Wednesday, October 30, 2013
Tuesday, October 29, 2013
OMARI KIMWERI KUGOMBANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC KWA MARA YA KWANZA MTANZANIA
![]() |
omari Kimweri |
Mpambano huo utakaopigwa nchi ya China November 30 na bingwa wa dunia wa uzito huo nchini china
xiong zhao zhong ni bingwa wa dunia WBC minimum weight ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipo zaliwa
![]() |
Omari Kimweri and Randy petalcoria |
na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC
Ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa Kimweri mwenye rekodi ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3 na mpinzani wake
Xiong
Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo moja
Mabondia hawo wote vijana wenye umri mdogo wa miaka 31 wate wawili wakitofautiana mwezi mmoja tu katika kuzalia mpambano huo umekuwa gumzo katika nchi tatu kwa sasa kwani kila mmoja anajiandaa kivyake
Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makari uku akipewa sparng na bondia Randy petalcoria wa Philippines ambaye ni bingwa wa light fly weight
Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri
Monday, October 28, 2013
AMOSI MWAMAKULA AMGALAGAZA SAFARI MBEYU
Bondia Amos Mwamakula akinyooshwa mkono juu baada ya kumchapa Safari Mbeyu kwa pointi wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Amosi Mwamakula kulia akimshambulia Safari Mbeyu wakati wa mpambano wao mwamakula alibuka na ushindi wa point wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALIJIKUTA AMEMECHISHA KOFIA NA MWAMAKULA YENYE NEMBO YA TMT AMBAYO ANATUMIA BONDIA FLOYD MAYWETHER WA MAREKANI |
AMOSI MWAMAKULA |
BONDIA AMOSI MWAMAKULA AKIJITAARISHA |
Bondia Amosi Mwamakula kulia akimshambulia Safari Mbeyu wakati wa mpambano wao mwamakula alibuka na ushindi wa point wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
AMOSI MWAMAKULA |
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
Sunday, October 27, 2013
VITALI KLITSCHKO AMFUATA PACQUIAO, YEYE ATAKA URAIS
BINGWA wa uzito wa juu wa WBC raia wa Ukraine,
Vitali Klitschko anataka kufuata nyayo za bondia mwenzake, Manny Pacquiao wa
Ufilipino kwa kujiingiza kwenye siasa lakini yeye anautaka Urais wa nchi hiyo
kwenye uchaguzi wa 2015.
Manny Pacquiao pamoja na kuwa mbunge lakini pia
anajishughulisha siasa na ni mbunge wa Bunge la Ufilipino, hali ambayo
imemvutia Klitschko ambaye mwezi Agosti alisema lengo kubwa ni kuifanya Ukraine
kuwa Ulaya, nchi ya kisasa yenye maisha ya kiulaya.
Anasema ataamua na watu wenye mtazamo mmoja, ndoto zinazofanana na kuingia kwenye siasa na kutokea ndani kufanya mabadiliko.
