Tangazo

Pages

Monday, March 25, 2013

AMOUR MZUNGU AMTISHIA NYAU MARWA


Zungu (kushoto) wakati akipima ubavu na Kiza Kinene (kulia)
BONDIA machachari mwenye makazi yake kisiwani Unguja Amour Said”Zungu”  amejitapa kumpiga vibaya na kumstaafisha ngumi bondia mkongwe aliyewahi kuchukua medali na mataji kadhaa katika ngumi za ridhaa na kuwa bingwa katika ngumi zakulipwa Joseph Marwa katika  pambano litakalofanyika katika ukumbi wa  CCM Mwinjuma-mwananyamala April  7.
Zungu alisema kuwa kwa namna alivyojiandaa atamnyuka Marwa maarufu kama Smart Man'.
"Marwa umri umekwenda, japo alikuwa mwalimu wangu, lakini lazima nimnyuke," alisema.
Mabondia hao watapigana katika pambano la raundi nane na watasindikizwa na mabondia wanaokuja vema katika mchezo huo nchini kwa sasa kama Issa Omar na Shaaban Madilu watakaocheza raundi kumi za ubingwa wa taifa wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO),Ambao upo wazi kugombaniwa na mabondia hao. 
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment