Tangazo

Pages

Monday, August 6, 2012

CHEKA AUNYEMELEA UBINGWA WA DUNIA!



Bondia Francis Cheka
Shirikisho la Ngumi za Kulipwa na Chama cha ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) kipo katika mchakato wa kuidhinisha pamnbano la ubingwa wa mabara katia ya bingwa wa IBF katika bara la Arika Francis Cheka na bingwa anayeshikilia ubingwa wa mabara Benjamim Simon wa Ujerumani.

Nafasi ya Francis Cheka inakuja baada ya kutamba kwenye orodha ya viwango vya abara vya IBF tola mwaka 2011 kama ifuatavyo:

 January 2011: Alikuwa kwenye namba 15

February 2011: Alikuwa kwenye namba 14

March 2011: Alikuwa kwenye namba 14

April 2012: Alikuwa kwenye namba 13

May 2012: Alikuwa kwenye namba 13

June 2012: Alikuwa kwenye namba 12

July 2012: Alikuwa kwenye namba 11

August 2011: Alikuwa kwenye namba 10

September 2011: Alikuwa kwenye namba 7

October 2011: Alikuwa kwenye namba 5

November 2012: Alikuwa kwenye namba 6

December 2011: Alikuwa kwenye namba 6

January 2012: Alikuwa kwenye namba 6

February 2012: Alikuwa kwenye namba 6

March 2012: Alikuwa kwenye namba 5

ALIHAMIA UZITO WA SUPER MIDDLEWEIGHT BAADA YA KUWA BINGWA WA IBF AFRICA

 April 2012: Alikuwa kwenye namba 5

May 2012: Alikuwa kwenye namba 14

June 2012: Alikuwa kwenye namba 15

July 2012: Yuko kwenye namba 15

Licha kwa taarifa za uongo zilizotolewa n Issac Gamba kwenye kipindi cha Radio One (ambacho hata hivyo Radio One hawakutaka kunitafuta wakati wakijua kuwa mimi ndiye mkuu wa IBF hapa Afrika)  kwamba Francis Cheka hatambuliki na IBF mpambano huo unakuja wakati tayari watu wenye tamaa za kama fisi wameshachungulia dili na kuanza kutoa taarifa za uongo ili waambiwe kuwa wao ndio wametafuta pambano hili.

Njaa na tamaa hizo zitaliharibia taifa hili heshima kubwa kwani watu hao wanadai kuwa wanafanya hayo kwa msukumo wa Wizara ya Habari na Michezo  Ikuguatana na kipindi hicho kkilivhorushwa na rdio One leo tarehe 4 Agosti siku ya Jumamosi saa moja na dakika arobaini na mbili usiku kikirushwa na Issac Gamba akimhoji Emmanauel Mlundwa).

Mpambano huo wa Ujerumani unaandaliwa na Promota Eva Rolle ambaye ni mdau mkuu wa IBF nchini Ujerumani. Wote tulishiriki kwemney mmktano mkuu wa IBF/USBA katika jiji la Honolulu mwaka huu kuanzia tarehe 28 may hadi 3 June 2012. Cheka akishinda mpambano huu ataingia kwenye viwango vya dunia na hivyo kumweka kwenye nafasi nzuri ya kucheza ubingwa wa dunia.

Napenda kuwashauri waandishi wote wanaotaka kupata habari sahihi kuhusu IBF hapa Afrika na mahali pengine popote duniani wawasiliane na mimi kwa kutumia simu namba 0754-360828 au barua pepe ngowio@yahoo.com .

Mimi ndiye kiongozi MKUU wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi. Hivyo kama kweli unataka kupata habari sahihi za IBF na sio za uongo wa kutunga naomba tuwasiliane kwa simu pamoja na barua pepe hiyo hapo juu!
 
Imetolewa na: 
Onesmo A.M. Ngowi 
Rais, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa 
Bara la Afrika, mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi

No comments:

Post a Comment