Bondia huyo mwenye elimu ya udaktari kwa kusomea ambapo ana masta yake ambayo alichukua baada ya kupata elimu ya juu kwa aliji ya kutibia binadamu
Saturday, October 26, 2013
KING CLASS MAWE ALIVYO AMTWANGA HASSANI BANDANI KWA POINT
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Bandani wakati wa mpambano wao usio na ubingwa uliofanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es salaam King Class Mawe alishina kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bonia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akimshambulia kwa makonde Hassani Bandani wakati wa mchezo wao usio na ubingwa uliofanyika katika ukumbi wa panandi panandi King Class Mawe alibuka na ushindi wa point mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Ibrahimu Class akioneshwa mshindi baada ya mpambano kumalizika mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
KING CLASS MAWE AKIWA NA MMOJA YA MASHABIKI WAKE BAADA YA KUSHUKA ULINGONI |
KING CLASS MAWE KWENYE POZI |
Bondia Chalo Issa kulia akipambana na Amour Mzungu wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa panandi panandi ilala bungoni Mzungu alishinda kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Shabani Kaoneka kulia akioneshana umairi wa kutupiana makonde na Halid Makwega wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa panandi panandi Kaoneka alishinda kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Halidi Makwega wakati wa mpambano wao Kaoneka alishinda mpambano huo mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
REFARII AKIMUONESHA MKONO JUU BONDIA SHABANI KAONEKA BAADA YA KUMDUNDA HALIDI MAKWEGA KWA POINT WAKATI WA MPAMBANO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PANANDI PANANDI ILALA BUNGONI DAR ES SALAAAM |
MABONDIA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO WA JUMAPILI KESHO
Mabondia Ramadhani Shauli kushoto na Cosmas Cheka wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika 27,10,2013 katika ukumbi wa frends Kona Manzese Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Cosmas Cheka akipima uzito uku Ramadhani Shauli akiangalia mpambano wao utakaofanyika 27,10,2013 katika ukumbi wa frends Kona Manzese Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Ramadhani Shauli akipima uzito uku Cosmas Cheka akiangalia kwa umakini mpambano wao utakaofanyika 27,10,2013 katika ukumbi wa frends Kona Manzese Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
bONDIA mOHAMED mATUMLA AKIPIMA aFYA KWA AJILI YA MPAMBANO WA KESHO |
Thursday, October 24, 2013
Tuesday, October 22, 2013
BONDIA WA UZITO WA JUU,Deontay Wilder KUPATA K,O YA 30 JUMAMOSI
![]() |
Deontay Wilder |
BONDIA asiyepigika duniani wa uzito wa juu 'heavyweight'
Deontay Wilder Mzaliwa wa Alabama, USA ambaye amecheza michezo 29 yote akishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na ya pili aliyejitaidi alifika raundi ya nne na kuambulia kipigo cha KO,
Mbaya sana katika raundi hiyo bondia huyo kwa sasa mwishoni mwa wiki hii atakuwa na kibarua kingine cha kusaka ko ya 30 atakapo pambana na Nicolai Firtha wa Ohio, USA
Katika mpambano wa raundi 10 utakaopigwa katika ukumbi wa Boardwalk Hall, Atlantic City, New Jersey, USA mpambano huo wa
Deontay Wilder wa 30 unaonekana kwa bondia huyo kuwa nyanya kwake kwa kotokana na rekodi ya mpinzani wake na yeye ni tofauti ingawa mpinzani wake amecheza mapambano mengi kuliko yeye
Saturday, October 19, 2013
TWARIBU MCHANJO AMGALAGAZA KELVIN MAJIBA
Bondia Twaribu Mchanjo kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Kelvin Majiba wakati wa mchezo wao uliofanyika gongolamboto mzambarauni Dar es salaam Mchanjo alishinda kwa point mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Twaribu Mchanjo kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Kelvin Majiba wakati wa mchezo wao uliofanyika gongolamboto mzambarauni Dar es salaam Mchanjo alishinda kwa point mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Twaribu Mchanjo akishangilia ushindi baada ya kumdunda Kelvin Majiba kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Emanuel Philomon kushoto akimtwanga makonde bondia Gaspar Hinde wakati wa mpambano wao philomon alishinda kwa K,O ya raundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Abdul Zugo kushoto akipambana na
Hassani Manula wakati wa mpambano wao uliofanyika Gongolamboto Dar es
salaa mpambano huo walitoka nguvu sawa yani ni Droo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MPAMBANO WA MTANZANIA SAID MBELWA SASA UPO KWENYE DVD
MPAMBANO WA MTANZANIA SAID MBELWA SASA UPO KWENYE DVD

Mtanzania Mbelwa alipocheza ngumi Afghanistan
*Pambano lawa gumzo katika nchi
KABUL
MTANZANIA Said Mbelwa, alipoteza pambano dhidi ya bingwa wa ngumi wa Afghanistan Hamid Rahimi, ambalo lilitazamwa na mashabiki wengi kwenye kwenye televisheni.
Pambano hilo la ngumi za kulipwa lilifanyika kwa lengo la kuhamasisha amani katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na vita, liliisha katika raundi ya saba baada ya Mbelwa kuacha kupigana kwa kudai ameumia bega.
Rahimi ambaye alizaliwa Afghanistan na kukulia Ujerumani na Mbelwa walitwangana kuwania ubingwa wa Mabara wa WBO uzani wa Middle.
HIlo ni pambano la kwanza la ngumu za kulipwa kwa Rahimi kulicheza katika nchi yake aliyozaliwa
Wakati mamilioni ya mashabiki waliangalia pambano hilo kupitia chaneli mbili za televisheni ikiwemo inamilikiwa na serikali ya Afghanistan yaRTA, mamia ya watu wakiwemo maafisa wa juu, wanasheria na mabalozi walijumuika katika ukumbi wa Loya Jirga mjini Kabul uliokuwa na ulinzi mkali kushuhudia pambano hilo.
Kiingilio cha pambano hilo kilikuwa dola 50 (zaidi ya sh. 75,000) na dola 100 (zaidi ya sh. 150,000).
Rahimi alipata ushindi raundi ya saba baada ya Mbelwa kudai ameumia shingo.
Akizungumza baada ya mechi, Rahimi alisema, " Mkanda huu si wangu, huu mkanda ni wa Afghanistan. Ni wenu. Ninawapenda," Rahimi alikuwa na furaha jukwaani aliwaambia mashabiki.
Pambano hilo lililopewa jina "Fight 4 Peace," (Pambano kwa Amani) lilikuwa tukio kubwa katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikipata maisha mapya niaa ya awali kuwa chini ya Taliban, awali ilionekana kama pambano hilo lingezuiwa.
Wataliban waliongoza nchi hiyo kati ya mwaka 1996 na 2001, na kuzuia raia wengi kushiriki katika shughuli nyingi za kijamii ambazo zinaonekana ni kinyume na Uislamu.
Uwanja mkubwa wa michezo uliopo Kabul, Ghazi ulikuwa ukitumika kwa kama uwanja wa kuwanyonga watu hadharani na kuwapiga watu waliotiwa hatiani kwa uhalifu katika miaka ya 1990.
"Nina uhakika hakuna mmoja kati ya (wapiganaji) wawili angethubutu kuingia nchini, kama Taliban wangekuwa bado wanaendelea. Nimesurahi sana kwamba sasa tunasonga mbele katika sehemu ambayo dunia inatutambua," Sayed Ahmad Peerzada, ambaye ni muuza duka ali.iambia Shirika la habari la Marekani, CNN.
Tukio hilo lilitawala katika vyombo vya habari vya kijamii ambapo watu wengi walikuwa wakiandika katika mitandao ya Twitter na Facebook kuonesha wanafuarahia kuwepo kwa mechi hiyo.
Tukio hilo lilimgusa hata Rais wa nchi hiyo, Hamid Karzai ambaye alitoa salamu kutoka Ikulu yake mjini Kabul kuwapongeza mabondia wote wawili.
"Rais, Mbalia ya kumpongeza Rahimi, anamshukuru mpinzani wake kutoka Tanzania ambaye alikuja Afghanistan kushiriki pambano hili," Taarifa kutoka ofizi ya Karzai ilisema.
Rahimi Alizaliwa Afghanistan mwaka1983 alitoroka kwenda Ujerumani akiwa na famiulia yake mwaka 1992 baada ya nchi yake kutawaliwa na vita ya wenywe kwa yenyewe.
Ana rekodi ya kushinda mapambano 20 kati ya 21.
