Tangazo

Pages

Sunday, June 17, 2012

PAMBANO LA MATUMLA NA MRUSI LAOTA MBAWA



DAR ES SALAAM, Tanzania
BONDIA wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana Kwa jina la ‘Siberian Tiger’ ameingia mitini yeye na kocha wake baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot na kuonyesha kumuofia mpinzani wake Rashid Matumla wa Tanzania.

Kwa mujibu Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa  Afrika(IBF)hii ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia huyo kuingia mitini kwa woga.
Ngowi alisema Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.

“Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani (WBU)alisema Ngowi na kuongeza akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali ya juu.


Alisema Matumla  amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni  ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi huyo.

“Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali, wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la ‘The Rumble on the Mountain’ na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini  Marekani Deidre Lorenz ambaye atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi Juni 24 mwaka huu”alisema Ngowi.

No comments:

Post a Comment