Tangazo

Pages

Sunday, January 4, 2015

BONDIA OMARI KIMWERI KUWASILI NCHINI FEBRUARI KUHAMASISHA NGUMIBONDIA wa kimataifa Mtanzania Omari Kimweri anayeishi nchini Australia


BONDIA wa kimataifa Mtanzania Omari Kimweri anayefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi  nchini Australia anatarajiwa kuwasili nchini Februari mwaka huu.

 Super D ambaye ni mratibu wa safari ya bondia huyo alisema, Kimweri atakuja nchini na ujumbe wa watu nane ambao watakuwa na kazi hiyo kwa muda wa wiki mbili.
Akizungumza jana , kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi, Tanzania Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa lengo ya bondia huyo kuja nchini ni kuhamasisha masumbwi.

Pindi atakapokuja atashikua uwanja wa Kia na baadaye atakwenda mkoani Tanga  ambapo ni nyumbani kwao alipo zaliwa kwa ajili ya mapumziko na baada ya hapo atakwenda Dar es Salaam.

Alisema kuwa pindi atakapokuwa Dar es Salaam atakuwa mgeni rasmi katika pambano litakalokuwa
siku ya wapendanao 'Valentine Da y' 
Kocha huyo wa kimataifa alitoa mwito kwa wadau wa mchezo huo kutoa ushirikiano pindi ujumbe huo utakawasili nchini.
bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine march 13 mpambano utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia

No comments:

Post a Comment