DVD
ZA MASUMBWI SASA ZINAPATIKANA KIURAISI ZAIDI FIKA MAKUTANO YA BARABARA
YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO AU PIGA SIMU KWA KOCHA WA MCHEZO
Rajabu Mhamila 'Super D'
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
Thursday, October 17, 2013
SASA KALAMA NYILAWILA KUMVAA SADO PHILEMON NOVEMBA 3 CCM MWIJUMA
KALAMA NYILAWILA |
MPAMBANO wa masumbwi uliokuwa uwakutanishe kati ya Bondia Kalama Nyilawila na Sado Philemon uliokuwa uchezwe Oktoba 20 jumapili katika uwanja wa CCM Mwijuma Mwananyamala umeailishwa kutokana na kupisha mpambano wa watani wa jadi simba na yanga utakaofanyika katika uwanja wa taifa
akiongea mratibu wa mpambano huo
Ibrahimu Kamwe 'amesema mpambano huo umeailishwa kwa muda kupisha mchezo
wa simba na yanga kwa kuwa mashabiki wa mpira ndio hawo hawo mashabiki
wa mchezo wa masumbwi hivyo kwa sasa mpambano uho utafanyika Novemba 3
katika ukumbi uho huo mpambano huo uliokuwa uwakutanishe mabondia
mbalimbali wakongwe na chipkizi sasa utachezwa siku hiyo alitaja
mapambano ambayo yatakuwepo kuwa '
Mwaite Juma na Shadrack ignas , nae bingwa wa zamani wa bantam Ajibu salum atapimana ubavu na Martin
Richard,huku mbena Rajab akizipiga na
Godwin Mawe, Ibrahim class 'King Class Mawe ' atazichapa na Rashid
Ali, Hassan kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim chuma na Shaban Manjoly,
mdogo wake francis miyeyusho Yona
miyeyusho atacheza na julias Thomas,
Abdalla ruwanje na Bakari zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa
mwananyamala sokoni joseph stanslaus(amita
au jose mawe) na mbabe wa manzese sokoni
shaban seif(body kitongoji) pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa
mabondia hawa, nae yasin omari atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na
mapambano mengine kadhaa ya vijana
wadogo wenye vipaji vya mchezo wa ngumi.
Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR(peche
boy) atakaezipiga na ATHONY MATHIAS katika pambano la round nane
na SADO PHILEMON atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito
wa middle kutafuta mshindi wa
atakaezipiga na Thomas mashali katika pambano la ubingwa.kwa ufupi
mabondia
wote wapo katika hali nzuri na wametakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili
ya mpambano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika ukumbi wa ccm
mwinjuma
mwananyamala A
CHUGA BOY ALIVYO MSAMBALATISHA ISMAIL KAJIMA
Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' kushoto akipambana ya Ismail Kajima wakati wa mpambano wao uliofanyika Mbezi kwa Msuguli katika ukumbi wa Samunge Dar es salaam siku ya kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga boy alishinda kwa pointi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ismail Kajima wakati wa mchezo wao uliofanyika mbezi kwa msuguli ukumbi wa Samunge Dar es salaam wakati wa kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga Boy alishinda kwa point mchezo uho Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ismail Kajima wakati wa mchezo wao uliofanyika mbezi kwa msuguli ukumbi wa Samunge Dar es salaam wakati wa kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga Boy alishinda kwa point mchezo uho Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Chuga Boy akitangazwa mshindi wakati wa mpambano huo |
Bondia Julius Kisarawe akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Rogat Mkude wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya Idi Hal Haj katika ukumbi wa Samunge uliopo Mbezi kwa Msuguli Dar es salaam Kisarawe alishinda kwa point mchezo huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
KINYOGOLI AMKUMBUKA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
MWALIMU Julius Kambarage Nyerere kipindi yuko madarakani,
alipenda michezo kuanzia mashuleni hadi kwenye makampuni na mashirika
mbalimbali hapa nchini, ingawa alikuwa akipenda mchezo wa bao.
Aliweka sera bora ya michezo na kufanikisha
kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1967 na kutoa fursa zaidi kwa wenye
vipaji kuvionyesha.
Kinyogoli ni mwanachama wa klabu ya Simba lakini hahudhurii michezo ya timu hiyo, mapenzi yake
yanabaki kwenye ngumi.
Nyota yake ya michezo ilianzia shuleni,
Manerumango Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mwaka 1958, alicheza soka, ngumi na
riadha, aliendelea na mchezo wa ngumi kwa sababu ndio ulikuwa ndani ya damu
yake, michezo mingine ilimshinda kwa sababu ya hasira za baadhi ya wachezaji
pindi zinapotokea rafu.
Kinyongoli wakati alipokuwa akicheza, alikuwa
pia akitoa mafunzo kwa wenzake, mwaka 1966, katika klabu ya Magomeni Centre
yalipo makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni alimfunza Majuto Mahavu ambaye
baadae alikuwa tishio kwenye timu ya Taifa.
Mwaka 1970 alijitosa rasmi kwenye ngumi baada ya
kuvutiwa na Titus Simba aliyeiletea medali ya kwanza Tanzania ya Jumuiya ya
Madola iliyofanyika Scotland, ndipo na yeye akaongeza ufanisi zaidi katika
mchezo huo.
Mwaka 1971 aliajiriwa kiwanda cha Bora baada ya
kuonesha umahiri katika mchezo huo, akafanikiwa kumfudinsha ngumi, Marehemu Zakaria
Yombayomba, mwaka 1973 aliasisi klabu ya ngumi ya Urafiki akawaibua akina
Charles Mhilu ‘Spinks’, Habibu Mzungu, Lazaro Makarious, Kwelu Msinjili na
wengineo.
Mwaka 1972 alishiriki mashindano ya Olimpiki,
Munich Ujerumani walikwenda na akina Titus Simba, Robert Mwakosye, Bakari
Suleimani ‘Match Maker’, Said Tambwe katika mashindano hayo, mwanariadha Clever
Kamanga aliipa Tanzania medali ya shaba kwa mbio za umbali za mita 400.
Katika mashindano hayo, Kinyogoli alifanya
vibaya baada ya kukatika kwa mshipa wa mkono wa kulia katika mazoezi nchini
humo, mchezo wa kwanza wa Olimpiki alishinda kwa pointi nyingi dhidi ya
Mcambodia, mchezo wa pili alipoteza pambano baada ya kujitonesha mkono wake na
damu zikatoka nyingi.
Maumivu hayo hakuyaona hadi, Profesa Philemon
Sarungi wakati huo alikuwa akisoma nchini humo, alijitolea kuisaidia timu hiyo.
Mwaka 1973 alishiriki All Africa Games jijini
Lagos Nigeria akarejea na medali ya fedha na kuchaguliwa kwenye timu ya Afrika
iliyoshiriki Inter-Continental
iliyofanyika Mexico , uteuzi huo pia uliwahusu pia akina Jacob Mussa,
Bakari Suleimani, Titus Simba na Mbaraka Mkanga wakati katika soka Tanzania
iliwakilishwa na akina Maulid Dilunga, Abdallah Kibadeni na Kitwana Manara.
Mwaka 1974 alisisi klabu ya Simba ambayo kipindi
hicho ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Abubakar Mwilima baada ya kuchana
mkataba wa Bora, baada ya uongozi mpya wa kiwanda hicho kutokupenda michezo,
akaondoka na wenzake wote aliokuwa nao kiwandani hapo kama Bakari Suleiman
‘Match Maker’, YombaYomba na wengineo.
1976 akiwa kwenye kambi ya maandalizi ya
Olimpiki alitangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa, mwaka 1978 akaanzisha
klabu za watoto wadogo Simba Sports Klabu na kuendelea na Relwe Gelezani, Simba wakachipuka akina ukoo wa Matumla
Rashid,Haji,ali,hassani,Mazimbo, Mbwana,Karimu Matumla, wote hawo ni wa ukoo mmoja na kina Iraq Hudu Mkumwena, Remmy Ngabo, Joseph Marwa,Shabani Mhamila 'Star Boy' Iddy Hamisi 'Bowe' Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni msaidizi wake katika kuinuwa vijana chipkizi, Mohamed Chipota,Oscar Manyuka na wengineo.
