![]() |
Floyd Mayweather Jr. (44-0, 26 KO’s) VS Saul “Canelo” Alvarez (42-0-1, 30 KO’s) step foot inside the ring on September 14th at the MGM Grand in Las Vegas, Nevada |
Thursday, May 30, 2013
Wednesday, May 29, 2013
KASEBA APANIA KUMKALISHA MMALAWI

BONDIA wa ngumi za
mateke ‘Kick Boxer’ Japhet Kaseba amesema amejipanga kuweka rekodi nzuri katika
tasnia hiyo kwa kumchapa Mmalawi, Rasco Chimwanza katika pambano lao la kuwania
ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati linalotarajiwa kuchezwa Juni 8, mwaka huu.
Akizngumza na Habari Mseto jijini Dar
es Salaam, Kaseba alisema anajua kama bondia huyo ni nyota katika tasnia
hiyo, lakini kutokana na maandalizi aliyoyapata atahakikisha anaweka heshima
katika ngumi za mateke.
“Namshukuru mungu nina afya nzuri hadi
sasa na naendelea na mazoezi kwajili ya pambano hilo naomba Watanzania
wajitokeze kwa wingi katika ukumbi huo wa DDC Magomeni,” alisema Kaseba.
Naye Katibu Mkuu wa Oganizasheni ya
ngumi ya za kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe alisema maandalizi ya
pambano hilo yamekamilika, na tayari wamemtumia nauli Mmalawi huyo na kwamba
anategemea kuingia nchini Juni 5.
Nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa
ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na
mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana
DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika
masumbwi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika
makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la
Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani
kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha
kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza
zaidi mchezo huo
Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila
,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya
Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe.
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super
D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
Monday, May 27, 2013
KING CLASS MAWE KUPAMBANA NA BAUNSA JUNI 16 PANANDI PANANDI ILALA
KING CLASS MAWE |
Patrick Kavako'Baunsa' |
Mpambano huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa na wengi nchini
mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu
Mhamila ‘Super
D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake
kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas
Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa
ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na
mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana
DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika
masumbwi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika
makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la
Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani
kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha
kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza
zaidi mchezo huo
Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila
,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya
Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe.
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super
D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
HAMADUU MWALIMU ALIVYO MWONESHA UBABE COSMAS KIBUGA
Bondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Cosmas Kibuga akimsubili kwa hamu hamaduu mwalim baada ya kudondoka chini wakati wa mchezo wao jana |
Bondia Hamaduu Mwalimu kushoto akioneshana umairi wa kurushiana makonde na Cosmas Kibuga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Mwalimu alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Mpambano wa utangulizi kwa ajili ya kusafisha uwanja |
DEO NJIKU ALIPOMSAMBALATISHA OMAR RAMADHANI MOROGORO
Bondia Deo Njiku kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Omari Ramadhani wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa Njiku alishinda kwa TKO ya raundi ya pili na kuwa bingwa mpya wa Taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akiwepo kushudia mpambano huo uliofanyika Morogoro |
Mabondia wa Utangulizi wakisafisha jukwaa kabla ya mtanange wenyewe |
Chembu Upcat Kidevu lazima ukae ndivyo inavyo someka picha hii |
Omari Ramadhani kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Taifa Njiku alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Tuesday, May 21, 2013
Sunday, May 19, 2013
TASWA FC YAWAFUNGA TIMU YA MPIRA YA MABONDIA KWA TABU 2.1
Bonia Daudi Muhuzi akishindana na Mbuyu wa timu ya TASWA FC Majuto Omari wakati wa mpambano wao |
Kocha wa kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D' akisisitiza jambo wakati wa mapumziko |
Mchezaji wa timu ya Taswa akipambana na bondia kuwania mpira |
SUPER D BOXING COACH AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA MAPUMZIKO WA MCHEZO HUO |
JONAS SEGU ALETA HESHIMA YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA BAADA YA KUMWENYESHA MTHAILAND, LAKINI AUMIA MKONO RAUNDI YA 6
Tanzania imetengeneza historia
mpya kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa
wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. Safari
hiiJEMBE, kijana mtanashati
anayeinukia kwenye masumbwi Jonas
Segu kutoka katika ukumbi wa mazoezi waRespect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha
kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi
wa Thailand pamoja na
nchi za ukanda wa Indo-China.
Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia
Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka
Thailand katika uzito wa Light
Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF. Mpambano wao
ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa na television
katika nchi zote za ukanda wa Indo-Chinaza Laos,
Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.
Mpambano wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia
wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito
ya kumshikisha adabu. Segu alitupa
makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana
na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya kwanza
ilimbidi Pathompothong ajilinde
na kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili kudhoofisha masumbwi yaSegu aliyekuwa anayachanganya
kama mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!
Jonas Segu alikuwa chini ya
uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George “Lister” Sabuni ambaye
aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye mpambano huo wa mwaka.
Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa
Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao
ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu
alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde
mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri
kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya
kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda
Thailand kuuchukua mkanda wa IBF
Pan Pacific na sio kufuata ulaji!
