Tangazo

Pages

Wednesday, March 13, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA MARCH 17 CCM TANDALESUPER D BOXING COACH
BONDIA Juma Fundi anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na Hassani Mandula katika mpambano wenye upinzani wa ali ya juu utakaofanyika


jumapili ya March 17 katika ukumbi wa CCM Tandale jijini Dar es salaam 

Akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mratibu wa mpambano huo Dikumbwaya Stamili amesema maandalizi yote yako sawa ikiwemo makubaliano ya mabondia kupanda ulingoni siku hiyo aliongeza kuwa mabondia wote watapimwa uzito na afya siku ya jumamosi katika ukumbi huo huo

Alitaja kuwa mapambano yatakayosindikiza siku hiyo ni Cosmas Kibuga atakaeoneshana kazi na Yohana Mathayo uku Ramahani Pido akioneshana ubabe na Faraji Sayuni pia kutakuwepo na burudani mbalimbali zilizoandalkiwa siku hiyo 


Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment