Tangazo

Pages

Sunday, June 3, 2012

UNYANYASAJI WAMPELEKA GEREZANI MKALI WA 'MAWE' BONDIA MAYWETHER



Mayweather, akisindikizwa na Mwanasheria wake, Karen Winckler  (katikati) na rafiki yake 50 Cent , wakati akiingia katika Mahakama ya Las Vegas kusomewa hukumu ya kesi yake.
 Mayweather akifungwa pingu tayari kuelekea katika gereza la  Clark County, Detention Center Nevada.
 Sare na Yeboyebo atakazotumia Mayweather kipindi atakachokuwa gerezani.
*********************************************
KUTOKA LAS VEGAS, Marekani

NI saa 72 zimepita sasa, kati ya saa 2160 ambazo mkali wa masumbwi duniani Floyd Mayweather Jr baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo chake jela. 
Mkali huyo wa masumbi amelimwa hukumu hiyo ya kutumikia kifungo kutokana na vitendo vya unyanyasaji majumbani aliofanya miaka miwili iliyopita.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Mayweather, alimfuata mpenzi wake wa zamani, Josie Harris, hadi nyumbani,   na kumtandika makofi, kabla ya kushtakiwa na kukutwa na hatia iliyomtia hatiani na kuhukumiwa kifungo hicho kwenye gereza la Clark County Detention Center  Nevada.
Akisomewa mashtaka hayo, Bondia huyo alikiri kumkunja mkono mpenzi wake, Harris, mama wa watoto wake watatu, ambapo alikilri kosa lake na kuwa alitenda hivyo baada ya ushauri wa kisheria, ambapo kama angeendelea kubisha na baadaye kukutwa na hatia, angeweza hata kufungwa miaka 34 jela – jambo ambalo wanasheria wake walimuhadharisha mapema.

50 Cent azungumzia kifungo cha rafiki yake
Wakati alipofika mahakamani na kisha kumaliza taratibu za kimahakama tayari kwenda jela, Mayweather alikuwa mpole akilengwa na machozi, kitu kilichomfanya ashindwe kuongea chochote, haikuwa hivyo kwa swahiba wake 50 Cent.

"Ni hali ya simanzi kwa kila mmoja akiwamo yeye mwenyewe, lakini naamini atakuwa sawa tu," aliongeza 50 Cent akionekana kuelemewa na sikitikoto.

"Kila mmoja ana tafsiri tofauti katika stori ile ile," aliongeza 50 Cent, ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson III.

"Yeye ukilinganisha mgogo kati ya Mayweather na Harris uliochangia kuvunjika kwa ndoa yao ambapo watoto wao watatu walihusika. Harris na watoto wake wanaishi huko Kusini mwa California.

"Hakuna tofauti kwa kila mmoja kuelekea mchakato wa talaka kwa umpendaye," alisema rapa nyota huyo na kuongeza: "Na namna rafiki yako anavyoweza kugeuka kuwa adui yako mkubwa."

Ni siku ya nne sasa, kati ya siku 90 za kuishi maisha ya kifungo, ambapo atakapotoka jela atalazimika kufanya shughuli za kijamii zitakazomfanya atumie kiasi Fulani cha pesa. 

Anasubiriwa kwa hamu na mashabiki hapo Agosti 30, 2012 kuona kama atakuwa amebadilika kiakili, kimwili na kiroho kama alivyoahidi.http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment