Tangazo

Pages

Friday, July 26, 2013

FRANSIC MIYEYUSHO KUTWANGANA NA MZAMBIA

Miyeyusho akitia saini
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -MICHEZO.

BAADA YA MABONDIA WA TANZANIA KUWATWANGA MARA KWA MARA MABONDIA KUTOKA KENYA,NA UGANDA,

SASA ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA[[TPBO -LTD] KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI MAARUFU YA GLOBAL PUBLISHERS-LIMITED WAMEZINGATIA MAOMBI YA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI ,YA KUTAKA SASA WAALIKWE MABONDIA KUTOKA NCHI ZA K
USINI MWA AFRIKA HUKU WAKITAKA KUWAONA MABONDIA KUTOKA ZAMBIA AMBAO MIAKA YA NYUMA WALIWATINGISHA MABONDIA WA KITANZANIA ,

ITAKUMBUKWA KATIKA MIAKA YA NYUMA TANZANIA ILIKUWA IKIWAALIKA MABONDIA KUTOKA ZAMBIA ,AMBAO WALIWEZA KUTOA BURDANI NZURI ,HASA MASHABIKI HAO WAKIMTAJA BONDIA CHARLES LIBONDO [marehemu] AMBAYE ALIKUWA MWIBA MKALI KWA MABONDIA WETU WA TANZANIA , BONDIA HUYO LIBONDO ALIWAHI KULETA MAAFA MAKUBWA MIAKA HIYO YA NYUMA ,KWANI ALIWEZA KUMSABABISHIA  KIFO MTANZANIA -ANTHONI NDAKI KATIKA PAMBANO LAO LILILOFANYIKA JIJINI DAR-ES-SALAAM.

KUTOKANA NA MAONI HAYO YA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA, SASA BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO [chichi mawe]  AMEBAHATIKA KUWA BONDIA  WA KWANZA KATIKA KUFUNGUWA UKURASA MPYA KWA KUPAMBANA NA BONDIA DARIUS LIPUPA KUTOKA ZAMBIA KATIKA UKUMBI MAARUFU WA BURUDANI WA DAR-LIVE ULIOKO MBAGALA JIJINI DAR-ES-SALAAM HAPO SIKUKUU YA IDDI -MOSI.

MABONDIA HAWA WATACHUANA KATIKA UZANI WA FEATHER [kilo 57]  NA PAMBANO LAO LISILO LA UBINGWA NA LITAKUWA LA RAUNDI NANE [8]

TAYARI MIKATABA IMESHATUMWA NCHINI ZAMBIA ,NA KOCHA MAARUFU WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI ZAMBIA ANTHONY MWAMBA AMEHAKIKISHA KWAMBA BONDIA WAKE AMBAYE AMEINGIA KATIKA NGUMI ZA KULIPWA HIVI KARIBUNI BAADA YA KUCHEZA NGUMI ZA RIDHAA HADI KUIWAKILISHA ZAMBIA KATIKA MASHINDANO MBALIMBALI YA KIMATAIFA,KWAMBA ATAKUJA  KUWASHANGAZA WATANZANIA KWA KUMTWANGA MIYEYUSHO NYUMBANI KWAO NA MBELE YA WAPENZI WAKE..

PIA SIKU HIYO BONDIA HATARI KUTOKA MKOANI IRINGA CHUPAKI CHIPINDI [DOUBLE  C]   ATAONYESHANA UBABE NA BONDIA RAMADHANI KIDO KATIKA UZITO WA JUU ,NA KUTAKUWEPO PIA MAPAMBANO YA UTANGULIZI ,YAKIWEMO PIA YA AKINA DADA.

BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO NI BONDIA HATARI AMBAYE AMEJINYAKULIA SIFA NYINGI BAADI YA KUWATWANGA MABONDIA WAKALI WA NCHI HII AKIWEMO  BINGWA WA ZAMANI WA WBA INTERCONTINENTAL [MBWANA MATUMLA NA BONDIA BORA CHIPUKIZI WA TASWA 2011-2012 NASIBU RAMADHANI., NI BONDIA MWENYE WAPENZI WENGI SANA KOTE TANZANIA.

TPBO-LIMITED INAWASHUKURU SANA VIONGOZI WA GLOBAL PUBLISHERS KWA KUAMUWA KUJIKITA KATIKA KUUENDELEZA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA NA PIA TUNAWAUSIA MABONDIA WAACHE KUWA WABABAISHAJI NA WAHESHIMU MIKATABA WATAKAYOINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZINAZOJITOKEZA KUUBEBA MCHEZO HUU KWA FAIDA YAO.,PIA TPBO-LTD INAWATAKA MABONDIA WOTE WA NGUMI ZA KULIPWA KUZINGATIA MAZOEZI NA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA .


                                                       IMELETWA KWENU NAMI;-

                                           YASSIN ABDALLAH NWAIPAYA-USTAADH
                                                           RAIS-TPBO-LIMITED

No comments:

Post a Comment