Tangazo

Pages

Tuesday, March 5, 2013

BINGWA WA NGUMI NA BINGWA WA KICK BOXER KUZICHAPA MACH 17




Bingwa wa kickboxing, Hamis Mwakinyo, anatarajia kupanda ulingoni kuzipiga na bingwa wa Taifa wa ngumi za kulipwa nchini uzito wa light weight kg 60, Said mundi, wa Tanga katika pambano la raundi nane.
SAIDI MUNDI KUSHOTI NA KING CLASS MAWE
Pambano hilo litakuwa ni maalum kwa ajili ya kusindikiza pambano la ubingwa wa mabara wa WBF kati ya Alan kamote na Jumanne Mohamed, litakalopigwa katika uwanja wa mkwakwani  jijini Tanga Machi 17, mwaka huu.
Hamis Mwakinyo ambaye ni bingwa wa ngumi na mateke afrika mashariki na kati wa  WKN-AFRIKA (World kickboxing Network- Afrika) na ameshawahi kuchalenji ubingwa wa dunia nchini iran, atazichapa na mpinzani wake huyo, ambapo pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa. 
Aidha pambno hilo limezidi kuwa gumzo midomoni  mwa mashabiki wengi wa mchezo huo, mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa muandaaji wa pambano hilo Promota, Ally Mwanzoa, amesema kuwa mabondia  hao tayari wameshakubaliana na kuridhia kutiliana saini  mkataba wa makubaliano wa pambano hilo.
Mwanzoa, alisema kuwa pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi kwa  mabondia kutoka sehemu mbalimbali za  Tanzania hususani  jijini Dar es salaam na anategemea kuongeza nguvu  za majaji wa mchezo huo kutoka nje  ya Tanzania ili  kuondoa malalamiko yeyote yanayoweza kujitokeza.

No comments:

Post a Comment