LILE pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya bondia, Alibaba Ramadhan na bingwa, Japhet Kaseba, sasa litakuwa na sura mpya ya mapigano, baada ya muandaaji wa pambano hilo, Ibrahim Kamwe, kuongeza mapambano la mchezo wa Kick Boxing (ngumi na mateke) ili kuleta radha zaidi.
Hatua
hiyo imekuja baada ya bondia mtanzania anayeishi nchini Canada Kareem
Kutch, ambaye anauraia wa nchini humo, aliyejigamba kuwa Tanzania hakuna wachezaji wa kiwango cha kimataifa wa mchezo huo na kutangaza kuwa hakuna mtu wa kucheza naye hapa nchini, jambo
ambalo lilipingwa na mabondia wa mchezo huo, waliomtaka muandaaji wa
pambano hilo, Bigright Promotion, afanye juhudi za kumleta nchini bondia
huyo ili kujione vipaji.
Bigright, iliamua kumtafuta bondia `Tata Boy` ambaye amekubali kucheza na Mkanada huyo katika pambano la uzito wa Kg 75 za mchezo wa kimataifa.
Pambano hilo litakalopigwa siku
ya jumapili ya Desemba 22, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner
hotel, siku ambayo kutakuwepo na mapambano mengi yakiwemo ya Ernerst
Bujiku, atakayezipiga na Sha Kasim, Lusekelo Daud, dhidi ya Mbaruku
Heri, Issa Omar, atapigana na Haji Juma, Moro Best na Issa Peche na
mapambano mengineyo mengi.
kwa ujumla ni mapambano ya kukaribisha sikukuu ya Krismas na
mwaka mpya kwa staili ya aina yake na kuuaga mwaka kwa usalama na
amani, ambayo yanasimamiwa na PST chini ya kiongozi wake Emanuel
mlundwa.
No comments:
Post a Comment