Tangazo

Pages

Saturday, July 6, 2013

KASEBA AINGIZA FILAMU YA BONGO MAFIA MTAANIBINGWA wa mchezo wa Kick Boxing nchini Chapion Japhert Kaseba ameingia katika fani ya utoaji filamu za mapigano Live akianzia na picha yake ya kwanza itakayo mtambulisha inakwenda kwa jina la Bongo Mafia

Filamu hiyo iliyo rekodiwa katika ubora wa hari ya juu sasa ipo mtaani Ikisambazwa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya wapenzi wa filamu nchini wajionee vitu tofauti kidogo kwani kuna wakali kibao alio washirikisha 
Picha hiyo ni mfululizo za picha zake nyingine ambazo zipo njiani kwani amekuja kufanya kazi katika jamii  ili watambue ipi pumba na upi mchele
Bongo mafia ilioshilikisha wasanii kama vile ,Dotnata,Kelvin,Muhogo Mchungu,Pendo Njau Champion na Rogers MASTER SHIVO,na Wasanii wengine kibao

Amesema filamu hiyo kwa sasa ni gumzoo mtaani wakati ndio kwanza inamaliza wiki moja tangu kuingia sokoni 

Kaseba ambaye hivi karibuni ali mdunda bondia Rasco Simwanza wa Malawi amejitamba kuendeleza ubabe  kwa mabondia wengine huku akifanya kazi zake za sanaa ambazo kwa kiasi kikubwa anamshukuru sana Dotnata kwa kuona kipaji chake hicho ambacho kilikuwa kimejificha na sasa kipo mtaani

Kaseba amesisitiza kwa mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua kazi hiyo kwani ndio kwanza ananza kulishika soko la filamu hapa nchini endapo wataendelea kumunga mkono na ndipo watakapofuraia kazi zake nyingi zilizopo jikoni kwani nina kazi tofauti tofauti Nne hivi na sijui nianze na ipi ndio mana nimeamua kutoa hii kwanza alisema Kaseba

No comments:

Post a Comment