Akizungumzia historia yake ya maisha ya ngumi bondia huyo alisema alianza kuupenda mchezo wa masumbwi tangu miaka ya nyuma akivutiwa zaidi na Rashidi Matumla ambaye alikuwa akifanya vizuri katika mchezo huo wa masumbwi hapa nchini
Ngange aliyezaliwa Oktoba 10 mwaka 1989 amesema noto zake ni kuwa bingwa wa unia wa mchezo wa masumbwi nchini kwani tangu aanze kucheza kumi ni miaka miwili iliyopita
ambapo alianza kufundisha na bondia Said Mbelwa nae kutoka kitongoji cha chanika ambaye ucheza mechi nyingi za nje ya nchi na kufanya atambulike kimataifa zaidi
Ngange ambaye ameshacheza michezo 8 kushinda 5 na kupigwa 3 alisema kuwa michezo ni ajira kubwa kwa vijana endapo watazingatia sheria na miiko ya mchezo huo kwani ina uwezo wa kukutoa kimaisha kama alivyo fanikiwa mwenzetu akimtaja bondia saidi mbelwa ambaye takribani kila mwezi uwenda ulaya kucheza mapambano ya ubingwa likiwemo lile la kulitakia amani nchi ya Afghanistan alipocheza za bondia Hamid Rahimi Oktoba 30,2012 wakati akigombea mkanda wa WBO Inter-Continental middleweight title
Ngange katika maisha yake ya kawaida yeye ni mpiga debe wa mabasi yanayokwenda chanika buguruni na bondia anakubalika na wapiga debe wenzie kuongoza amani kituoni kwako kwakuwa wao kwa sasa ni kioo cha jamii na wanakubalika na wananchi mbalimbali katika kitongoji hicho
bondia huyo ana kumbuka mmpambano mmoja ambao alicheza na Jonas Segu ambaye alimpa tabu sana na kupoteza mchezo huo kwa point daa nilikutana na kigingi yule jamaa anajua sana mana pale ningepogwa kwa K,O lakini nika jitutumua mpaka kumaliza nae mpambano wote kwa kuwa na mimi niliandaliwa vizuri na kocha wangu Rasta Banju ambaye ndio nipo nae mpaka sasa
na mafanikio yangu ya kufanya vizuri ulingoni ni kuwasikiliza makocha na kufuata wanacho kisema wao ndio na ukiongezea na mazoezi basi wewe utakuwa unaweza kudumu sana katika mchezo
hila kwa sasa natamani kupambana na bonia machachali awapo ulingoni anae nolewa na Kambi ya Ilala si mwingine kwa sasa ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jamaa anajua na ni mzuri sana awapo ulingoni ila na mimi nataka ajue kuwa wapo wanaojua kama yeye bondia huyo anae nolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa mwiba pindi anapo kutana na mabondia wenzie ulingoni
Bondia huyo amewaomba waau mbalimbali kujitokeza kuzamini mchezo wa masumbwi ili uendelee kuwa na hamasa nchini kutokana na watu wengi kuupenda mchezo huo
kwani ni ajili moja wapo kwa vijana endapo wadhamini wakienderea kujitokeza basi vijana wengi watakuwa na muhamko wa kupenda mchezo wa masumbwi nchini na kututangaza kimataifa zaidi
No comments:
Post a Comment