Tangazo

Pages

Friday, June 1, 2012

MABONDIA WA TANZANIA WAWEKWA KATIKA VIWANGO VYA KIMATAIFA


Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limewaweka mabondia wa Tanzania katika orodha ya viwango .

Mabondia hawa ambao watakuwa miongoni mwa mabondia 15 bora duniani katika uzito wao ni:

Francis Miyeyusho, Fadhili Ramadhani, Mbwana Matumla, Seba Temba, Allan Kamote, Pascal  Bruno na Francis Cheka.

Katika kikao cha Kamati ya Viwango (Ratings Committee) ambacho kilikaa jana chini ya Uenyekiti wa William James, IBF/USBA iliridhishwa na viwango vya mabandia wa Kitanzania na kutoa ahadi kuwa watawaangalia kwa karibu zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili kuwaongeza katika orodha ya viwango.

Hii ina maana kuwa mabondia hao waliowekwa kwenye orodha ya viwango vya IBF vya mabara wanaweza kupigania ubingwa wa IBF wa Afrika na mabara wakati wowote.

Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba ya Uajemi iliwakilishwa kwenye kikao hicho na Rais wake Onesmo Ngowi toka Tanzania. Katika vikao hivi vya viwango ni Marais wa mabara na viongozi wakuu wa IBF wanaohudhuria peke yao.

Ngowi aliwapendekeza pia mabondia kadhaa wa Kenya, Uganda, DRC, Afrika ya Kusini, Namibia, Zimbabwe, Mali, Gabon, Benin, Bukina Faso, Ghana, Nigeria, Morocco, Cameroon, Ivory Cost, Tunisia, Misri, Dubai na Jordan.

Kumekuwepo na uchakachuaji mkubwa wa rekodi za mabondia katika bara la Afrika kwa mapromota na mawakala wa ngumi kuweka viwango vya mapambano ya uongo katika rekodi za mabondia wao kweney mtandao wa Boxrec. Hii inawapa wakati mgumi sana mabondia wa Kiafrika kupata mapambano ya ngumi ya kimataifa.

Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi inaongozwa na rais wake Onesmo Ngowi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment