Tangazo

Pages

Thursday, December 5, 2013

MASUMBWI KUFANYIKA MOROGORO DESEMBA 27

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
BONANZA la mchezo wa ngumi za ridhaa na kulipwa linatarajiwa kufanyika Desemba 27, mwaka huu, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, mjini hapa.
 
Akizungumza na mtandao huu, msemaji wa bonanza hilo, Andrew Mtabazi alisema lengo la kuandaliwa kwa bonanza hilo ni kuibua na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi wa mkoani Morogoro na maeneo ya jirani.
 
Mtabazi alisema siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya masumbwi yatakayoanza kupigwa majira ya saa 10 jioni.
 
Alisema mabondia kutoka klabu mbalimbali za mkoani Morogoro watapanda ulingoni kudhihirisha uwezo wao katika mchezo huo.
 
“Huu ni mpango mkakati wa kuendeleza mchezo huu mkoani hapa hivyo tunaomba wadau watuunge mkono”, alisema.
 
Aidha, Mtabazi ametoa wito kwa wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi na kudhamini bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika kila mwisho wa mwezi.
 
“Gharama za maandalizi ni kubwa mno hivyo tunaomba wadau pia watusaidie katika hili ili tuweze kutimiza malengo yetu”, alisema.

No comments:

Post a Comment