Tangazo

Pages

Friday, June 29, 2012

BIG RIGHT KUWAZAWADIA MABONDIA WAKE ENDAPO WATASHINDA



 Kocha wa ngumi wa Kambi ya mazoezi ya Big Right, Ibrahim (katikati) akiwa na mabondia wake wakati akiwasimamia katika Kambi yao ya mazozi ya pamoja kama timu kujiandaa na mapambano yao yanayotarajia kufanyika Julai 15 katika Ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es Salaam, mwaka huu.
********************************************

KATIBU wa Vijana wa CCM Kata ya Kinondoni, Rehema Mbegu, ameahidi kutoa zawadi ya Baiskeli kwa Mabondo wa Klabu ya Mazoezi ya Big Right ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, iwapo watashinda katika mapambano yao yanayotarajia kufanyika hivi karibuni, ili kuwa moyo zaidi vijana kuupenda mchezo wa Masumbwi.

Rehema mbegu, mara kadhaa amekuwa akishirikiana na vijana wa Kata yake katika masuala mbalimbali ya Kijamii na ya kuendeleza michezo, ambapo amekuwa karibu zaidi na vijana wa rika zote na kuwapa sapoti kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri kujishughulisha na michezo zaidi ili kuepuka kutojiingiza katika mkumbo wa matumizi ya madawa ya kulevya.

Mabondia hao baada ya kuhakikishiwa zawadi nono ya kila atakayeshinda kuibuka na Baiskeli, wamezidi kuwa na morali zaidi na kutoa ahadi zao kwa Katibu huyo kuwa watafia ulingoni hadi kieleweke kwa kutupa mawe ya ukweli kwa wapinzani wao watakaokutana nao siku hiyo ya pambano.

Vijana hi wamekwishaanza kambi yao ya pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja kama timu chini ya Kocha wao, Ibrahim Bigright na kuongeza muda wa mazoezi ambapo kwa sasa wanafanya mara tatu hadi kwa siku.

Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele, kutoka Kambi ya Matumla, katika uzani wa fly weight, Mwaite Juma kutoka Bigright Boxing,ambaye atapigana mkongwe Anthony Mathias,  katika uzani wa Bantam.

Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa ni kati ya JUMA
FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo kutoka kambi ya mzazi
 
Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa

No comments:

Post a Comment