Tangazo

Pages

Monday, May 6, 2013

MAYWEATHER Jr AMCHAPA ROBERT GUERRERO KWA POINTI

 Bondia Floyd Mayweather Jr (kushoto) akimsulubu Robert Guerrero katika pambano la masumbwi kwenye Ukumbi wa MGM Grand Garden, jijini Las Vegas, Marekani. Mayweather Jr alishinda kwa pointi pambano hilo la kwanza tangu amalize kifungo cha miezi miwili jela.
 Mayweather Jr akiendelea kumuadabisha Guerrero, kiasi cha majaji wote watatu kumpa ushindi sawasawa wa pointi 117-111 na kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBC uzani wa ‘welter.’ 
 Guerrero akiwa na jeraha juu ya jicho la kushoto lililotokana na makonde mazito ya Mayweather Jr.
 Guerrero akipewa maelekezo na kocha wake, wakati wa mapumziko ya moja ya raundi za pambano hilo, ambalo alipigwa kwa pointi na kukiri mpinzani wake ni mjanja na ana kasi kubwa ulingoni.
 Mayweather Jr (kushoto), akikwepa fataki la kushoto kutoka kwa Guerrero katika pambano hilo.
 Guerrero akiendelea kushambulia 'upepo' kutokana na Mayweather Jr kuwa mbunifu katika kukwepa makonde yake kama anavyoonekana pichani.
 Mayweather akaweka mzaha kando na kuanza kujibu mapigo, ambapo makombora yake yalikuwa yakitua sawasawa mwilini mwa Guerrero, ingawa hayakuweza kumdondosha na kuishia kumuumiza tu na kutokwa damu.
 Guerrero akipokea konde zito la Mayweather. Baada ya pambano, Guerrero alikiri kushindwa na kumsifia mpinzani wake: "Nilimpiga baadhi ya makonde mazuri. Lakini yeye ni bondia mkubwa na bora. Ni mjanja na mwepesi mno ulingoni"
 Mayweather Jr akiwa amebebwa baada ya kutangazwa mshindi kwa pointi 177-111 kutoka kwa majaji watatu wa mtanange huo ndani ya Ukumbi wa MGM Grand Garden, Las Vegas, Marekani.
 Mayweather Jr (kulia mwenye kapero) akishangilia ushindi wake na baba yake Mayweather Sr (kushoto), huku wapambe wake wakinyanyua juu mikanda anayoishikilia baada ya ushindi wake dhidi ya Guerrero.


Mayweather baada ya pambano hilo alisema: "Najisikia vibaya kwa sababu sikuweza kushinda kwa ‘knockout’ ambayo mashabiki wangu walikuwa wakitaka. Nilipigana kadri niwezavyo kuhakikisha nashinda kwa ‘knockout,’ lakini hilo halikutokea ulingoni"

No comments:

Post a Comment