Bonzo(63yrs)
akitoa nasaa baada ya kumpiga bondia chipukizi james martin(22)ambae
ni sawa na mwanae wa tatu.upande wa kulia ni Ibrahim kamwe na kushoto
ni Yasin Abdallah-Ustadh
Mohamed Bonzo(63) inasemekana ndio bondia mzee nchini atacheza siku ya iddi mosi.
Kampuni
ya Mwanzoa Promotions ya Tanga chini ya mkurugenzi wake Ally Ommar
inaendeleza mkakati wake wa kunyanyua vipaji vya wanamichezo wa jiji la
Tanga hasa katika mchezo wa ngumi kwa mapambano ya ubingwa wa Afrika
mashariki yatakayopigwa siku ya iddi mosi na iddi pili.
Ally
omar’Mwazoa’ akikimuhakikishia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini
Ibrahim kamwe”bigright” kuwa maandalizi ya mapambano yote yamekamilika na
mabondia wapo katika hali nzuri ya ushindani ambapo siku hiyo ya iddi
mosi katika ukumbi wa CCM HALL, Said mundi wa Tanga atazipiga na Habibu
pengo wa Dar es salaam.
Katika
kugombania ubingwa wa Taifa wa TPBC uzito wa super feather raundi
kumi,nae jumanne Mohamed wa Tanga atazipiga na ali bugingo wa Dar es
salaam uzito wa light weight raundi kumi,katika uzito wa super fly Haji
juma(Tanga) na Mwaite juma(Dsm) watacheza raundi nane na mapambano
mengineyo mengi ya utangulizi wa mabondia wa watakaotoka katika
vitongoji mbalimbali vya jiji la tanga.
Na
siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa la
ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga na
bondia toka Uganda ni pambano la raundi kumi pia zuberi kitandula wa
Tanga atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi kumi,jay
jay ngotiko wa tanga atapigana na bondia juma afande toka morogoro pia
kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia wakongwe wa
tanga na wale chipukizi takribani mabondia wote wa kulipwa wa jiji la
Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na matatizo binafsi.
mwazoa alimalizia kwa kusema hizi ni mbio za kuyakusanya
mataji yote ya Tanzania na Afrika mashariki yaje mkoani Tanga na tayari
mpaka sasa ina mabingwa sita wa Tanzania na mmoja wa Afrika mashariki.
No comments:
Post a Comment