Raudi ta 5 Pathompothong aliingia
ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na kutembea
ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kenye kamba ili amkandamizie
masumbwi yake. Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia
na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia
ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa
yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya
mazoezi ya kutosha. Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye
ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania,
Tanzania, Tanzania!
Katika
raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana
masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani
mwenza. Ni katika kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono
na Mthailand Pathompothong. Inawezekana kuwa ni katika juhudi
za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia
mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani
mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati
wa kitanzania.
Katikati ya raundi ya saba Segu aliona
kuwa hawezi kuutumia mkono wake vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa
anaacha!
Wednesday, May 15, 2013
MSANII DIPO AJIUNGA KWENYE MASUMBWI
Kocha wa mchezo wa masumbwi Klabu ya Amana CCM ,Kondo Nassoro Kulia akimwelekeza msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'dipo' Dar es salaam jana jinsi ya kutupa makonde alipokwenda kufanya mazoezi ya ngumi kwa ajili ya kujiweka sawa sawa katika kuakikisha anafanya vizuri kwenye fani yake.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'dipo' akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Omari Bai wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika GYM ya Amana CCM Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Kocha wa mchezo wa masumbwi Klabu ya Amana CCM ,Kondo Nassoro Kushoto akimwelekeza msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'dipo' Dar es salaam jana jinsi ya kutupa makonde alipokwenda kufanya mazoezi ya ngumi kwa ajili ya kujiweka sawa sawa katika kuakikisha anafanya vizuri kwenye fani yake.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Monday, May 13, 2013
Friday, May 10, 2013
SUPER D AFYATUA DVD TATU MPYA ZA MAFUNZO YA MASUMBWI
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super
D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo
Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. DVD MPYA ZA MASUMBWI HIZI HAPA
![]() |
DVID MPYA ZA MASUMBWI KWA SASA ZIPO TAYARI KWA AJIRI KUPATA BURUDANI UKIWA NYUMBANI ZAID TUWASILIANE 0713406938 AU TEMBELEA www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Tuesday, May 7, 2013
BONDIA SAID MBELWA AMGALAGAZA SAID MKONDE KWA K,O
Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pil picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Chilambo Hemed kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Boniface Urasa wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki Chanika Chilambo alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Said Mbelwa akipambana |
Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Refarii Saidi Chaku akimwinua mkono juu Bondia saidi Mbelwa kuashilia ni mshindi katika mpambano huo |
Monday, May 6, 2013
MAYWEATHER Jr AMCHAPA ROBERT GUERRERO KWA POINTI

Bondia Floyd Mayweather Jr (kushoto)
akimsulubu Robert Guerrero katika pambano la masumbwi kwenye Ukumbi wa
MGM Grand Garden, jijini Las Vegas, Marekani. Mayweather Jr alishinda
kwa pointi pambano hilo la kwanza tangu amalize kifungo cha miezi miwili
jela.
Mayweather Jr akiendelea kumuadabisha
Guerrero, kiasi cha majaji wote watatu kumpa ushindi sawasawa wa pointi
117-111 na kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBC uzani wa ‘welter.’
Guerrero akiwa na jeraha juu ya jicho la kushoto lililotokana na makonde mazito ya Mayweather Jr.
Guerrero akipewa maelekezo na kocha
wake, wakati wa mapumziko ya moja ya raundi za pambano hilo, ambalo
alipigwa kwa pointi na kukiri mpinzani wake ni mjanja na ana kasi kubwa
ulingoni.
Mayweather Jr (kushoto), akikwepa fataki la kushoto kutoka kwa Guerrero katika pambano hilo.
Guerrero akiendelea kushambulia 'upepo'
kutokana na Mayweather Jr kuwa mbunifu katika kukwepa makonde yake kama
anavyoonekana pichani.
Mayweather akaweka mzaha kando na
kuanza kujibu mapigo, ambapo makombora yake yalikuwa yakitua sawasawa
mwilini mwa Guerrero, ingawa hayakuweza kumdondosha na kuishia kumuumiza
tu na kutokwa damu.
Guerrero akipokea konde zito la Mayweather. Baada ya pambano, Guerrero alikiri kushindwa na kumsifia mpinzani wake: "Nilimpiga
baadhi ya makonde mazuri. Lakini yeye ni bondia mkubwa na bora. Ni mjanja na mwepesi
mno ulingoni"
Mayweather Jr akiwa amebebwa baada ya
kutangazwa mshindi kwa pointi 177-111 kutoka kwa majaji watatu wa
mtanange huo ndani ya Ukumbi wa MGM Grand Garden, Las Vegas, Marekani.
Mayweather Jr (kulia mwenye kapero)
akishangilia ushindi wake na baba yake Mayweather Sr (kushoto), huku
wapambe wake wakinyanyua juu mikanda anayoishikilia baada ya ushindi
wake dhidi ya Guerrero.
Mayweather baada ya pambano hilo alisema: "Najisikia vibaya kwa sababu sikuweza kushinda kwa ‘knockout’
ambayo mashabiki wangu walikuwa wakitaka. Nilipigana kadri niwezavyo
kuhakikisha nashinda kwa ‘knockout,’ lakini hilo halikutokea ulingoni"
Subscribe to:
Posts (Atom)