazipiga na zumba kukwe, pia kutakuwa na pambano kali la vijana wanaocheza ngumi zenye uwezo wa hali ya juu Issa Omar Nampepeche”peche boy” atakae zipiga na Ramadhani kumbele katika pambano la raundi nane,hili pambano linategemewa kuwa zuri kutokana na mabondia wote kuwa na spidi kubwa wawapo ulingoni. Ukiachilia na  mapambano haya yenye vibweka pia kutakuwepo na mapambano mengine ya utangulizi kama vile Yule mwimbaji maarufu wa mapacha watatu khareed chokolaa atakapozipiga na daud giligili, chidi  mbishi  atamvaa Ramadhan hamis, dj kulwa atazipiga na alex kado na e masango komakoma ataminyana na Mohamed amir”alkaida”
Mapambano haya yameandaliwa na bigright promotion,chini ya kiongozi wake wake Ibrahim kamwe ambae siku zote amejitahidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha michezo ina kuwa ajira kwa vijana na inachezwa mara kwa mara kuweka ufanisi zaidi. Akizungumza na vyombo vya habari bw Ibrahim kamwe alisema maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekamilika na mabondia wapo katika hali nzuri ya ushindani na kuwasihi watu wajitokeze waje kuangalia ngumi za kali zenye ushindani ukizingatia kuwa ukumbi umekarabatiwa na kila mtu atakaa katika kiti chake na ulinzi mkali utakuwepo ili kuboresha mchezo wa ngumi usiwe sehemu ya mchezo wa fujo na kila atakaekuja kwa nia ya kufanya fujo atachukuliwa hatua kali za kisheria mojakwamoja bila kusita

No comments:

Post a Comment