Hivi sasa, Kinyogoli anafundisha klabu ya
Amana ya Ilala na akiendelea na Simba pia akiwa na changamoto nyingi ambazo
ni uwezeshwaji wake kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sababu ameutengeneza mchezo
huo tangu alipokuwa akifanya kazi na alitumia gharama zake lakini sasa, kazi
hafanyi na wadau wengi wa mchezo huo kuto mkumbuka kwa kutoa sapoti ya aina yoyote hivyo anatoa wito kwa wote pamoja na taifa zima kuwa yeye kwa sasa anapatikana Amana Ilala Dar es salaam hivyo anawaomba wadau wamsaidie angalau vifaa vya mchezo ili aweze kuenderea kuwanoa vijana wengi zaidi kama alivyofanya hapo nyuma kwa wanaoitaji kumsaidia kocha huyo wanaweza kumpigia simu 0655928298 au 0756928298
au zaidi wafike kumuangalia anavyo endelea kuinua vipaji vya vijana wengi kwa sasa pale Amana ukifika uliza MASTER KINYOGOLI kocha wa mchezo wa masumbwi nchini zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini
Rajabu
Mhamila 'Super D'
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
Tuesday, October 15, 2013
BONDIA LULU KAYAGE AJIFUA KWA KUZIPIGA NA FATUMA OMAR OKTOBER 26
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akiwasimamia mazoezi bondia Lulu Kayage na Amir Shekh wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya mazoezi Ilala iliyopa Amana Dar es salaam jana picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
BONDIA LULU KAYAGE BAADA YA KUMALIZA MAZOEZI AKIWA AMEPOZI |
Mabondia Amir Shekhe kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Lulu Kayage wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Amana Dar es salaam jana Lulu ana jiandaa na mpambano wake na Fatuma Omari utakaofanyika Oktober 26 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
PAMBANO LA KARAMA MAANDALIZI YA NGUMI YAKAMILIKA
Maandalizi ya mapambano ya ngumi
yanayotegemewa kufanyika katika ukumbi
wa ccm mwinjuma-mwananyamala ambayo
inawezekana yakavunja rekodi ya mapambano mengi kufanyika kwa mara moja kwa
mwaka huu kuliko mengine,kwani kuna zaidi ya mapambano 14 makali ya
utangulizi.hii itasaidia kwa wale watakaokuwa mpirani wa samba na yanga kuwahi
mapambano makubwa yatakayosalia ambayo
ni ya bondia mwenye ngumi za hatari na
mara nyingi huwazimisha wapinzani wake Zumba kukwe au chenji dola kama anavyojiita
mwenyewe wa kibaha atakae zipiga na Ali
boznia wa Tanga atakaefuatana na alan kamote na meneja wao ali mwanzoa
wakitokea mkoani tanga, mapambano mengine ni
Mwaite Juma na Shadrack ignas hii ni vita kali ya ulingoni wote sugu
wote wabishi kushindwa, nae bingwa wa zamani wa bantam Ajibu salum atapimana ubavu na Martin
Richard,huku mbena Rajab akizipiga na
Godwin Mawe, Ibrahim class na Rashid
Ali, Hassan kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim chuma na Shaban Manjoly,
mdogo wake francis miyeyusho Yona
miyeyusho atacheza na julias Thomas,
Abdalla ruwanje na Bakari zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa
mwananyamala sokoni joseph stanslaus(amita
au jose mawe) na mbabe wa manzese sokoni
shaban seif(body kitongoji) pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa
mabondia hawa, nae yasin omari atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na
mapambano mengine kadhaa ya vijana
wadogo wenye vipaji vya mchezo wa ngumi.
Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR(peche
boy) atakaezipiga na ATHONY MATHIAS katika pambano la round nane
na SADO PHILEMON ambae anategemewa kuwasili alhamis akitokea songea atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito
wa middle kutafuta mshindi wa
atakaezipiga na Thomas mashali katika pambano la ubingwa.kwa ufupi mabondia
wote wapo katika hali nzuri ya ushindani na wanategemea kupima afya zao na
uzito siku ya jumamosi saa nne asubuhi hapohapo katika ukumbi wa ccm mwinjuma
mwananyamala A
Subscribe to:
Posts (Atom)