Bondia huyo amebainisha hadi jana
mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya
pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya
mara mbili.
Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari
alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la
uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
“Hadi sasa sijui kama pambano litakuwepo hiyo
Jumamosi au la kwani nimekuwa nikijifua, lakini sijaambiwa chochote
kuhusu kuwepo kwa pambano hilo,” alisema Miyeyusho.
Alisema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano hilo kumemuingiza katika gharama kubwa za maandalizi yake.
Hadi jana mchana Shirikisho la Ngumi za Kulipwa
Tanzania (TPBF) halikuwa limetoa kibari cha pambano hilo ambapo rais wa
TPBF, Chatta Michael alisema wanasubiri agizo la Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) ili kutoa kibari cha pambano hilo.
Kwa mujibu wa promota wa pambano hilo, Jay Msangi
huenda pambano hilo likasogezwa tena mbele endapo hakutapatikana kwa
mwafaka kati yake na BMT ambayo ilimpa sharti la kulipa madeni yote
ambayo anadaiwa licha ya kueleza tayari ametimiza masharti hayo na BMT
bado inaendelea na msimamo wa kumfungia.
No comments:
Post a Comment